Alhamisi, 5 Desemba 2013

JE UNALO JAMBO LA IMANI LITAKALO MGUSA MUNGU,WAKATI WA KUFA KWAKO ? * sehemu ya mwisho*


Mtumishi Gasper Madumla.


Nakusalimu mpendwa katika Jina la Bwana;
Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya...

Ni matumaini yangu U mzima wa afya siku ya leo,Nami ninakukaribisha tushiriki pamoja kujifunza mambo ya msingi kwa habari ya maisha yetu ya kila siku.

Mkristo yakupasa uwe na mambo ya IMANI utakayoyaacha kama ALAMA katika kipindi ambacho hautakuwepo hapa chini ya jua,
Au katika kipindi cha hatari ya kufa kwako,ambapo ALAMA hiyo itakusaidia kwa kukuongezea muda wa kuishi.

Leo ngoja nianze tena,kwa hivi;

Haitupasi tufe tukiwa na mambo mengi tuliyoyashikilia katika vichwa vyetu,

mfano;
Tufe tukiwa na mipango mingi ambayo hatukuweza hata kuwashirikisha wengine,
Au
Tufe tukiwa hatukuifanya kazi ya BWANA kiukamilifu.

*Muda tulionao wa kuyafanya mapenzi ya BWANA ndio sasa.

Yatupasa tufe tukiwa watupu/EMPTY yaani zile karama ambazo Bwana ameweka ndani yetu,tuhakikishe tunazitumia ipasavyo,na wala tusife nazo pasipo kuzitumia.

Mungu atusaidie tufe katika hali ya Neema na toba,tukiwa hatuna vitu tulivyovishilikilia.
Kwamba tufe tukiwa tumeifanya kazi ya BWANA kiukamilifu.

Kufa ukiwa umeifanya kazi ya Bwana kiukamilifu,pamoja na kuyaachilia mambo ya kiimani/Alama ya kiimani,ndiko kufa ukiwa EMPTY.

Najua kwa habari hii,yawezekana ikawa ni jambo gumu kwako lakini yote yanawezekana tukiwa ndani ya Kristo.

Haleluya...

Kufa,kupo mpendwa,
Yeye aliyekufa amekufa tu.
Biblia ina
dhibitisha jambo hili;
" Na kama vile watu wanavyowekewa kufa Mara moja,na baada ya kufa hukumu." Waebrania 9 : 27.

Hivyo ikiwa kufa kupo,
basi hatuna budi tuwe na mambo,vitu vya kiimani vya kuviacha hapa duniani,ambavyo kwa hivyo vitamkumbusha BWANA MUNGU hata kughahili kifo chako ukiwa katika hatari ya kufa kwa kukuongezea tena miaka mingine ya kuishi kama kwa habari ya Hezekia.

Haleluya...

Kumbuka,
Tunalojifunza hapa ni juu ya jambo,au kitu unachotakiwa kufanya sasa ukiwa ndani ya Kristo Yesu,ambapo kupitia jambo hilo la IMANI litaweza kumkumbusha BWANA Mungu akutoe na kukuponya kutoka katika mauti.

Tuliangalia mfano wa mtu mmoja,Hezekia, aliyekuwa katika hatari ya kufa na ilimbidi amkumbushe BWANA MUNGU kwa mambo yote aliyoyafanya.
Na tazama BWANA Mungu akamuongezea Hezekia muda wa miaka mingine wa kuishi.

Sasa sikia;

Muda wa miaka kumi na mitano aliyoongezewa Hezekia (2 Wafalme 20:6)
Ni muda usiohesabika kwa akili za mwanadamu,
maana miaka 15 ya Mungu sio miaka 15 ya mwanadamu.

Uponyaji wa Hezekia,ulitegemea kumkumbusha Bwana Mungu kwa yote aliyoyafanya mbele zake BWANA MUNGU.

Laiti kama Hezekia asing'emkumbusha Bwana yale mema,basi yamkini ang'elikufa.

Tunasoma,;

"Nakusihi,BWANA,ukumbuke sasa ,jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu,na KUTENDA YALIYO MEMA MACHONI PAKO.Hezekia akalia sana sana."2 Wafalme 20:3

Bwana Mungu aliweza kuchungulia ndani ya ile kweli aliyotenda Hezekia,na alipoiona ya kwamba ni kweli anayoyaomba yanafanana na matendo yake mbele za Bwana.

Hezekia ;anatufundisha jambo moja kubwa siku ya leo,kwamba
Lazima tuwe na jambo la kumkumbusha Bwana nyakati zetu za hatari ya kufa.

* Hatuwezi kumkumbusha Mungu juu ya jambo ambalo halipo kiuhalisia tukategemea majibu kama ya Hezekia.

Mfano;
Mmoja akiwa katika hatari ya kufa,kisha aanze kuomba hivi;
" Baba wa Mbinguni,tazama nilivyokwenda mbele yako kwa ukamilifu,nikikutumikia kwa moyo mkunjufu..."

Lah! kumbe ni muongo tu!
Kwamba anachokiomba hakifanani na maisha yako halisi.
Ni sawa na kusema unampenda Yesu lakini haufanyi mapenzi yake.

Nasema mtu wa namna hiyo hakika hatajibiwa maombi yake,na kama kufa atakufa katika uovu wake,kwa sababu kile alichokiomba mbele za Bwana hakifanani na maisha yake.

* Jambo au tendo la kiimani lenye nguvu mbele za Bwana,
Ndilo Bwana huguswa nalo,pindi akikumbushwa.

Ooh!
Kumbe,

Kuna wakati ambao BWANA anahitaji kukumbushwa juu ya jambo jema.
Si kana kwamba Yeye Mungu hakumbuki,hapana, Yeye Mungu hukumbuka vyote.
Bali anachohitaji kwako ,ni kukuona wewe unanyenyekea mbele zake.

Hezekia alikuwa mtu mwenye moyo wa ukamilifu,tena alikuwa ni mfalme mwenye kumtegemea BWANA MUNGU kwa kila kitu.

Tunasoma;
"Alimtumaini BWANA,Mungu wa Israeli;hata baada yake hapakuwa na mfano wake katika wafalme wote wa Yuda,wala katika hao waliomtangulia."2 Wafalme 18:5

Mungu hupendezwa na watu wake.
Mungu hawezi kuongwa,Bali huvutwa na mtu mmoja anayeishi kwa kuyafanya mapenzi yake,kwa maana mtu huyo atakumbukwa.

Tuangalie mfano mwingine wa mtu aliyekufa,akafufuliwa kwa sababu ya mema aliyokuwa nayo,
Naye si mwingine Bali ni Lazalo.

Lazalo alikuwa ni rafiki yake Bwana Yesu
Na ndio maana hata Yesu alipopata habari ya kifo chake Lazaro,
hakusita kumuendea,naye akamfufua.

Kilichomfanya Lazaro afufuliwe ni ule ushirika aliokuwa nao yeye na Bwana Yesu (Yoh.11:35 )
Soma pia Yoh.11:1-44

Hivyo tumuombe sana BWANA MUNGU atusaidie tuweze kuishi kwa mapenzi yake,ili tuwe na jambo la imani litakalo tusaidia tukiwa katika hatari ya kufa kwetu.

Kwa maombezi;
* 0655 111149.

MWISHO.

UBARIKIWE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni