Jumanne, 7 Oktoba 2014

USUHUDIAJI WA MTU KWA MTU KANISA LA TAG VCC ARUSHA

NA mama Mcungaji CATHERINE MBUGHI
Kushoto ndie mama Mchungaji Catherini Mbughi akisisistiza jambo la MUNGU katika jukwaa la Injili na kulia ndie Baba Mchungaji Aloice Mbughi.Picha na Makitaba.

Ninayo furaha ya hali ya juu kukukaribisha ewe msomaji wa blogu hii ya www.mwakasegeinjili.blogspot.com katika ujumbe huu wa leo kama ulivyotolewa kwenye kanisa la VCC na huyo mtumishi wa MUNGU kwenye mafundisho ya asubuhi ya wanafunzi na maandiko.

Ninae kuandikia ujumbe huu na kukuletea ni mimi OSCAR SAMBA na moja kwa moja tuzame kwenye somo letu la leo ambalo linalenga kukutia moyo wewe uliye okoka kuhusu kuwashuhudia wengine.

Luk 10:23-26
10.23 Akawageukia wanafunzi wake, akasema nao kwa faragha, Heri macho yaonayo mnayoyaona ninyi.
10.24 Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona
ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.
10.25 Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi
uzima wa milele?
10.26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?

Mpendwa kumbuka kuwa Inatupasa kuwashuhudia watu wote, Yohana 3:16, 3.16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu
amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.                    

,Unapo mshuhudia mtu msome NENO la Mungu kwani ndio silaa yetu na haikupasi kwenda vitani bila silaa.
Yohana 14.15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.Mpendwa andiko hili yatupasa kuhakikisha ya kwamba tunalishi hili kama kweli tunalipendana, kwa kuanza kushuhudia, na hii sio amri tuu bali pia ni agizo kuu.

Waambie ya kwamba mshahara wa dhambi ni mauti wala usiwafiche waeleze kuhusu jehanamu na pia wakumbushe uzuri wa mbinguni na waambie mbingu ipo kwa ajili yao tuu kama wakiamini.

Ukisha maliza muulize je, upo tayari kumapa YESU maisha yako akisema ndio muongoze sala  ya toba na akisema laa mulize na sema nae kuhusu hatima ya maisha yake nakumuliza je, anafahamu nini kuhusu hatima ya maisha yake baada ya kufa,mkumbushe kwa herufi KUBWA na msisitizo kinywani kuwa ni hukumu na hukumu yake MUNGU ni ya HAKI.

Mpe mfano wa tajiri na Lazaro kwani mara baada ya kifo kila mmoja alivuna alichopanda, Lazaro mbinguni tena kifuani mwa Ibrahimu na Tajiri motoni.

Hakika kupitia NENO la Mungu inawezekana kuwafanya watu kuingia mbinguni.Maandiko tuliyoyasoma hapo juu yanatutaka tuwapende jirani zetu kama Nafsi zetu pia “1 YOHANA 4-20-21   4.20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana
asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
4.21 Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.
Kwa hiyo yatupasa kutimiza andiko hili kwa Moyo wote kwani upendo wa kweli kwa Mungu wetu huanza kwa kumpenda jirani yako na upendo wa kweli kwa jirani yako uliyo na matendo ni kumwambia habari za YESU.

Weka mpango na mikakati yakuhakikisha yakwamba ndugu zako na rafiki zako wanaokoka,usikubali waende huko kwani kunatisha mnoo.
Mliliye YESU nasema nae kuhusu ndugu na jamaa zako lakini pia toka ka’a waambie hao watu ya kwamba YESU anaokoa.

MAMBO MUHIMU
1.Uwe na huruma ya KIMUNGU ndani yako,hakikisha unaguswa na tabu zao na mateso yao
2.Uwe na upendo wa MUNGU ndani yako YOHANA 3:16
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu
amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Usikubali juma hili lipite bila kuwaambia habari za YESU,ukikutana nae njiani ama popote pale mwambie YESU anampenda.Hata kama hataokoka leo lakini hakikisha unampandia NENO.
Upendo unagarimu,upendo unahitaji kujitoa kwa hiyo hakikisha unaingi gharama kwa kusugua goti ili watu waende mbinguni.Litumie NENO kwani hili NENO linauwezo wa kumuokoa na kumbadilisha kumbuka IMANI huja kwa kusikia kwa mantiki hiyo hilo NENO huweza kufanyika uponyaji kwake.
Kuna vilio vya aina mbili cha kwanza—ni cha mtu aliyeomba maji akiwa Jehanamu na B yake ni cha mtu aliyeomba ndugu zake wasiende jehanamu.
Luka 16:19-31
“16.19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula
sikuzote kwa anasa.
16.20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
16.21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata
mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
16.22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye
akafa, akazikwa.
16.23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali,
na Lazaro kifuani mwake.
16.24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake
majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
16.25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika
maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
16.26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku
kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
16.27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
16.28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
16.29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
16.30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
16.31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.”

Embu jiulize angalikuwa ni ndugu yako yuko huko jehanamu ungali jisikiaje ?
Na kilio chapi ni cha mtu uliyemshuhudia na kukataa kuokoka..
Zingatio kuu la somo la leo : TUKIKOSA HURUMA HATUTA VUNA
Naam hadi kufikia hapo ndio mwisho wa ujumbe huu tafadhali endelea kutembelea blogu hii ya www.mwakasegeinjili.blogspot.com kwa makala na habari zaidi.Pia kumbuka siku chache zijazo blogu hii itakuwa na na jina jingine ambalo ni www.ukombozig.blogspot.com na kwa sababu zaidi soma habari iliyopita.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni