Jumanne, 3 Desemba 2013

KIRK FRANKLIN JUKWAA MOJA NA JOYOUS CELEBRATION


Kirk Franklin@praisecleveland
Kundi la Joyous Celebration linatarajiwa kuimba jukwaa moja na nyota wa muziki wa injili duniani Kirk Franklin kutoka nchini Marekani katika tamasha kubwa linalotarajiwa kufanyika jumapili hii katika uwanja wa Griquas Rugby Park uliopo Kimberly kaskazini mwa Cape.

Kirk akiwa amemkumbatia Ntokozo kutokana na uimbaji wake.

Katika tamasha hilo Joyous watakuwa wakimsindikiza kiongozi wao mchungaji Jabu Hlongwane ambaye ndiye aliyekaribishwa rasmi lakini ataambatana na kundi hilo. Aidha waimbaji wengine katika tamasha hilo ni pamoja na kijana Khaya Mthethwa mshindi wa mwaka jana wa Idols Afrika ya kusini akiwa pia mwimbaji wa kundi la Joyous Celebration akiambatana na Alive gospel kwaya.

Hii si mara ya kwanza kwa mwanamuziki Kirk Franklin kufika nchini humo kwa matamasha ambapo aliwahi kushiriki katika moja ya matamasha mwaka 2007 katika tamasha lililoitwa "One World concert" katika ukumbi wa ICC Durban, na kushangazwa na uimbaji mahiri wa mwanadada Ntokozo Mbambo mke wa Nqubeko Mbatha ambao wote kwa pamoja waliwahi kuwa waimbaji wa Joyous wakishirki katika uimbaji pamoja na nyadhifa nyingine Nqubeko akiwa mwandaaji mkuu wa muziki wa kundi hilo huku Ntokozo akiwa mkufunzi ama mwalimu wa sauti katika kundi hilo.

Wakati huo huo mashabiki watakaohudhuria tamasha hilo watabahatika kuona viwango zaidi vya kundi la Joyous wakati huu likijiandaa kurekodi DVD yao ya 18 mwezi huu nchini Afrika ya kusini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni