Alhamisi, 19 Desemba 2013

MOTO WA INJILI UNAWAKA MAJUMBASITA, WANAFUNZI WASHUHUDIA

NA GOSPLE KITAA

Mchungaji Moses Maghembe.
Mungu azidi kujidhihirisha katika mkutano wa injili Afrika kumepambazuka ulioandaliwa na kanisa la T.A.G Majumbasita chini ya mchungaji Moses Maghembe. Mkutano huo ulioanza tarehe 8 mwezi huu unatarajiwa kumalizika tarehe 29 ukiongozwa na kichwa kisemacho "Yesu ni yeye yule jana leo na hata milele". Wahubiri katika mkutano huo uliofunguliwa na mchungaji Abdiel Mshashi kutoka mkoani Kilimanjaro na kupokewa na mwenyeji mchungaji Moses Maghembe ambaye atampisha askofu Elia Lugwami kumalizia ngwe.
Ambapo kati ya shuhuda zilizosisimua mpaka sasa ni pamoja na shuhuda za watoto mmoja aliyeeleza jinsi alivyokuwa akitumika kwa njia za kishirikina, mwingine pia kueleza jinsi walivyokuwa wakitumiwa na mapepo hali iliyosababishwa kuitwa kwa waganga wa kienyeji na wachungaji ili washindane namna ya kuyatoa. Lakini kubwa zaidi iliyowaacha watu na mshangao ni pale mtoto mwenye miaka 12 kueleza alivyoshikwa na pepo la ulevi kupindukia ingawa hata kwao walikuwa hawajui ambapo watoto wote walipata uponyaji katika mkutano huo ambao bado unaendelea mpaka tarehe 29 mwezi huu.












Picha mbalimbali kutoka katika mkutano huo. ©Filemon Rupia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni