Jumamosi, 7 Desemba 2013
JOYOUS YAMUOMBA DRUMMER WAO WA ZAMANI AREJEE KUNDINI KUOKOA JAHAZI
Siyabulela Sabu Satsha.©Sabu Facebook page.
Kundi la Joyous Celebration limeamua kumuomba mpiga ngoma(drum) wake wa zamani Siyabulela Satsha kurejea kundini, ili kuwasaidia kuwapigia ngoma katika rekodi yao ya DVD ya 18 inayotarajiwa kufanyika tarehe 20 na 21 mwezi huu katika kanisa la City Hill lililopo Durban Afrika ya kusini.
Katika ujumbe aliowahi kuweka katika ukurasa wake wa Facebook Sabu ambaye aliachana na Joyous mwishoni mwa mwaka jana baada ya kurekodi DVD ya 17, aliwaambia mashabiki na marafiki zake kwamba atakuwepo siku ya jumapili yaani kesho kuwapigia drum Joyous katika onyesho ambalo kundi hilo litashirikiana na mwanamuziki nyota Kirk Franklin wa Marekani na kumalizia kwamba "I'm back" maana yake nimerejea. Baada ya ujumbe huo mashabiki wameonekana kufurahishwa na uamuzi wa Joyous wakumrudisha mpigaji huyo.
Pamoja na hilo mpigaji huyo anayemiliki fimbo maalumu za kupigia drum zinazouzwa nchini humo, amekuwa na kazi ya ziada kuwaelewesha mashabiki na marafiki zake ambao wengi walitaka kujua ni kwanini sasa Joyous iliwapa ajira wapigaji wengine wawili wakiongozwa na Irebolaji Arowolo lakini hawamtumii katika rekodi hiyo, hali iliyomfanya mpigaji huyo kufunguka zaidi na kuwaambia ameitwa maalumu kurekodi tu na sio kwamba amerejea kimoja, maana wapigaji bado wapo na Joyous lakini ni uamuzi wa kundi lenyewe ambao wameamua kumuita ili awapigie nyimbo zote katika rekodi hiyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni