Jumatatu, 23 Desemba 2013

HATUA SABA ZA KUIMARISHA USHIRIKA WAKO NA MUNGU.(maamuzi saba)

Wa kwanza kulia ni Catherine Mbughi ambae ni mama mchungaji na wa kwanza kushoto ni ALOYCE MBUGHI ambae ndie Mchungaji wa kanisa hili la TAG VICTORY CHURCH,wengine ni watoto wao.
Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha ewe mteule wa MUNGU wetu aliye mbinguni katika makala hii, ambayo inalenga kukujuza na kukuhabarisha njia kuu saba ambazo zitakusaidia kuimarisha mahusiano yako na MUNGU.
Ujumbe huu umetolewa leo madhabahuni katika kanisa la VICTORY CHURCH LA TAG lililopo hapa mkoani ARUSHA eneo la kwa MOROMBO na mwalimu EZEKIELI JOSEPH kutoka jijini DR ES-SALAAM,       KARIBU SASA.
Mstari wa kusimamia.
ZAB 27:4 Neno moja nimelitaka kwa Bwana  nalo ndilo nitakalolitafuta,nikae nyumbani mwa Bwana siku zote za  maisha yangu niutazame uzuri wa BWANA nakutafakari hekaluni mwake.


1.Hatu ya kwanza [KWAME USIPOTEZE NJAA NA KIU YAKO KWA MUNGU,
Usimkinai MUNGU wala kumuona kama hana umuhimu,kwani adui akifanikiwa kuipoteza kiu na njaa hiyo atakupoteza kiimani.Pia kumbuka yya kwamba Mungu ndio dira yetu ukimpoteza utayumba na kuangamia,Usipoteze njaa na kiu mbele ya MUNGU wako ,usikate tama ewe mteule wa MUNGU.
 ZAB 63:1 Ee MUNGU,MUNGU WANGU NITAKUTAFUTA MAPEMA NAFSI YANGU INAKUONEA KIU MWILI WANGU UNAKUONE SHAHUKU KATIKA NCHI KAME NA UCHOVU ISIYO NA MAJI.
 Inasemekana ya kwamba Daudi alikuwa katika jangwa la Yuda lililokuwa kame.Ila kiu inayotajwa hapa inatokana na shahuku na hamu aliyonayo moyoni mwake kuhusu kuimarika kwa ushirika wake na MUNGU,Anaposema MUNGU wangu maana yake anaonesha uhusiano wake na huyu MUNGU.
Unaweza ukawa na habari za MUNGU lakini usiwe na ushirika na Mungu kwa mfano walimu wa thiolojia katika chuo kikuu cha Dar es salaamu unakuta anafundisha bibilia huku mkononi akiwa na kipisi cha sigara, lakini anafundisha tena vizuri ila NENO HILO HALINA UWALISIA KWAKE.
Mfano mwingine ni kwa  wana waiziraeli; waliyajua matendo ya MUNGU ila Musa alizijua njia za MUNGU, wanawaiziraeli walikuwa wakikosa tuu maji wanalalamika.
Katika mapito yeyote unayo pita muite MUNGU wako kama Daudi.
ISAYA 6 soma uwone jinsi Nabii  Isaya alivyokutana na MUNGU, kadiri unavyo zidi kumsogelea Mungu ndivyo utakavyo zidi kubadilika.Kuna matatizo mengine ufumbuzi wake unapatikana katika NENO LA MUNGU,kwani mapito yako anayaelewa, upitapo katika shida yoyote mfanye MUNGU kuwa ni hitaji lako la kwanza.
ZAB 119:2 HERI WAZITIO SHUHUDA ZAKE WAMTAFUTAO KWA MOYO WOTE.
HERI maana yake ni baraka,pia kuzitii shuhuda zake ni kuzitunza na kuzifanya kuwa ni sehemu za maisha yako.Yaani heri wale wamfanyao BWANA kuwa sehemu ya kwanza ya maisha yao.Watu walio muweka MUNGU kama hitaji lao la kwanza kwenye maisha yao ni wenye heri yaani baraka.
Unapokuwa mbali na MUNGU unapoteza ushirika nae hali amabayo itakufanya kuwa mpagani angali bado upo kanisani,tafuta muda kaa jifungie lia na MUNGU wako.
Mpendwa hauna budi kukumbuka ya kwamba MUNGU sii mganga wa kienyeji kwa hiyo usimfwate ili akutajirihse hata kama asipo kutajirisha endelea kumwabudu kwani hata ukifilisika yeye atabaki kuwa MUNGU.
Jenga tabia ya kukutana na MUNGU mapema asubuhi, huwezi kuubadilisha ulimwengu kama huna ushirika na MUNGU.Hakikisha una soma neneo kila siku,maombi na kumsifu MUNGU aliye hai.
Kwaleo tunaishia hapo na tafadhali kesho tufwatilie ili uapte mwendelezo wa sehemu inayo fwata,
LANGU JINA NI OSCAR SAMBA, nimeokoka na ninampenddaa YESU WEWE JE?
Kama bado basi ungana nami kwenye sala hii kisha utaokoka kumbuka kuokoka sio dini mpya bali ni mwanzo mpya na MUNGU WETU ALIYE MBINGUNI , tuanze sasa;
“Ee MUNGU WANGU ULIYE MBINGUNI MIMI NI MWENYYE DHAMBI NA MIMESIKIA HABARI ZAKO NA KUZIAMINI EWE YESU NI SAFISHE KWADAMU YAKO NA UNIKOWE”

Ongera kwa kuokoka na sasa tafuta kanisa la walokole linalo hubiri injli iliyo hai,siku njema na endelea kuifwatilia blogu hii ya www.mwakasegebibilia.blgspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni