Alhamisi, 26 Desemba 2013
SOWETO GOSPEL CHOIR KUREJEA AFRIKA YA KUSINI BAADA YA ZIARA BARANI ULAYA
Soweto Gospel Choir ©SGC
Baada ya ziara ya takribani miezi miwili barani ulaya, kundi la Soweto gospel choir linatarajia kurejea nyumbani kwao Afrika ya kusini mwishoni mwa wiki kujiunga na familia zao kusherehekea mwaka mpya. Kundi hilo ambalo kwasasa lipo nchini Ujerumani likimalizia ngwe yake, lilikuwa katika ziara ya kusherehekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.
Kati ya mambo ambayo waimbaji wa kundi hilo walionekana kutoamini macho yao ni pale walipofanya onyesho lao mjini Monaco nchini Ufaransa wiki mbili zilizopita ambapo mwisho wa onyesho hilo malkia wa Monaco princess Charlene alikwenda jukwaani ili kupata picha ya pamoja na kundi hilo ambao pia walimwimbia wimbo wa taifa la Afrika ya kusini. Malikia huyo aliwatumia picha hiyo kwa njia ya bahasha, kitendo hicho cha kupiga picha na malkia huyo kiliwafurahisha waimbaji wa kundi hilo hususani wadada ambao hawakuacha kuelezea furaha yao kupitia mitandao ya kijamii kama facebook na instagram ambako waliweka picha wakiwa na malikia huyo.
Nikiwa na Shimmy pamoja na Sipokazi kati ya nguzo na viongozi na waimbaji wa Soweto gospel choir walipofanya onyesho lao ukumbi wa wimbledon theatre jijini London mwezi uliopita.
Kundi hilo ambalo lipo kwenye ziara limebeba wakongwe wengi ambao wapo kundini toka kuanzishwa kwake huku kundi ambalo limebaki Afrika ya kusini ambalo pia lilishiriki kwenye msiba wa mzee Nelson Mandela liko na waimbaji wengi wapya na wachache wakongwe ambao walibaki kutokana na majukumu mengine yakifamilia. Baada ya sherehe za mwaka mpya kundi hilo litarudi njiani kuelekea Marekani ya kaskazini kuendelea na ziara yao.
Soweto gospel choir wakiimba wimbo wa taifa lao jukwaani nchini Ufaransa nyuma picha ya Nelson Mandela katika kumuenzi ilipotangazwa kuwa amefariki.
www.mwakasegeinjili.blogspot.com
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni