Jumatatu, 2 Desemba 2013

KWETU PAZURI YAWAKONGA WAZAMBIA


Sarah Uwera akitambulishwa mbele ya umati wa watu(hawaonekani pichani) wakati wa tamasha lao uwanja wa Levy Mwanawasa uliopo Ndola nchini Zambia.
Kwaya ya Ambassadors of Christ kutoka Rwanda ambao walikuwa ziarani nchini Zambia wamemaliza ziara yao kwa mafanikio baada ya mwitikio mkubwa wa watu wa nchini humo ambao walikuwa na hamu kuliona kundi hilo.

Katika matamasha matatu waliyofanya nchini humo inadaiwa kwamba wengi waliohudhuria walikuwa na hamu ya kuwaona waimbaji hao ingawa pia waliuzika na mtindo wa kwaya hiyo kutumia CD badala ya kuimba live. Kati ya jumbe za Facebook ambazo GK imebahatika kuzisoma kuna baadhi ya waliohudhuria kutamani kurudi nyumbani kusikiliza CD badala ya kuangalia maigizo ya waimbaji hao.

Licha ya hayo yote kwaya hiyo inatarajiwa kurejea tena nchini Zambia mwakani ingawa tarehe na mwezi bado haijajulikana.



Baadhi ya waimbaji wa Ambassadors wakiwa na wafanyakazi uwanja wa ndege wa Zambia.


Wakiweka sawa mambo ya uhamiaji uwanja wa ndege.


Furaha pamoja na mwenzie wakiwa katika basi maalumu kuwapeleka kanisani walipofikia.




Basi likiwa na waimbaji wa Ambassadors of Christ mbele ya kanisa la Kisabato Libala.




Hapa nikatika tamasha lililofanyika juzi jumapili uwanja wa Levy Mwanawasa.



Waimbaji wakitambulishwa mbele ya watazamaji.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni