Jumamosi, 7 Desemba 2013
NENO : KUONA NJAA, KUSHIBA , KUWA NA VINGI NA KUPUNGUKIWA
Mtumishi Gasper Madumla.
Tusome WAFILIPI 4 : 12-13
‘’ Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. ‘’
Watu wengi haswa tena wakristo ,wameupotosha maana halisi ya mstari huu,au wamehutafsiri vibaya mstari huu,ila leo fungua moyo wako na upokee.
Mstari huo ahukunzia hapo tu kwamba “ nayaweza mambo yote katika Yeye anitiaye nguvu.”
Hiyo sentensi inayosema kwamba NINAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU,
Bali neno la Mungu limeanzia hapo kwamba ‘’ Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
Sasa kumbe ;
ili uyaweze mambo yote katika Yeye akutiaye nguvu,YAKUPASA UJUE KUONA NJAA,NA KUSHIBA, KUWA NA VINGI NA KUPUNGUKIWA,.
Watu wengi hawapendi kuwa nanjaa,wala kupungukiwa bali hupenda kuwa na vingi na kufanikiwa tu siku zote.
Na hili ni tatizo sugu,mtu wa namna hii HAYAWEZI MAMBO YOTE KATIKA YEYE AMTIAYE NGUVU,maana hajajifunza kuwa na njaa, wala kupungukiwa.Na ndio maana makanisa mengi siku hizi uhubiri juu ya Baraka na kufanikiwa tu kimwili na si kiroho,Hii ni hatari sana.
• KUONA NJAA
Kuna kipindi cha mapito ambacho mimi au wewe mkristo
Ninachotaka kukufundisha hapa katika KUONA NJAA ni wakatri njaa ikujiapo,USIJE UKAMUACHA YESU,maaana njaa ni ya muda mfupi
Njaa yako inawezekana ni kupata mototo,mchumba,mali,nyumba,kuishi katika maisha magumu,kukosa pesa,N.K
Vikujiapo vyote hivi yakupasa kujifuza tu,pia nakuona kama sehemu ndogo sana ambayo Yesu Kristo anaweza kuisawazisha mara moja hiyo hali ya njaa upitayo,hivyo njaa isitutenge na upendo wa Kristo
Tunasoma WARUMI 8 : 35,39
“ Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
Wala yaliyo juu,wala yaliyo chini,wala kiumbe kinginecho chotehakitawezakututenga na upendo wa Mungu ulio katika Yesu Kristo Bwana wetu “
www.mwakasegebibilia.blogspot.com
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni