Jumatatu, 23 Desemba 2013

IBADA MAALUMU YA KRISMASI LUTHERAN JIJINI LONDON KATIKA PICHA

Hapo jana imefanyika ibada maalum ya sikukuu ya Krismasi katika kanisa la St. Anne's Lutheran lililopo jijini London nchini Uingereza na kuhudhuriwa na watu zaidi ya mia moja kutoka Afrika mashariki ambao makazi yao yapo nchini humo. Ibada hiyo iliyoambatana na ubatizo wa mtoto mmoja iliongozwa na askofu Jane akisaidiwa na mchungaji mwenyeji aliyeongoza ibada hiyo Tumaini Kalaghe pamoja na mchungaji Moses Shonga. Baada ya ibada waumini wote walijumuika kwa pamoja kupata chakula kusherehekea Krismasi.



Kwaya ya vijana Anoint ya kanisa hilo ikimsifu Mungu.


Masomo ya Krisimas yalisomwa.




Furaha kwaya wakismifu Mungu.




Askofu Jane na mchungaji Tumaini wakiongoza ibada.




Furaha kwaya ama kwaya kuu wakimsifu Mungu.


Wazazi na wadhamini wakiwa mbele na mtoto tayari kwa ubatizo.







Askofu Jane akimfanyia ubatizo mtoto keisha.


Likifuatiwa na pambio la kusmifu Mungu huku mbatizwaji akiwa mikononi mwa mchungaji Tumaini.






Baadhi ya waumini waliofika kanisani hapo.




Pia kuna mtoto alizaliwa hivyo keki ilikatwa.


Wadau wa GK wakiwa mstari mmoja kwa furaha ya Krismasi.






Baada ya picha kazi ikaanza., Zawadi Machibya wa BBC Swahili akifanya mahojiano.


Na hii ndio ratiba kwa mkazi wa Uingereza

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni