Jumatatu, 9 Desemba 2013

SHAMRA SHAMRA ZA MIAKA 25 YA KWAYA YA UINJILISTI KIJITONYAMA ILIVYOFANA


Kijitonyama Lutheran .

Jana ilikuwa jubilee ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama Lutheran jijini Dar es salaam, jubilee hiyo iliyokuwa ya aina yake ilihudhuria na mamia ya washarika wa kanisa hilo, waimbaji wasasa na wazamani, wageni waalikwa, ndugu jamaa na marafiki wa kwaya hiyo, ikiwemo kwaya ya Tumaini Shangilieni Arusha ambao kazi yao ilikuwa njema.

Kati ya matukio ya kupendeza ilikuwa ni uzinduzi wa nembo mpya ya kwaya hiyokusikia historia jinsi kwaya hiyo ilivyoanzishwa, kwaya ya Tumaini kuimba wimbo wa Naburudika wa Kijito huku wenyeji nao wakiimba wimbo wa Hakuna Mungu kama wewe ulioimbwa na Tumaini katika album yao iliyopita.

Lakini kubwa zaidi na lakupendeza ni uwepo wa mwanadada Lilian Mlelwa ambaye alikuwa mwimbaji nyota wa kundi la Kijitonyama Upendo Group kabla yeye na mumewe kutoka kundini humo hapo jana alikuwa sambamba na kwaya yake hiyo akikumbushia enzi hizo alipokuwa mmoja wa masolo wa kutegemewa wa kwaya.

Lakini awali kama uliwahi kusoma KWA TAARIFA YAKO ya kwanza kabisa tulikufahamisha kwamba kundi la Kijitonyama Upendo Group lilizaliwa ndani ya kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama.



Kijito Uinjilisti ilikuwa full hapo jana hata jukwaa lao lilikuwa dogo, hii ndio namba ilivyokuwa enzi hizo.



Mwenyekiti wa kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama bwana Emanuel Shedo akizungumza kuhusu uzinduzi wa nembo itakayokuwa ikitumiwa na kwaya hiyo.



Baadhi ya waimbaji wa Tumaini wakiwa jukwaani.



Baadhi ya wapigaji wa kwaya ya Tumaini wakiongozwa na John Mtangoo akikung'uta gitaa la solo ndani ya Kijitonyama.



Witness na wenzake wa Shangilieni wakimuabisha shetani ndani ya Kijitonyama hapo jana.



David Mosha na mkewe pamoja na wadhamini wengine wa kwaya ya Kijito wakiongozwa na Riki wakiwa katika mapozi ya kuchangia huduma ya kwaya hiyo.



Nembo ya kwaya ya uinjilisti Kijitonyama ambayo ilizinduliwa hapo jana.



Kijito Uinjilisti wakiwa jukwaani ndani ya pamba mpya.



Uinjilisti Kijito wakiwa katika pamba nyingine mpya, Lilian Mlelwa wa pili kutoka kulia akiwa sambamba na solo nyota wa sasa wa Kijito Oliver Mujumba.



Ibada ikiendelea.



Baadhi ya waimbaji wa Tumaini wakiwa nje ya jengo la Kitega uchumi cha Kijitonyama Lutheran baada ya ibada.


Walipendeza kwa hakika.



Mapozi sasa ya watumishi wa BWANA



Furaha baada ya huduma ilikuwa mwendo wa picha tu.



Kusamba wa Tumaini akiwa na wanakwaya wa Kijito



Picha ya pamoja kwa baadhi ya wanakwaya wa Kijito na Tumaini.Picha kwa hisani ya mdau wa GK Samuel Kusamba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni