Jumatano, 30 Oktoba 2013

BARAZA LA MAKANISA KENYA LAUNGA MKONO VIONGOZI WA MAKANISA KUKABIDHIWA BUNDUKI KUJILINDA


Katibu mkuu wa Baraza la makanisa nchini Kenya NCCK mchungaji Peter Karanja. ©Dailynation.
Watu mbalimbali nchini Kenya wakiwemo waumini wa dini ya Kikristo wamepinga wazo lililotolewa na viongozi wa dini hiyo kwamba wakabidhiwe bunduki aina ya AK47 ili kupambana na waumini bandia wa dini ya kiislam nchini humo ambao wamesababisha kifo cha mchungaji pamoja na kuchoma kanisa huko mkoani Mombasa nchini Kenya.Wakizungumza kwa nyakati tofauti kupitia mitandao ya kijamii watu hao wametaka serikali kutokubali maombi yao badala yake wazidishiwe ulinzi majumbani pamoja na sehemu zao za ibada. Akizungumza huko Kaloleni Mombasa wakati wa maziko ya mchungaji Charles Mathole wa RCG aliyeuwawa kwa kupigwa risasi kanisani mijini Mombasa, mchungaji Lambart Mbela wa kanisa hilo aliiomba serikali ya Rais Uhuru Kenyatta na mwenza wake William Ruto kuwakabidhi wachungaji na viongozi wa dini ya kikristo silaha aina ya AK47 ili kupambana na waislamu bandia wanaoharibu hali ya hewa nchini humo.

"Wachungaji, maaskofu na viongozi wote wa Mombasa tumeona sasa yatosha kuendelea kunyanyasika na hali hii kutoka kwa waumini bandia wa kiislamu ambao wanaua wachungaji wakati wa maandamano, wanachoma moto makanisa, hebu serikali tupeni haki ya kumiliki AK47 kwakila mchungaji, askofu na viongozi wa kanisa ili kupambana na waumini hawa bandia, kwa kujilinda, kuwalinda waumini wetu na makanisa yetu na mali zetu maana maisha ya wachungaji yapo hatarini, sasa tunaomba tukabidhini tuwafundishe kazi kwamba kanisa ninani". amesema mchungaji Lambart Mbela

Wakati huohuo baraza la makanisa nchini Kenya NCCK tofauti na matarajio ya wengi, limeunga mkono ombi la viongozi wa dini hiyo mjini Mombasa yakukabidhiwa silaha hiyo kutokana na viongozi hao kuona silaha hiyo itakuwa muafaka kwa ulinzi wa maisha yao, waumini na mali zao.

Taarifa zaidi kuhusu uamuzi uliotolewa na baraza hilo tazama video hii kwa mujibu wa KTN Kenya.

Maoni 1 :

  1. Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,

    Kwaheri Gerd Ulrich

    JibuFuta