Ijumaa, 27 Desemba 2013

KRISMASI YA KILIO MOMBASA KENYA KANISA LALIPULIWA KWA MABOMU


Picha ya kanisa lililochomwa moto mwezi Octoba mwaka huu mjini Mombasa.©jihadwatch

Taarifa kutoka Mombasa nchini Kenya zinasema vijana wanaosadikiwa kuwa kati ya waumini wa dini ya kiislamu ama wanaounga mkono chama cha Mombasa republican council(MRC) kinachodai uhuru wa mji wa mombasa ambao wakazi wake wengi ni waislamu kujitenga na Kenya, wamechoma moto makanisa mawili mjini humo siku ya sikukuu ya krismasi kwa mabomu ya petroli.

Taarifa za jeshi la polisi zinasema bado hawana uhakika kamili na watu wanaosaidikiwa kutenda jambo hilo ambalo limeshuhudia kanisa la Christ Outreach ambalo likiwa limeharibiwa vibaya bali wanahisi vijana hao watakuwa wametokea kati ya makundi mawili ya dini ama chama kinachoendesha kampeni zakutaka pwani ya Mombasa kujitenga kutoka Kenya.

Kwa mujibu wa afisa wa polisi wa Likoni Mombasa Robert Mureithi amesema kwamba siku ya krismasi waumini walipewa tishio mapema na kundi la vijana wa mji huo waliowataka kufunga makanisa yao. Ambapo tayari wameanza kufanyia uchunguzi tukio hilo.

Aidha kwa mujibu wa mshauri mkuu wa baraza la kiislamu nchini Kenya shehe Juma Ngao amekaririwa na Reuters akisema kwamba"wanataka kuona wakristo wanapigana na waislamu ili Al Shabaab wafanikiwe mpango wao nchini Kenya kirahisi, lakini wakristo wanahekima" amekaririwa shehe Ngao.

Naye mmoja wa waumini wa kanisa la Christ Outreach lililoharibiwa vibaya kwa tukio hilo bwana Moses Andayi ameiambia Reuters kwamba walikuta ujumbe getini mwa kanisa hilo ukisema "Pwani si Kenya" yaani Mombasa sio upande wa Kenya, ujumbe ambao hutumika na chama cha MRC ambacho kinaendesha mambo yake kimagendo kutokana na kutosajiliwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni