Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 10 Machi 2015

WAPENDA MIUJIZA MAKANISANI, HII IMEWAPATA WENZENU

Hakika muyaonapo haya jua kwamba ule mwisho umekaribia… habari hii ya kusikitisha ni taa nyekundu kwa wakristo wote wanaotafuta miujiza ya watoto ama utajiri kwa kuhama hama makanisa yao kwa madai ya kutafuta neno la Mungu..

Wanawake na mabinti waliopewa mimba na nabii huyo.

Huko nchini Nigeria wanawake zaidi ya 20 wakiwemo wake za watu na mabinti wamepachikwa mimba na "nabii" wao ambaye amedai aliambiwa na Roho mtakatifu kufanya nao mapenzi wanawake hao. Nabii huyo alifahamika kwa jina la Timothy Ngwu ambaye ni mchungaji kiongozi wa kanisa la Vineyard Ministry of the Holy Trinity huko Enugu tayari anashikiliwa na jeshi la polisi la jimbo hilo kwa kosa la kuwalazimisha kufanya nao mapenzi na wanawake hao.


Mchungaji huyo amedai anatii wito wake wa kinabii na kiroho alioitiwa na kufanya sawa na mapenzi ya Mungu kwa kuwapa mimba yeyote yule aliyechaguliwa na kuwekwa wazi na Roho mtakatifu bila kujali kama mwanamke huyo ameolewa ama la alisema msemaji wa jeshi la polisi Enegu kamanda Ebere Amaraizu akitoa taarifa kwa vyombo vya habari na kudai kwamba mwanamke akijifungua mtoto hubakia kwenye huduma hiyo na mzazi wake


Taarifa kutoka kwa familia za mchungaji huyo zinasema mkewe aitwaye Veronica Ngwu ambaye alichoshwa na tabia ya mumewe hasa alipompa ujauzito mdogo wake na kuamua kumripoti Polisi. Kwa upande wa kaka wa mtuhumiwa ambaye hakutaka jina lake lifahamike ameiambia Vanguard report kwamba amekuwa akimuonya kaka yake juu ya tabia yake kwa muda mrefu lakini hakutaka kusikiliza, amesema gadhabu ya Mungu imeshuka juu ya kaka yake.

"Ngoja niwaambie hasira ya Mungu imemshukia kaka yangu tumekuwa tukimuonya kila siku kuacha alichokuwa akifanya amejaza boma letu kwa kuzaa watoto bila uangalifu na kutuambia tunamuonea wivu kwasababu anafanya maagizo ya Mungu" alisema kaka mtu na kuongeza kwamba angalia majengo yote ya kanisa ameyageuza kuwa ya kwake kwa jina la huduma yake, alimfukuza mkewe wa ndoa waliyezaa naye watoto watatu na kuanza kuwajaza mimba wake za watu na mabinti wadogo, we angalia boma lote limejaa watoto wa jinsia zote alilalamika kaka huyo.

Aidha kaka huyo amesema waumini wote wa kanisa la kaka yake ni wapumbavu kwasababu mwanamke hawezi kumuacha mumewe na kwenda na mwanaume mwingine kwa kisingizio cha kwenda kumuabudu Mungu na kufanya zinaa, na kudai hawezi kujiingiza katika tatizo hilo, "Vero amefungua msaada kwa wamama hao ngoja wayamalize na polisi ila nataka huduma hii ifungwe kabisa" alisema

Ngwu ameiambia NaiJ kwamba kaka yake ana wake wapatao watano na watoto 13 pamoja na wake za watu kwa madai ya kufuata mapenzi ya Mungu. Amedai hajawahi kufanya mapenzi na wake za watu ila amefanya hivyo endapo waume zao wamekubaliana na ombi la Roho mtakatifu. Calista Omeje na Assumpta Odo ni wanawake ambao waliawaacha waume zao ili kuishi na nabii huyo kwakuwa ilikuwa ni upako wa kinabii wa mchungaji huyo.


Calista ambaye ana watoto 10 na mumewe alipewa mimba na mchungaji huyo ila mtoto alikufa, amesema mwanamke huyo alimkabidhi mchungaji huyo binti yake huku Odo naye amesema mchungaji huyo amempa mimba yeye na binti yake.


Chanzo ni Wilfredasuquo
- See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2015/03/wapenda-miujiza-makanisani-hii.html#sthash.MeRl5fwF.dpuf

Jumanne, 7 Oktoba 2014

Biblia inasemaje juu ya kutoa fungu la kumi ama Sadaka ya Michango ?

Hawa ni wataalamu wa injili kwa watu wote GFAP wakiwa katika picha ya pamoja huko ROMBO KILIMANJARO

Jibu: Kutoa fungu la kumi ni jambo ambalo wakristo wengi hung’ang’ana nalo. Katika makanisa mengine kutoa fungu la kumi imesisitizwa kupita kiasi. Wakristo wengi pia hukataa kutii agizo la kutoa sadaka kwa Bwana. Kutoa fungu la kumi au sadaka inahitajika kuwa ni kitendo cha furaha na baraka. Lakini sivyo katika makanisa ya sasa.

Kutoa fungu la kumi ni agizo la agano la kale. Hili lilikuwa sharti la kila mwenye kupata zao au mfugo alete sehemu ya kumi ya pato hekaluni (mambo ya walawi 27:30; hesabu 18:26; kumbukumbu la torati 14;24; mambo ya nyakati ya pili 31:5). Wengine huchukulia ya kuwa fungu la kumi, katika agano la kale ilikuwa kama sehemu ya ushuru uliokuwa ukitolewa kwa ajili ya makuhani na walawi. Agano jipya haiamrishi wala kupendekeza mfumo halali wa kutolea fungu la kumi. Paulo asisitiza kuwa waumini watenge sehemu ya mapato yao kwa ajili ya kusimamia kanisa (wakorintho wa kwanza 16:1-2).
(1 Wakorintho 16 : 1-24
16.1 Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi
fanyeni vivyo.
16.2 Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili
kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;)

Agano jipya halielezi kiasi cha pato ambacho ni kitengwe kwa ajili ya kusimamia kanisa. (wakorintho wa kwanza 16:2). Kanisa la kikristo leo limechukua kile kiwango cha fungu la kumi kutoka kwa agano la kale na kukisisitiza kuwa ndicho kiwango cha chini cha mkristo kutoa. ijapokuwa agano jipya haitoi kiwango cha kutoa, inaelezea umuhimu na manufaa ya kutoa.

Ni watoe sawa na uwezo wao “ kulengana na pato lake.” Wakati mwingine ina maana ya kutoa zaidi ya fungu la kumi,

 Yote hutegemea uwezo wa mkristo mwenyewe na mahitaji ya kanisa. Kila mkristo sharti aombe na kutafuta hekima kutoka kwa Mungu juu ya swala hili (Yakobo 1:5). “ kila mtu niatoe kile alicho azimia kutoa kutoka ndani ya moyo wake, si kwa manung’uniko wala kulazimishwa, kwa kuwa Mungu hupenda kwenye kutoa kwa moyo mkunjufu” (wakorintho wa pili 9:7).

Pia hilo andiko nalipeleka kwa wale watumishi wa MUNGU wanao wapangia watu kiasi cha kutoa hususani kwenye michango,hakika jambo hili sio jema kwani kutoa kwa Toka KWA BWANA na haipendezi kumpangia mtu atoe nini bali kama alivyo sikia MOYONI mwake.

Pia katika makanisa ya leo usipo toa wanakuona kama mtu asiye endana nao yaani ajenti au msaliti hili sio sahihi kwani mtu kama mimisiwezi kutoa bila kusikia kwa hiyo hata msisitizo wakibina damu huwe mkubwa kiasi gani ni lazima nisikie kwa BWANA ama sivyo utakuwa tuu ni mchango na haifai kutoa kisha kunung'unika.

Siku njema na endelea kuetmbelea www.mwanakondooinjili.blogspot.com

USUHUDIAJI WA MTU KWA MTU KANISA LA TAG VCC ARUSHA

NA mama Mcungaji CATHERINE MBUGHI
Kushoto ndie mama Mchungaji Catherini Mbughi akisisistiza jambo la MUNGU katika jukwaa la Injili na kulia ndie Baba Mchungaji Aloice Mbughi.Picha na Makitaba.

Ninayo furaha ya hali ya juu kukukaribisha ewe msomaji wa blogu hii ya www.mwakasegeinjili.blogspot.com katika ujumbe huu wa leo kama ulivyotolewa kwenye kanisa la VCC na huyo mtumishi wa MUNGU kwenye mafundisho ya asubuhi ya wanafunzi na maandiko.

Ninae kuandikia ujumbe huu na kukuletea ni mimi OSCAR SAMBA na moja kwa moja tuzame kwenye somo letu la leo ambalo linalenga kukutia moyo wewe uliye okoka kuhusu kuwashuhudia wengine.

Luk 10:23-26
10.23 Akawageukia wanafunzi wake, akasema nao kwa faragha, Heri macho yaonayo mnayoyaona ninyi.
10.24 Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona
ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.
10.25 Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi
uzima wa milele?
10.26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?

Mpendwa kumbuka kuwa Inatupasa kuwashuhudia watu wote, Yohana 3:16, 3.16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu
amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.                    

,Unapo mshuhudia mtu msome NENO la Mungu kwani ndio silaa yetu na haikupasi kwenda vitani bila silaa.
Yohana 14.15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.Mpendwa andiko hili yatupasa kuhakikisha ya kwamba tunalishi hili kama kweli tunalipendana, kwa kuanza kushuhudia, na hii sio amri tuu bali pia ni agizo kuu.

Waambie ya kwamba mshahara wa dhambi ni mauti wala usiwafiche waeleze kuhusu jehanamu na pia wakumbushe uzuri wa mbinguni na waambie mbingu ipo kwa ajili yao tuu kama wakiamini.

Ukisha maliza muulize je, upo tayari kumapa YESU maisha yako akisema ndio muongoze sala  ya toba na akisema laa mulize na sema nae kuhusu hatima ya maisha yake nakumuliza je, anafahamu nini kuhusu hatima ya maisha yake baada ya kufa,mkumbushe kwa herufi KUBWA na msisitizo kinywani kuwa ni hukumu na hukumu yake MUNGU ni ya HAKI.

Mpe mfano wa tajiri na Lazaro kwani mara baada ya kifo kila mmoja alivuna alichopanda, Lazaro mbinguni tena kifuani mwa Ibrahimu na Tajiri motoni.

Hakika kupitia NENO la Mungu inawezekana kuwafanya watu kuingia mbinguni.Maandiko tuliyoyasoma hapo juu yanatutaka tuwapende jirani zetu kama Nafsi zetu pia “1 YOHANA 4-20-21   4.20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana
asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
4.21 Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.
Kwa hiyo yatupasa kutimiza andiko hili kwa Moyo wote kwani upendo wa kweli kwa Mungu wetu huanza kwa kumpenda jirani yako na upendo wa kweli kwa jirani yako uliyo na matendo ni kumwambia habari za YESU.

Weka mpango na mikakati yakuhakikisha yakwamba ndugu zako na rafiki zako wanaokoka,usikubali waende huko kwani kunatisha mnoo.
Mliliye YESU nasema nae kuhusu ndugu na jamaa zako lakini pia toka ka’a waambie hao watu ya kwamba YESU anaokoa.

MAMBO MUHIMU
1.Uwe na huruma ya KIMUNGU ndani yako,hakikisha unaguswa na tabu zao na mateso yao
2.Uwe na upendo wa MUNGU ndani yako YOHANA 3:16
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu
amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Usikubali juma hili lipite bila kuwaambia habari za YESU,ukikutana nae njiani ama popote pale mwambie YESU anampenda.Hata kama hataokoka leo lakini hakikisha unampandia NENO.
Upendo unagarimu,upendo unahitaji kujitoa kwa hiyo hakikisha unaingi gharama kwa kusugua goti ili watu waende mbinguni.Litumie NENO kwani hili NENO linauwezo wa kumuokoa na kumbadilisha kumbuka IMANI huja kwa kusikia kwa mantiki hiyo hilo NENO huweza kufanyika uponyaji kwake.
Kuna vilio vya aina mbili cha kwanza—ni cha mtu aliyeomba maji akiwa Jehanamu na B yake ni cha mtu aliyeomba ndugu zake wasiende jehanamu.
Luka 16:19-31
“16.19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula
sikuzote kwa anasa.
16.20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
16.21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata
mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
16.22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye
akafa, akazikwa.
16.23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali,
na Lazaro kifuani mwake.
16.24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake
majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
16.25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika
maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
16.26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku
kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
16.27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
16.28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
16.29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
16.30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
16.31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.”

Embu jiulize angalikuwa ni ndugu yako yuko huko jehanamu ungali jisikiaje ?
Na kilio chapi ni cha mtu uliyemshuhudia na kukataa kuokoka..
Zingatio kuu la somo la leo : TUKIKOSA HURUMA HATUTA VUNA
Naam hadi kufikia hapo ndio mwisho wa ujumbe huu tafadhali endelea kutembelea blogu hii ya www.mwakasegeinjili.blogspot.com kwa makala na habari zaidi.Pia kumbuka siku chache zijazo blogu hii itakuwa na na jina jingine ambalo ni www.ukombozig.blogspot.com na kwa sababu zaidi soma habari iliyopita.


Alhamisi, 25 Septemba 2014

KUHUSU LAANA (MAKALA)

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI JACKLINI AKIMTUKUZA MUNGU KATIKA MKUTANO WA INJILI WA GFAP ULIOFANYIKO HUKO ROMBO MKOANI KILIMANJARO JUMA LILOPITA.

KUHUSU LAANA (Kupakua/Download bonyeza link ifuatayo:
Katika waraka huu tunataka kuangalia juu ya wazo hili la “laana” itokanayo na mambo yaliyopita. Tunataka kuangalia, iwapo laana ya mtu binafsi au itokanayo na vizazi vilivyopita, inaweza kuwafungia wakristo ndani ya vifungo na kuwazuia kutokana na kupokea baraka za Mungu na Urithi wao katika Kristo. Kuanzia hapa mwanzoni mwa makala hii, hebu tuweke wazi kabisa kuwa hapa tunaongelea kuhusu mtu ambaye amehukumiwa kwa tendo la dhambi zake, akatubu na kugeuka kutoka katika dhambi zake, na akamwamini Bwana na Mwokozi Yesu Kristo kwa ajili ya wokovu wake, amezaliwa mara ya pili na kujazwa Roho wa Mungu, ameingizwa katika Agano Jipya ndani na kupitia Yesu Kristo. Hapa, kwa mtu huyo, hakuna zaidi! Hakuna kitu kilicho pungua na kwa wakristo kama ilivyoelezwa katika Agano Jipya, kuwa wakristo wa aina hiyo kama mitume walivyokuwa wakiwaandikia.

Ushahidi wa Agano Jipya

Ni kitu gani basi ambacho mitume wamewaandikia wakristo katika Agano Jipya? Wanayashughulikiaje mambo yanayojitokeza katika makanisa na watu wa Mungu? Wanayatambuaje matatizo hayo na wanatoa ushauri gani na maelekezo yapi kwao? Kwa mafundisho yoyote yale mapya, ambayo yanatoa ushauri na maelekezo yanayohusiana na wakristo, ni lazima mafundisho haya yasimamie katika misingi au yapate kuungwa mkono na maandiko ya mitume au kutoka katika mafundisho ya Yesu mwenyewe.

Kwa hiyo basi, mitume wanasemaje juu ya mafundisho yahusuyo wazo hili la “laana” zilizopita, kwamba zinaweza kuzuia maisha ya wakristo, au ya kanisa au nchi isipate kuendelea! Kwa kweli mitume hawasemi chochote kile, hakuna chochote wasemacho. Hakuna; na halikadhalika, hakuna hata mstari mmoja wa Neno la Mungu unaosema chochote kile! Wala mitume hawajaribu angalao kutamka au kugusia juu ya jambo hilo. Akili zao haziwapi kufikiria kabisa juu ya jambo hili. Yako wapi basi mausia yao wanayoyatoa kwa wakristo katika kuchunguza maisha yao ili kuhakikisha na kuwa makini sana, kwamba laana haitendi kazi yake wakati wanapokuwa katika shida ndani ya mienendo yao binafsi na kiroho? Mausio ya aina hiyo hayapo kabisa. Ni kweli kwamba Mtume Paulo anazungumza kuhusu laana, lakini anaizungumzia katika mtindo wa tofauti kabisa – yaani, anazungumzia kuhusu Kristo “akitukomboa kutoka katika LAANA ya sheria”. Tunakuja kuangalia kwa makini kuhusu jambo hili baadaye kidogo, lakini, hakuna sehemu yoyote ile ndani ya Agano Jipya lote, ambayo hata kutajwa tu kwamba laana kutoka katika mambo yaliyopita au kwamba inaweza kuzuia mwenendo wa kiroho wa mkristo au kanisa au Taifa.

Lakini sasa, sisi tutoe sababu gani tunapoona jambo hili liko kimya katika Biblia? Mafundisho hayo ya kisasa au mapya yako wazi sana na yametiririka kwa undani sana na kwa kuwa ni hivyo, basi bila shaka yangepasa kuwakilisha sehemu muhimu sana na ya lazima katika ukombozi wetu katika huyo Kristo Yesu; ikiwa jambo hili kama lingekuwa lina ukweli wowote ule.

Vitabu vingi sana vimewahi kuandika kuhusiana na jambo hili la laana, basi bila shaka, kwa hakika tungetegemea kupata misingi fulani ya mitume na ya kibiblia ndani ya mafundisho yao hayo mapya. Lakini basi, kwa nini hakuna hata mtume mmoja ndani ya Biblia anayejaribu kulitaja jambo hili katika nyaraka zake wanapoyaandikia makanisa? Je, wao walikuwa ni wajinga kiasi kwamba wameshindwa kuelewa umuhimu wa ukweli huu? Ikiwa ni hivyo basi, wao wanahusika katika kuwaacha ndani ya ujinga huo, sio tu wakristo wa vizazi vingi vijavyo, na kwa hiyo kuwazuilia uhuru wao katika Kristo. Kama ni hiyo, basi mitume wamewaachia umati mkubwa wa watu katika vifungo na giza kupitia katika karne nyingi kwa sababu ya kushindwa kwao kupokea na kufundisha mapokeo haya? Bila shaka yoyote ile, kulikuwepo na uzinzi na mila mbaya nyingi nyakati za Agano Jipya. Kwa hiyo, kwa nini basi, hawa mitume hawakuwaonya watu wa Mungu, ili wafahamu kwamba tatizo lolote lile mnalopata linatokana na laana iliyowatangulia? Kwa nini basi hawakusihi ili kuchunguza maisha yao ili waone iwapo wao wenyewe au mababu zao kama watakuwa wamehusika katika matendo ya kiShetani ambapo wengi wao wangeweza kuwa hivyo, na hivyo wangefanya hima kutubu na kuungama mambo hayo na kisha kutangaza uhuru wao katika Kirsto? Ni wapi ambapo wanashauri kufananishwa na mtu binafsi, kanisa au nchi? Ikiwa mambo hayo ni ya ukweli, basi, hilo sasa ni tatizo kubwa sana.

Hatuwezi kuachwa katika ujinga wetu, wala hatuwezi kuachwa katika vifungo! Lakini cha ajabu ni kwamba, jambo hili la laana ya mababu halitajwi mahala popote pale wachilia mbali kufundishwa pia. Elimu hiyo wanayoitoa kwa watu sio sehemu ya mafundisho ya mitume, ya Yesu Kristo wala Biblia kwa makanisa halikadhalika Agano Jipya halijafundisha hiyo kwa makanisa pia. Hakuna sehemu yoyote ile ya Agano Jipya ambapo Yesu Kristo au hata mitume wanapojaribu kutia laana ya Agano la Kale lililofanywa kati ya Mungu na Waisraeli kuitii kwa wale walioingizwa katika ufalme wa Mungu kwa kupitia uzao mpya wanavyofanya nyakati hizi.

Haya, au pengine labda wakristo wa nyakati za Agano Jipya, wao walikuwa na “usafisho zaidi na kabisa” wakati wlipookoka kuliko wakristo wa nyakati hizi za leo, na kwa hiyo hao hawakuwa na matatizo na hawakuhitaji aina hii ya mafundisho? Lakini kwa hakika mawazo hayo sio ya kweli kulingana na Neno la Mungu linavyotuonyesha. Watu walipata kuokolewa au kupokea ujumbe wa Injili kama mtu binafsi au maelfu ya watu kwa wakati mmoja. Na yawezekana pia kuwa hali ya mioyo ya wengine wao haikuwa safi au walianza vema, lakini hawakuendelea kutembea katika utiifu wa Imani na Upendo. Kama ilivyokuwa nyakati hizo halikadhalika nyakati hizi. Kimsingi, watu ni wa aina ile ile katika kila kizazi na huyapokea mambo kwa njia ya tofauti katika wokovu ambao Mungu amewapa. Na kama vile ilivyo nyakati hizi za leo, kama tusomavyo katika Agano Jipya ndivyo ilivyo kuwa pia nyakati za Agano Jipya – yaani, watu makanisani walikuwa na aina zote za matatizo yanayotofautiana: dhambi, tabia za kimwili, matendo ya uongo, uchungu, mivutano n.k. Jaribu tu kujisomea mwenyewe Wakorintho au Wagalatia, kwa mfano – utagundua haya!

Haya, iwapo wokovu wa Mungu ni ule ule leo kama vile ulivyo kuwa nyakati hizo, na iwapo mwitikio wa watu na matatizo yao ni ule ule leo, kama vile ilivyo kuwa nyakati zile za Agano Jipya; basi sasa ni kwa nini! Oho, jamani! Ni kwa nini basi Yesu Kristo mwenyewe pamoja na mitume wake hawakuwafundisha watakatifu au hata makanisa juu ya mambo hayo (au hata wale wasioamini) kwamba laana zilizopita zinaweza kuwaathiri watu wa Mungu na kuwaweka katika vifungo au giza – kama tunavyoelezwa leo na hao walimu wa kisasa? Kwa nini hawakuweza kabisa kuonyesha kwamba matatizo yetu tunayoyapata sasa tukiwa kama ni watu wa Mungu, yanatokana na laana kutoka mambo yaliyopita? Jambo hili halipaswi liwe kama vile jambo la kudhanidhani au kubuni, au kama kazi ya ubunifu ya mwanadamu. Ni jambo la hatari sana katika utata wake, kwamba ni lazima tuwe makini sana hapo katika kuyagundua mafundisho kutoka katika Agano Jipya; kwa sababu humo katika Biblia mumejazwa taarifa zote zihusuzo ukombozi wetu na wokovu katika Kristo. Lakini hata hivyo hakuna popote pale ndani yake unapoweza kuyaona mafundisho yao hayo!

Kutokana na hilo, basi hii pekee ingetosha kabisa kutuonya sisi leo, kuwa kuna kitu ambacho si cha kweli ndani ya mafundisho yao hayo na kwamba hatupaswi kuyapokea ndani ya mioyo yetu. Hii ni nyongeza yao kwenye Injili. Hii ni sumu ndani ya mioyo yetu iliyokwisha kombolewa na Kristo. Hata kama itatokea baadhi ya watu kuamini kuwa wanaweza kuipata mistari katika Agano la Kale inayounga mkono mawazo yao, bado ni lazima tutambue kuwa, kitu chochote kile kinachotakiwa kwa ajili ya wokovu na ukombozi wetu na maisha ya Ki-Mungu, kimeunganishwa na kufunuliwa hivyo pia ndani ya Agano Jipya. Kazi ya Agano la Kale ni kuonya mbele juu ya wokovu na ukombozi kwa njia mbalimbali na hii inasaidia zaidi na kufafanua na kukielezea vizuri kile kinachofundishwa ndani ya Agano Jipya. Lakini kama tunafundisha kama kwa kulazimisha kwa wokovu wetu au ukombozi kama wakristo na tunajaribu tu kupata maelezo mengine kutoka Agano la Kale kwa ajili ya kukidhi dhamira yetu ya kutaka kuungwa mkono katika jambo hilo, pasipo hata kuliona kwanza jambo hilo likifundishwa pia au kutajwa ndani ya Agano Jipya; basi ikiwa ni hivyo, hapo mafundisho yetu yatakuwa yanapingana na ukweli wa Injili.

Na hiyo sio sawa hata kidogo: hiyo ni hila, nasi tutakuwa tukiwadanganya wengine katika kufundisha hilo. Elimu yao hiyo, inapinga kabisa mafundisho ya Yesu Kirsto na ya kwamba yeye Yesu ndiye aliyesulibiwa. Hiyo ni nyongeza ya kibinadamu katika waraka wa Wagalatia. Bila shaka hakuna kupishana kabisa kati ya Agano la Kale na Agano Jipya, lakini yapo maendeleo na mabadiliko ya kimsingi. Yamechukua sehemu yake kwa sababu ya yale yaliyofanywa pale Kalvari. Kama vile ilivyo kwa makosa mengine mengi, hasa yale ya nyakati hizi za leo; mafundisho hayo hayakutokana na Biblia, bali watu wameyaanzisha au kuyabuni kutokana na mawazo yao au mtindo wao wa kufikiri, kisha wakayafasiri maandiko kulingana na matakwa ya muundo wao. Na wanapindisha na kubadilisha maana halisi ya maandiko, wakayatumia mpaka yakubaliane na muundo wa mawazo yao. Hivyo ndivyo wanavyofanya katika wanachoweza kukitumia katika Agano Jipya ili kuunga mkono mafundisho (mapokeo) yao.
Lakini hebu tutazame jinsi ambavyo watu hao wangejaribu kutafsiri baadhi ya maandiko kutoka katika Agano Jipya, ambayo ndiyo mistari wanayoitumia kunukuu. Yak.3: 7-10 na Ufu. 22:3. Hayo ni baadhi ya maandiko yanayotumiwa kunukuliwa ili kuonyesha watu kuwa laana na kulaaniwa ni vitu vinavyoendelea kuwepo leo. Kwa kadri ilivyo siyo mbaya, lakini pia wao wanaendelea kusema kuwa, kwa sababu laana inaendelea kuwepo, kwa hiyo wakristo wenyewe wanahitajika kutambua kuwa inewezekana kabisa wameshawishiwa na kuzuiwa katika maisha yao kwa laana. Lakini maandiko haya “rukii” kwenye ufahamu wa hatua hiyo wanayodai wao. Kwa kweli maandiko hayo mawili hapo juu wala hayafundishi hivyo; badala yake ingalipo inaendelea siku za leo, na watu wanafanya mambo ambayo hawapaswi kuyafanya, kwa mfano, kuwalaani wengine, na kwamba katika mbingu mpya na nchi mpya hakutakuwepo tena na laana, au tungeweza kusema kuwa, hakutakuwepo tena na hukumu – kwa ajili ya dhambi na uasi. Hata hivyo mistari hiyo hapo juu haileti uhusiano wowote kati ya matatizo ya maisha ya wakristo na laana ambayo ingeweza kuwekwa kwao au kwa mababu zao, kana kwamba hayo ndiyo iwe ni sababu ya mataizo katika maisha yao! Hakuna mahali popote pale katika nyaraka zote za Agano Jipya, ambapo hata kwa umbali tu inahesabiwa au hata kutajwa tu kwamba ndiyo sababu inayosababisha matatizo au mateso katika maisha ya wakristo, (au katika maisha ya mji au taifa). Yakobo hasemi hapo kuwa, “Tazameni, watu wanalaani, kwa hiyo mnajua laana bado inaendelea kuwepo, na kwa hiyo maisha yenu yatazuiwa kwa laana. Na kama mnalo tatizo linaloendelea katika maisha yenu, basi hilo linaweza kuwa limesababishwa na laana zilizopita. Kwa hiyo mnapaswa kuchunguza miienendo ya mababu zenu kwa makini sana ili kugundua kuwa uwezekano wa mizizi ya aina hii ya laana katika maisha yenu, na hivyo kuomba ukombozi kutokana na hilo.” Huu ni upumbavu mkubwa sana kutafsiri maandiko hayo ya Yakobo kwa jinsi hiyo. Anachokifanya Yakobo hapo katika mistari hiyo, ni kutufundisha tu kwa uwazi kwamba maneno yetu tunaposema yasiwe matamu na machungu, uchafu na usafi, baraka na laana. Jambo hilo liko wazi tu hapo, hayo ni mafundisho yenye afya nzuri tu hapo; ni mausia na kukemea kuhusiana na kuokolewa kwetu! Lakini kama nilivyotaja hapo juu, waalimu hao wanajaribu kutumia sura yoyote ile ya maandiko wanayoweza kuitumia, kisha kuipindisha na kuibadilisha, kisha kupanua maana yake halisi.

Yawezakana pia mahala pengine baadhi ya waandishi hawa wanaweza kumnukuu hata Yesu, pale anaposema, “…Wabarikini wale wanaowalaani ninyi” (Luka 6:28). Lakini katika mambo ambayo nimepata kusoma, sijaigundua hata sehemu moja ambapo waandishi hawa wanapelekea kutaja mistari hiyo pale wanapojaribu kuunga mkono mawazo yao kuhusiana na laana. Na yawezekana kuona kuwa ndiyo maana haishangazi, mafundisho hayo ya Yesu “hayapindi” kwa urahisi ili yafananishwe na mtindo wa mawazo yao. Yakobo anatueleza kuwa, anaona watu wanaendelea kulaani, wakati hawapaswi kufanya hivyo. Mafundisho hayo mapya yanasema kuwa eti ikiwa mtu bado anaendelea kulaani, kama vile Yakobo alivyosema, basi maisha ya wakristo yatadhurika kwa laana hiyo ya watu wengine. Lakini Yesu mwenyewe hasemi kuwa kama mtu atakulaani, basi “uwe mwangalifu sana, yawezekana laana hiyo ikakupata. Unauhakika kuwa hujafanya dhambi? Maana unaweza ukawa tayari uko chini ya nguvu za laana katika maisha yako, na lazima uhakikishe kwamba unataka kutoka katika laana hiyo.” Hapana. Haiwi hivyo hata kidogo; kwa sababu hata kabla ya pale Kalvari, Yesu Kristo aliwaambia watu maana halisi ya kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu na tabia yake. Yesu alisema, Ikiwa yeyote yule atawalaani, ninyi mbarikini! – Amen! Kwisha! Hakuna zaidi ya hapo. Uwabariki tu! Hayo ndiyo mafundisho yake Yesu Kristo.

Yesu hawezi kutujaza akili zetu na mawazo ya kiushirikina na udanganyifu kuhusu mambo ya uovu yanayoweza kutujia ikiwa watu watatulaani. Hakuna lolote linaloweza kutudhuru iwapo tunafuata yaliyo mema (1 Petro 3:13). Hayo ni marejeo yaliyo adimu kuhusu laana katika Agano Jipya ambamo Yesu Kristo mwenyewe aliyatoa. Kwa hakika Biblia inacho kitu cha tofauti na cha muhimu inachoweza kutufundisha. Ni kumbukumbu za pekee ndani ya Agano Jipya ambazo hutuelekeza cha kufanya na kuelezea pia kwamba tabia zetu zinapaswa kuwaje pale mtu atakapotulaani! Sasa kwa nini basi walimu hawa wanayapinga na kuyakataa yale ambayo Yesu mwenyewe anayasema kuhusu njia ya kuifuata pale mtu atakapolaaniwa? Kwa nini basi wao hawayafundishi yale ambayo Yesu Kristo anayafundisha?

Hivyo ndivyo ilivyo katika Yakobo 3:7–10, na Ufunuo 22:3. Huo ndio “Ushuhuda” wao wanaoutumia kutoka katika Agano Jipya ili kuonyesha kwamba wakristo leo wanaweza kuwa na wamo katika vifungo, giza au magonjwa – eti hiyo yote ni kwa sababu ya laana zilizopita! Na jinsi gani tunapaswa kufuatilia au kugundua laana hizo zilizopita, ambapo inaweza kwa kufanya hivyo kutupeleka nyuma zaidi ya miaka mia moja iliyopita?
Mpendwa msomaji, unafikiriaje? Je, na wewe unaamini kuwa mistari hii inatufundisha mambo hayo wayasemayo? Je, hayo ndiyo mafundisho ya Yesu au Mitume? Je, unaweza kuyapata mafundisho hayo mahala popote pale katika Agano Jipya? Ni jambo la kufurahisha kuona kuwa, bila shaka kitabu maarufu sana na chenye kuvutia na kinavyoshabikia kasoro hizi hapa ulimwenguni pote, hakijaribu hata kidogo kutoa ushahidi wowote ule katika Agano Jipya ili kuunga mkono mafundisho hayo.

TAARIFA YA UBADILISHAJI WA JINA LA BLOGU HII,KUTOKA MWAKASEGE INJILI NAKUWA HUDUMA YA UKOMBOZI GOSPLE NA ANUANI YAKE KUTOKA www.mwakasegeinjili.blogspot.com na kuwa www.ukombozig.blogspot.com

Mkurugenzi wa kampuni ya HAKI LEO ambayo ndiyo inamiliki blogu hii Oscar Samba anayo furaha kuwatangazia kwamaba siku chache zijaro jina na anuani ya blogu hii vitabadilika kama ilivyo ainishwa hapo juu.

Sababu kuu ya mabadiliko hayo  inatokana na uanzishwaji wa huduma mpya itakayokuwa chini yake naitaitwa UKOMBOZI GOSPLE.

Maono yake na malengo yake yatakuwa hatharani rasimi baada ya uzinduzi wa huduma hiyo utakao fanyika siku hiyo ya ubadilishaji wa jina hili.

Pia anaomba radhi kwa usumbufu utakao jitokeza,na tafadhali upatapo tangazo hili mtaarifu na mwenzako.

Jumatatu, 12 Mei 2014

ISRAEL HOUGHTON KUIMBA NCHINI UGANDA MWEZI UJAO, HAKUNA KIINGILIO


Watoto Children Choir namba 66 wakiimba kanisani kwao kabla ya kuelekea nchini Australia kwa ziara wiki mbili zilizopita.
Nyota wa muziki wa injili duniani Israel Houghton kutoka nchini Marekani anatarajiwa kuwa mwimbaji mwalikwa katika sherehe za kutimiza miaka 30 ya huduma ya kanisa la Watoto Uganda pamoja na miaka 20 ya huduma ya wanawake na watoto kupitia Watoto child care ministries zote zikiwa chini ya kanisa la Watoto ambalo umaarufu wake umetokana na kwaya ya Watoto children chini ya waanzilishi wa huduma hiyo Gary na Marilyn Skinner zitakazofanyika mwezi wa sita nchini

humo.

Israel na kundi lake la New breed wanatarajiwa kuimba siku ya alhamis tarehe 5 katika kanisa la Watoto west tukio ambalo halitakuwa na kiingilio lililopewa jina la 'Watoto Big Party'. Hii itakuwa si mara ya kwanza kwa mwimbaji huyo kuimba jukwaa moja na Watoto children choir ambao amekuwa akikutana nao sehemu mbalimbali. Mwimbaji huyo atakuwa nchini Uganda wiki moja baada ya kumaliza tamasha lake kubwa la uimbaji litakalofanyika jijini London nchini Uingereza tarehe 27 mwezi wa tano akiwa na kundi lake kamili.

Haya kwa wale wapenzi wa mwanamuziki huyo, ni kujipanga nauli ya kwenda na kurudi na sehemu ya kufikia bila kusahau chakula, onyesho halitakuwa na kiingilio.

Jumamosi, 10 Mei 2014

KANISA LA KILUTHERI MWANZA LATOA TAMKO JUU YA BOMU KANISANI KWAO


Kanisa la Kilutheri jijini Mwanza.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria (DMZV), limeitaka Serikali kuhakikisha inawatafuta watu waliohusika na tukio la bomu lililolipuka kanisani hapo juzi.Pia, limewataka Wakristo kuwa watulivu, wasiogope wala wasitishwe na mashambulizi hayo na kwamba wasilipize kisasi.

Akizungumza kwenye Kanisa la Imani Makongoro Misheni jana, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria, Andrew Gulle alisema wanaamini shambulio hilo ni la kigaidi na kwamba, Serikali inapaswa kuchukua hatua ya kuwasaka wanaohusika “Kanisa tunaamini tukio hili linahusiana na ugaidi, umefika wakati Serikali ikachukua hatua za kuwasaka waliohusika ili sheria ifuate mkondo wake,” alisema Gulle.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya dini wanasema huenda tukio hilo linatokana na migogoro inayoendelea kanisani hapo kwa sababu tayari kuna baadhi ya waumini wamejitenga kwa kuanzisha kanisa lingine “Wasikwepe matatizo yao ya ndani, kuna askofu aliuawa kwa kupigwa tofali kutokana na migogoro, hivyo hata hili (tukio) litakuwa ni migogoro inayoendelea,” alisema mmoja wa waumini ambaye hakutaka kutajwa jina lake.
Askofu Gulle alikanusha kuwapo kwa migogoro kanisani hapo na kwamba, tukio hilo halihusiani na mgogoro wowote ndani ya Kanisa bali ni ugaidi.

Majeruhi aendelea vizuri

Hali ya majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea kanisani hapo, Benadeta Alfred, imeelezwa kuendelea vizuri katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando alikolazwa. “Hali ya mgonjwa ni nzuri ukilinganisha na tulivyompokea kwani hata kuongea alikuwa hawezi, lakini hivi sasa anaweza kuongea japo kwa shida,” alisema Lema.

Jumatano, 30 Aprili 2014

HABARI PICHA KUTOKA MBEYA: MAZISHI YA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA WANAWAKE WA INJILI EAGT


Picha ya marehemu Mama Benja (Junitha B. Mwamnyila)

Shujaa umekwenda, Kazi umemaliza mama kapumzike, ni baadhi ya maneno yaliyosikika na GK kwa waombolezaji waliojitokeza katika viwanja vya kanisa la EAGT Gilgal Mwanjelwa kuuaga mwili wa Mwinjilisti na Mkurugenzi wa WWI Taifa Mama Benja na kisha kwenda kuulaza kwenye nyumba ya milele maeneo ya Sabasaba.


Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio yaliyojiri kama ambavyo GK iliahidi kukuletea baada ya kupiga kambi msibani hapo, ambapo awali ilikupa picha za awali.

VIONGOZI WAKUU WA EAGT TAIFA NA WACHUNGAJI



















Mchungaji Daniel Kulola



MKE WA MAREHEMU MOSES KULOLA NAE ALIKUWEPO







WATOTO NA NDUGU WA MAREHEMU MAMA BENJA













MARAFIKI WALIKUWEPO KUFARIJI







WATU MBALIMBALI WALIJITOKEZA KUAGA
















WENGINE WALISHINDWA KUJIZUIA




















MWILI ULISHUSHWA KABURINI












MAVUMBINI TUTARUDI






Marehemu ameacha watoto wanne, ambapo uzao wake wote umekuwa watoto mapacha, mara ya kwanza akijifungua mapacha wa kike, na kisha uzao wake wa pili ukiwa mapacha tena, wa kike na wa kiume. Na katika maisha yake, Mama Benja (Benjamin likiwa jina la marehemu mume wake aliyekwisha fariki miaka mingi iliyopita) amekuwa mwinjilisti hodari na kushika nyadhifa mbalimbali kwenye kanisa la Evangelistic Assemblies of God.


Kama hukupata fursa ya kusikia maneno yake ya mwisho, basi bofya hapa, usikie alichosema marehemu ambaye alizaliwa tarehe 2 Oktoba 1951, na kufariki dunia tarehe 24 Aprili 2014. Kwa watumiaji wa simu bofya hapa kuipakua. Gospel Kitaa inawaombea wafiwa wote wapate nguvu katika kipindi hiki kigumu. BWANA ametoa, na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.