Jumanne, 8 Oktoba 2013

SAA YA UFUFUO NA UZIMA; ENEO JIPYA ARUSHA, UPAKO MARADUFU MKUTANO UFUFUO





Mara baada ya shughuli ya takribani siku kumi kumalizika kwenye viwanja vya relini jijini Arusha, sasa saa ya ufufuo na uzima imehamia Engo Sheraton, ambapo kuna uwanja umekabidhiwa kwa ajili ya shughuli ya kuendelea kumuaibisha shetani aliyekuwa anawatesa wakazi wa jiji hili na vitongoji vyake.


Gospel Kitaa ambayo ilifika eneno hilo na kushuhudia maelfu ya watu, ambao walipata fursa ya kufundishwa kuhusu nyota, na kisha mchungaji kiongozi Gwajima kuombea pamoja na kuwekea mikono, kama ambavyo alikuwa akitamani kwa muda mrefu kumfikia mtu mmoja mmoja.


Zifuatazo ni badhii ya picha ya siku ya jana, ambayo ni ya kwanza kwa eneo hilo jipya, hakika kwa namna umati ulivyofika hapo, ni dhahiri kuwa watu bado walikuwa na kiu ya uponyaji na kujuzwa zaidi kuhusu ufalme wa Mungu na utendaji wake wa kazi kupitia watumishi wake.


Kama hujapata fursa ya kufika eneo hili ambapo huenda Ufufuo na Uzima Mega Church Arusha ikaanzia hapo, basi fanya hima upate kusikia mafundisho mbalimbali ikiwemo kuhusu ndoto, kafara ya damu, nyota, na hata namna ya kufufua wafu.


Mchungaji Gwajima akifundisha madhabahuni.



Hwakuwa na hamu ya kukalia viti, ila walitaka kuwa karibu na madhabahu waone kinachoendelea bila chenga.



Dawati la habari. Geofrey (kushoto) akipambana na lens wakati Davie akihakiki sauti ya mahubiri kwenye mtandao, ilhali Amoure (kofia nyekundu) na Baraka (kulia) nao wakiwajuza watu kinachoendelea kupitia mitandao ya kijamii.



Sehemu ya waliohudhuria








Mwenye simu na alirekodi



Simu zikiwa bize kunasa matukio ya sauti kwa ajili ya kumbukumbu


Kama kawaida hapitwi mtu
























Muonekano wa juu wa mahudhurio ya siku ya kwanza viwanja vipya





























Hakuna maoni:

Chapisha Maoni