Ijumaa, 13 Desemba 2013

AMBWENE MWASONGWE AACHIA VIDEO YA MISULI YA IMANI


Hatimaye baada ya kusubiri kwa muda mrefu video ya Ambwene Mwasongwe imeanza kupatikana jana baada ya kukamilika kwake. Video hiyo iliyobeba jina la "Misuli ya Imani" audio yake imetokea kupendwa na kuwavutia wengi hasa jumbe zilizomo katika nyimbo hizo ambazo zimejaa matukio ya kweli yanayowatokea watu.


Ambwene Mwasongwe Mwasongwe
10 hours ago via mobile
Video ya misuli ya Imani tuliyoingoja muda mrefu sasa iko madukani kuanzia Leo! Napenda kukushukuru kwa maombi yako na naamini ile nguvu ya Mungu iliyokuwa katika nyimbo hizo itakugusa na kukuhudumia! Karibu tubarikiwe site.Ambwene ambaye alitoa video ya kwanza ya Majaribu ni mtaji, alikuwa kwenye mpango wa kutoa album mbili za video kwa pamoja ikiwa ni toleo lake la pili na la tatu ambapo ameamua kuachia kwanza toleo la tatu ambalo lilikuwa likiuliziwa na watu wengi hasa kukiwa na nyimbo kama Upendo wa kweli, Misuli ya imani, Natamani na nyingine nyingi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni