Jumamosi, 21 Desemba 2013

MKRISTO KAMA SIMBA.*sehemu ya kwanza*


Mtumishi Gasper Madumla. NA GK

Bwana Yesu asifiwe...

Nasema;

Haleluya…

Karibu katika fundisho hili ambalo limekujia katika muda na wakati sahihi kabisa.

Leo nimemfananisha mkristo kama Simba,nami ninakuita wewe uliye mkristo ni Simba.

Wakristo wengi hivi leo wameshindwa kujitambua nafasi zao katika maisha yao dhidi ya kushindana katika roho.

Na ndio maana utakuta mkristo anamkimbia mganga wa kawaida kabisa. Wakati mganga yeye hana nguvu kama alizonazo mkristo,na yeye mganga ndie anayepaswa kukimbia.
Sasa hii yote ni kushindwa kujitambua.

Wakristo wengine huwakimbia mapepo,au huama hata nyumba walizopanga au mtaa pale wanaposikia habari mbaya za kulogwa.Huku nako ni kushindwa kujitambua. Lakini kupitia fundisho hili,najua wengi watajitambua ya kwamba mkristo ni kama SIMBA.

Ngoja nikupe mfano kidogo, labda utaanza kunielewa;

*Mtu mmoja alikuwa akiishi maeneo ya kijijini,alijaribu kutafuta kitoto cha simba akakafuga. Kisha kale katoto cha simba akakichanganya na kondoo aliokuwa anawafuga,

Siku moja sasa wakati hawa kondoo walipokuwa malishoni pamoja na kale katoto cha simba,gafla Simba wakubwa wakatokea na kunguruma .."griiiih!" walinguruma.

Wale kondoo na kale katoto cha simba,wote wakakimbia kwa sababu ya ule mlio mkali sana.

Ikawa kila waendapo malisho wanakutana na Simba angurumaye,nao hukimbia mbele yake, Lakini cha ajabu wale simba wangurumaye hawakuwadhuru kabisa.

Sasa siku moja walipokuwa majini katika malisho yao,gafla simba wakaanza kunguruma huku wakiwafuata,basi wale kondoo wote wakaanza mbio..

Lakini kale kasimba katoto chenyewe kalisita kukimbia,kakaangalia kwenye maji na gafla akajiona sura yake katika maji yaliyokuwa yametulia kwamba aliiona sura yake inafanana na wale Simba wakubwa waliokuwa wakinguruma,baada ya muda akajitambua kwamba yeye sio kondoo Bali ni simba sawa sawa na wale wengine.

Hata wale simba walipokalibia kale katoto cha Simba,gafla wakawa marafiki."

Haleluya...

Umeona hapo,
Na ndivyo hali ilivyo kwako wewe mkristo ujidhaniaye kwamba umefanana kama kamnyama kadogo,lakini kumbe wewe umefanana na Simba mwenye nguvu kiroho.

Sikia hapa,
Bwana Yesu ametufananisha kama kondoo kati ya mbwa-mwitu,mfano huu haikumaanisha sisi ni chakula cha mbwa-mwitu.
Hapana!

Bali maana halisi hapo ni hii;
*Tumefananishwa na kondooo kwa sababu tabia moja wapo ya kondoo ni ,
Kumsikia mchungaji wake.
Na ndio maana ukimchukua kondoo na kumuweka sehemu fulani,ujue kwamba ukirudi utamkuta sehemu ile ile uliyomuacha,

tofauti kabisa na wanyama wengine ambao ukiwaachukua na kuwaweka sehemu fulani basi hao huama na kuamia sehemu nyingine.

Sasa ile tabia ya KONDOO ya kuchungika ndio hiyo Bwana Yesu anayoizungumzia katika Mathayo 10:16

"Angalieni,mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu..."

Sisi ni kweli kabisa tumefananishwa kama kondoo kati ya mbwa-mwitu ikiwa na maana kuwa;
tuwe wasikivu,waelewa kwa kumtegemea mchungaji wetu mmoja ambaye ni BWANA YESU.Maana wenyewe kwa akili zetu hatuwezi kupambana na mbwa-mwitu,Bali tunaweza kwa msaada wa Roho wa Bwana.

Haleluya..

OK,
Sasa,sisi pia ni kama simba katika ulimwengu wa roho.
Tunazo nguvu ndani yetu zitokazo kwa Bwana Yesu maana Yeye BWANA ni Simba wa kabila la Yuda.

Maana yeye tuliye naye ni simba wa kabila la Yuda,
Bwana wa Bwana,
Mfalme wa wafalme,
Bwana wa vita.

Labda nikueleze hivi,kwamba kwa nini mkristo kama Simba,

Simba yule wa kawaida tunayemfahamu sote anasifa kubwa sana,baadhi ya hizo ni hizi sifutazo;

*Simba ni mfame wa mwituni
*Simba ni jasiri sana
*Simba hakubaligi kula mzoga,hupenda kutafuta ndipo hula.
*Simba huthubutu.N.K

Ngoja nikusimulie hii habari,kabla hatujasoma andiko.

"Siku moja nalikuwa mbugani,nikijifunza maisha ya wanyama. Tulipomuona Simba mbele yetu,ilibidi tusimame kwanza maana tulikuwa ndani ya gari. Tulisimama sio kwa kupiga picha la hasha!,

Bali tulisimama kwa sababu simba aliposikia tu sauti ya gari hakukimbia gari,Bali alilikimbilia gari kwa mbele,naye akalala chini, mbele ya gari, wakati muda huo wanyama wengine walikimbia,wakajificha"

Hapa nikajifunza kitu,
Yakwamba Simba ni mfalme wa mwituni,naye ni JASIRI.
Sababu mfalme siku zote hakimbi kimbii mbele ya adui,Bali humkimbilia adui.

Sisi ni uzao mteule,miliki ya Mungu-Sisi ni uzao wa kifamle.
Tunafana na simba wa kibila la Yuda.

Tunasoma;
"Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia,Usilie;tazama,Simba aliye wa kabila ya Yuda,shina la Daudi,yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu,na zile muhuri zake saba." Ufunuo 5:5

Neno linasema usilie...
Nami nakuambia usilie,
Yupo mmoja Simba wa kabila la Yuda,shina la Daudi,Yeye ameshinda
Naye yu hai kwa habari ya maisha yako...

ITAENDELEA...

*Kwa maombezi;
*0655 111149.

UBARIKIWE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni