Jumatano, 11 Desemba 2013

WEZI WAVUNJA NYUMBANI KWA ASKOFU DESMOND TUTU AKIWA MSIBANI


Askofu mkuu mstaafu wa kanisa Anglikana Afrika ya kusini, Desmond Tutu ©standard

Polisi wamesema wizi huo ulifanyika wakati bwana Tutu akiwa katika ibada ya Nelson Mandela Mjini Johannesberg.
Aidha wameelezea kuwa uvamizi ulifanyika nyumbani kwake mjini Cape Town Ahamisi jioni baada ya kutoa hotuba katika ibada ya Mandela siku hiyo.Inaarifiwa Tutu aliibiwa vitu vyake wakati akiwa anahudhuria ibada maalum ya kumuaga Hayati Nelson Mandela siku ya Jumanne.
Ibada hiyo ilifanyika katika uwanja wa FNB mtaani Soweto.
Wizi na uvamizi wa nyumba za watu ni jambo la kawaida nchini Afrika Kusini ambako visa vya uhalifu viko juu sana.
Chanzo BBC SWAHILI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni