Alhamisi, 5 Desemba 2013

JUMAPILI HII HAPATOSHI KIJITONYAMA LUTHERANI, SOMA MWENYEWE


Baadhi ya wamama wa Tumaini wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ibada ya uzinduzi wa album yao mpya na mabasi mawili ya kwaya hiyo.
Wapenzi wa kwaya ya Tumaini Shangilieni kutoka kanisa la Mtakatifu James Anglikana Arusha waishio jijini Dar es salaam, jumapili hii wanatarajiwa kuwa na nafasi ya kipekee kuiona kwaya hiyo ikimtukuza Mungu katika kanisa la Kilutheri Kijitonyama jijini Dar es salaam ikiwa nikatika kusheherekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwa kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama.

Kwaya hiyo ambayo ilikuwa nchini Afrika ya kusini wiki iliyopita imekuwa katika mazoezi katika usharika wao jijini Arusha wakifanyia mazoezi nyimbo zao za zamani ambazo wapenzi wao wangependa kuzisikia pamoja na nyimbo mpya kutoka katika album yao iitwayo "Nisamehe"lakini pia wanatarajia kuachia surprise moja kwa watu watakaohudhuria.




Wenyeji Uinjilisti Kijitonyama wakienda sawa na Modest Morgan.
Jumapili inatarajiwa kuwa siku ya kipekee katika usharika wa Kijitonyama kwani wenyeji Uinjilisti Kijitonyama ambao wanajulikana kwa nyimbo mbalimbali zilizowapa umaarufu, siku hiyo wataimba nyimbo zao za zamani sambamba na waimbaji waliowahi kuimba katika kwaya hiyo siku za nyuma, wakiwemo masolo maarufu kutoka kundi la Kijitonyama Upendo Group ambao kabla ya kuanzishwa kwa kundi hilo walikuwa waimbaji wa kwaya ya Kijitonyama.



Baadhi ya waimbaji wa Tumaini Arusha wakiongozwa na mwenyekiti wao Dkt. Emanuel Mtangoo upande wa kuume.ww.mwakasegebibilia.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni