Jumatano, 11 Desemba 2013

KWA TAARIFA YAKO : JE UNAJUA KWANINI FLORA MBASHA ANAAMBATANA NA MUMEWE KILA MAHALI?

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


KWA TAARIFA YAKO hii leo tupo kwa mjukuu wa gwiji la injili Tanzania marehemu Dkt. Moses Kulola huyu si mwingine bali ni Flora wa Emanuel Mbasha ambaye ni kati ya nyota wa muziki wa gospel nchini Tanzania, kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa mwimbaji huyu tangu aanze uimbaji na kujulikana ndani na nje ya nchi kupitia katika nyimbo zilizomtambulisha kama "Jipe moyo utayashinda, Tanzania, Mwanamke simama imara, Aliteseka BWANA Yesu na nyingine nyingiii.


KWA TAARIFA YAKO tangu Flora aanze kuonekana majukwaani akimtukuza Mungu mimi binafsi kama GK sijawahi kumuona akiwa peke yake bila uwepo wa mumewe bwana Emanuel Mbasha lakini wajua Flora mwenyewe anasemaje juu ya kampani ya mumewe kila anakokwenda ambapo na hivi sasa pia bwana Mbasha naye ameanza kutoa nyimbo zake? KWA TAARIFA YAKO Flora aliwahi kusema kupitia GK kwamba anajisikia furaha sana kuwa na mumewe kokote aendako kwakuwa anajisikia amani na ulinzi juu kitu ambacho anasema anafurahia sana katika maisha yake ya ndoa.



Flora na mumewe Emanuel Mbasha wakihudumu nchini Marekani.
KWA TAARIFA YAKO Flora akaenda mbali zaidi kwakusema anampenda Mbasha ndio maana alichagua kuolewa na Emanuel Mbasha nasio mtu mwingine kwakuwa ndio maisha yake, zaidi ni mpango wa Mungu yeye kuwa na Mbasha na kwahivyo basi ataendelea kumpenda daima ili ndoa yake izidi kuimarika kila siku, amesema ni nadra sana kuwakuta hawako pamoja ni muda wote wapo pamoja kwa umoja.
KWA TAARIFA YAKO Flora na mumewe tayari wamefanya huduma katika nchi za nje Marekani ambako walihuduma kwa takribani miezi mitano, wakaalikwa nchini Uingereza ambako walikaa kwa takribani wiki mbili, lakini pia wametembelea Afrika ya kusini, Congo, Kenya, Zambia na nchi nyinginezo na kote huko ni kama kawaida wapo wawili. Flora amewataka waimbaji wa muziki wa injili kuwa mfano kwa jamii inayowahubiria ili kusiwepo sababu za jamii hiyo kuwanyoshea vidole, hata vikiwepo basi visiwe na ukweli wowote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni