Wapili kutoka kushoto ndie Mtumishi Jeremiah Mlawa akiwa na watumishi wenzake katika maeneo ya Ibada, (Picha na Makitaba) |
Na Mtumishi
Jeremiah Mlawa
1.Uwe na Imani,Hakikisha ndani ya uokovu wako
uwe ni mtu wa imani,jiamini na pia amini
sehemu unayoabudu.
2.Uwe Mkweli,Epuka kuwa muongo na penda kuwa
mkweli kwa kushuhudia kweli ya MUNGU,pia usiwe mzungumzaji kwa mtu ambaye
unajua atahadhiri uokovu wako.Unapo mshuhudia mtu kuhusu uokovu hakikisha wewe
mwenye ni msafi ndani ya moyo wako na ukifanya hivyo jina la MUNGU halitatukanwa
na ushuhuda wako utakuwa barua.
3.Uwe Mtii,Hakikisha kwenye eneo unalolelewa
unatii unaloambiwa,usiwe mwepesi wa kuitikia na kutokutii.Unapo weka ahadi kwa
mtumishi ama mpendwa hakikisha unatii.Penda kutii muda wako katika maswala yako
yakimaisha kama ibada inaanza saa 2 kamili hakikisha unatekeleza ama kutimiza hilo,Baraka
za MUNGU huenda na wampendao.
4.Uwe ni Mtu
wa Haki.Hakikisha kwenye maisha yako
unaishi kwa haki na watu wote,na mwenendo wako uwe wa haki,tafuta amani na watu
wote.Usijiesabie haki kwa kumuona mtu Fulani ambae ni mwenye dhambi anahatia na
wewe ni bora kuliko yeye,Mungu wetu ni Mungu wa wote wenye mwili.Kama unawaona
wako kinyume wewe waombe.
Ukiyazingatia
haya hakika hali yako ya kiroho itakuwa ya utofauti kwa viwango vikubwa mno.MUNGU
wetu wa mbinguni na BWANA YESU akuwezeshe kutii hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni