Jumatatu, 7 Oktoba 2013

KANISA LA MITO YA BARAKA WAMSHUKURU MUNGU KUWA NAO KILA HATUA


New Jerusalem Choir, kwaya ambayo Silas Mbise wa GK anaiwajibikia pia.

Kanisa la EAGT Mito ya Baraka limemshukuru Mungu kwa mengi ikiwemo kuwavusha kila kunapokuwa na matatizo, kutimiza ahadi zake, na kuendelea kuonesha ukuu wake juu ya yale wanayoyahitaji, ambapo siku hiyo iliambatana na chakula cha pamoja.

Ni miaka 10 tokea Mito ya Baraka ianze, ambapo zamani ilikuwa ikiitwa kanisa la Mnazi Mmoja, na kisha kama likapotea tena kabla ya kurejea kama Mnazi Mmoja Mpya chini ya Askofu Bruno Mwakibolwa, na sasaa Mito ya Baraka.

Ahadi anazosema Mungu na kweli zinatimia, Nguvu Mpya, Mito ya Baraka watu wanapokea, ikiwemo Neno la Bwana juu yao kila mwaka, ambapo 2010 ilikuwa Nimesikia maombi niko pamoja nao, mwaka 2011 ulikuwa mwaka wa vurugu, na kweli ikashuhudiwa hivyo kuanzia Misri na kwingineko, kisha 2012 ukawa mwaka wa mema yote, na kisha 2013 ukaitwa mwaka wa mabaya - ila ukiwa na Mungu atakuinua.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za siku hiyo kama ambavyo Gospel Kitaa ilikuwepo na kujumuika pamoja na watumishi wa Mungu kanisani hapo.


Upendo Kilahire akimsifu Mungu madhabahuni.




Zamu ya Rhema Singer's, nao wakaimba pia


Baadhi ya washirika waliokuwa wakitoa sadaka ya shukurani, mzee wa kanisa akiwa na kipaza sauti kumshukuru Mungu.





Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya, Ruth akiwajibika kwa Yesu.



Muda wa picha za makundi makundi pamoja na kuondoka


Taswira ya nje mara baada ya kujumuika pamoja.


Askari Polisi ambao wana jukumu la kulinda makusanyiko wakishuhudia na kusimamia watu waondoke kwa amani.


Tukutane tena mwakani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni