PICHANI NI WANAKWAYA WA KANISA HILI LA VCC WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA MADHABAHUNI,picha na makitaba mwanzoni mwaka huu. |
NA OSCAR SAMBA.
Hakika ni siku nyingine
tena iliyosheheni utukufu mkuu wa MUNGU wetu wa mbinguni,Kwa jina la BWANA wetu
YESU KRISTO nina kukaribisha katika makala hii inayo zungumzia Kuzaliw akwa
YESU pamoja vitu muhimu vinavyo ambatana na sikuu hiyo.
Ujumbe huu
umetolewa jana madhabahuni katika kanisa la VICTORY CENTRE LA TAG lililopo hapa
mkoani ARUSHA eneo la kwa MOROMBO na mwalimu EZEKIELI JOSEPH kutoka jijini DR
ES-SALAAM,
Bila
kupoteza muda na tutazame maandiko; MATHAYO 2:1-12.
Mpendwa ukisoma
maandiko hayo utaona Yesu alivyozaliwa katika bethilehemu ya uyagudi enzi za
mfaulme Herode,,Ukiendela utaona jinsi mamajusi walivyo tazama nyota na kwenda
kumuona YESU pia walimtolea zawadi nyingi.
Wengine
wanafikiria ni wanawake kwa sababu wanaitwa mamajusi na wengine wanazani ni
mijusi,,MAMA JUSI NI WINGI UMOJA NI MAJAS,ndini ya ZOROTEANISM ilianzishwa Iran
kabla ya YESU ilikuwa ni dini kubwa ya WAHAMEDI na WAHEDENI ambao makuhani wao
waliitwa hivyo.
Walikuwa
wakisomea elimu za nyota na zakishirikina za kusoma nyota.
Chakushangaza
ni kwanini MUNGU alijifunua kwa watu hawa ,Ila nimegundu haya kwamba MUNGU
humtumia mtu yeyote,
MTHAYO 16:2-3 akajibu akawaambia kukiwa jioni mwasema Kutakuwa kianga kwa
maana mbingu ni nyekundu,,,na asubuhi mwasema leo Kutakuwa na dhoruba kwa maana
mbingu ni nyekundu,tena kumetanda.Enyi wanafiki mwajua kuutambua uso wa mbingu
bali Ishara za zamani hamuwezi kuzitambua.
Manaeno haya
YESU alikuwa akizungumza na watu wenye uwezo wa kutambua mambo kupitia sanyansi
ya asili,ambayo ni miongoni mwa hizo elimu za kusoma nyota..Elimu hii ilikuwa sana
kule mashariki ya kati, na baadae kuonekana paka kwa wayahudi.
Wahubiri wengi
hutumia andiko hilo kuhubiri mafundisho ya kusafisha nyota ila kibibilia
mafundisho hayo hayapo; yanayo halalisha mahubiri hayo.
Habari ya
kusafisha nyota ni mambo ya wanajimu nasio walokole,Mafundisho ya kusafisha
nyota ni utapeli kama utapeli mwingine.
Torejee tena
kwenye somo letu,Kusudi la safari yao (MAMAJUSI) ili kuwa ni kumwabudu MFALUME,
kuabudu kwao kulifunua tabia tatu za mwabudu wa kweli.
1.FURAHA, MATHAYO 2:10, NAO
WALIPO IONA ILE YOTA WALIFURAHI KWA FURAHA KUBWA.
Kuabudu ni
jambo la furaha kwa mwabudu linalotokana na furaha ya kweli kwa MUNGU wake
,wito wetu wa kwanza ni kumwabudu MUNGU,katika kuabudu ndipo unaweza kuitwa
MCHUNGAJI au MWINJILISITI….
Unapo
mwabudu MUNGU kwa furaha unakutana na furaha yake pia furaha ya MUNGU ni nguvu
tele.
ZAB 16:11, UTANIJULISHA NJIA ZA UZIMA MBELE ZA USO WAKO ZIKO FURAHA
TELE NA KATIKA MKONO WAKO WA KUUME KUNA
MEMA YA MILELE.
Kama adui
atafanikiwa kuiba furaha yako basi amekwisha kukupokonya nguvu na ukishaishiwa
nguvu ni dhairi ya kwamba umekwisha kushindwa.
2.HALI YA UNYEYEKEVU,
Lilionekana pale walipo msujudia mototo mdogo
MATHAYO
2:11A. WAKAINGIA
NYUMBANI WAKAMUONA MTOTO PAMOJA NA MAMAYE MARIAMU, WAKAANGUKA WAKAMSUJUDIA.
Unyenyekevu
ni jambo la kiroho na linaanzia kwenye MOYO wa mtu,
MATHAYO 11:29-30
JITIENI NIRA YANGU MJIFUNZE KWANGU KWA KUWA MIMI NIMPOLE
NA MNYEYEKEVU WA MOYO. KWA KUWA NIRA YANGU NI LAINI NA MZIGO WANNGU NI MWEPESI.
Nira ni ile
ambayo wanaolima kwa kutumia ng’ombe huwafunga shingoni ila ile ni nzito na ni ngumu
kwani huwachubua shingoni.Lakini YESU anasema ya kwake ni nyepesi na ni laini.
Kama hakuna
unyenyekevu hakuna KUABUDU badala yake kuna mizaha ya kidini,Unyenyekevu ni
maisha ya kiroho ya mwamini hakuna.Mambo ya kiroho ynahiytaji unyenyekevu
mkubwa.
ISAYA 6. Ukisoma utamuona Isaya alivyo waona
malaika walivyo kuwa wakimwabudu MUNGU na kufunika sura zao; kwa maana hiyo
walitaka MUNGU aonekane nasio wao,mfano wapo wachungaji na wahubiri ambao
hutaka waonekane wao kwanza nasio MUNGU.
Ukifanya
mabo ya YESU iliwewe utukwizwe safari yako ya kiroho haitakuwa ndefu,
3.WALITOA, UTOAJI UNAENDANA NA KUABUDU,
MWANZO 2:5- IBRAHIMU AKAWAMBIA VIJANA WAKE KAENI
HAPA NITAENDA NA KIJANA KUABUDU NA KUWARUDIA TENA, BASI IBRAHIMU AKAMTWIKA ….
Isaka
alifundishwa kuabudu kwa njia ya kumtolea MUNGU,tuwafundishe watoto wetu kumtolea
MUNGU. Wapo watu wanaohitaji kubarikiwa kama IBRAHIMU lakini hawahitaji
kutembelea kwenye njia alizo tembelea IBRAHIMU,nisawa na kusubiri meli kwenye
stendi ya ubungo jambo ambalo haliwezekani ila ukiisubiri bandarini inawezekana.
Kwa hiyo
huwezi kubarikiwa bila kufwata kanuni .MUNGU wetu hafanyi kazi nje ya NENO,Watu
wapo tayari kuoga uchi njia panda,kukaa kwenye makaburi usiku kucha na kula
nyama za watu, ikiwa ni mashariti ya mganga wa kienyeji.
Ila kwa mambo
ya rohoni watu hawako tayari kumtii MUNGU, kwa namna yoyote ile,kama kunamchawi
wa kwanza katika maisha yako ni wewe mwenyewe fanya kile kitu ambacho MUNGU
anataka ufanye,usipotoa hautafanikiwa; maisha yako yana hubiri kuliko maneno yako
yenyewe.
Utoaji wa
fungu la kumi hatutoi kama sheria toa kama upendo,wapo watu ambao saluni
hutumia fedha nyingi lakini hutoa kidogo.Mtu yuko tayari kukaa saluni masaa
saba ila mbele za MUNGU hakai masaa saba.Kusuka sio dhambi ila ni vizuri kuweka
usawa.
Soma ..MALAKI 1:6-8 METHALI 3:9
Fedha ambazo
unazizuia kwa MUNGU zitaenda sehemu nyingine.
Tutazame
jinsi ambavyo MAMAJUSI WALIVYO MTOLEA MUNGU;
1.DHAHABU,
ili kuwa ni zawadi ambazo wakipewa wafalume au watawala.Watu hawa walielewa
nafasi ya YESU kama MFALUME.Ingawa watu hawa hawakuwa na ufahamu wa kutosha kwa
MUNGU ila walitoa.
Unapo toa
vitu vya dhamana kwa MUNGU unaonesha ni kwajinsi gani unavyo mjali,
2.UVUMBA, uvumba uliashiria kazi ya kikuhani (KUHANI
MKUU) walikuwa wakivukisha sehemu ya PATAKATIFU-PAPATAKATIFU kwa maana nyingine
walimtambua YESU kama KUHANI MKUU.MAKUHANI wa AGANO LA KALE ili kuwa ni kivuli
cha YESU,UKUHANI wao haukuwapa kibali watu kuingia mbele za MUNGU ila UKUHANI
wa YESU umetupa nafasi ya kuingia wote.Kwahiyo unaouwezo wa kenda mbele zake.
3.MANEMANE, manemane hili ni dawa ya kuzikia miili ya watawala iliyogunduliwa
miaka ya 300 kabuka ya KRISTO,zilipakwa ili wasioze.
Kwa maana
nyingine zilitabiri kifo cha YESU,ndo maana baada ya kifo chake wanafunzi wake
walipaka mwili wake manukato ambayo ndiyo manemane.
KUABUDU NITENDO LA UFUNUO.
YOHANA 4:24 MUNGU NI ROHO NAO WAMWABUDIYE YEYE YA WAPASA KUMWAMUDU
KATIKA ROHO NA KWELI.
Zamani
walikuwa wakiabudu katika sehemu mbalimbali na hapo walikuwa wakibishana na
kuvutana katika sehemu ya kuabudu, kwa
pamoja tusome..
EFESO 2:1 NANYI MLIKUWA WAFU KWA SABABU YA
DHAMBI NA MAKOSA YENU.
Mtu kama
hajaokoka ni mfu,kama mtu amekufa kiroho hawezi kuabudu,wengine wajua ya kwamba
kuabudu ni kupiga magoti au kuimba nyimbo za polepole ila kuabudu ni UFUNUO WA
ROHO YA MTU.Mafarisayo na Makuhani pia Waandishi walikosa huo ufunuo ingawaje
waliyajua hayo yote.
Mpe YESU
nafasi ya kwanza moyoni mwako unapo mwabudu weka pembeni mabo yote elimu,cheo
au fedha.MAMAJUSI MUNGU aliwapa UFUNUO wa kipekee ambao uliwafanya wa MTAMBUE
YESU KAMA MFALUME.
Kuabudu ni
maisha yako ya kila siku, hakikisha unaishi maisha ya ibada,wapo watu ambao
kanisani wanongea ila nyumbni haongei huo ni usanii wa wakaida haya ni maonesho
ya kidini na mizagha,Ibada ni mfumo wa
maisha yetu kinyume cha hapo ni USANII.
Tengeneza
kila wakati,YAKOBO aliwakaja watu kuacha
makorokoro yote ili waka MWABUDU MUNGU.Kila unalolitenda hakikisha ni
jema,Kabla ya kuusogelea utukufu wa MUNGU.
YESU AZALIWE KWENYE MOYO WAKO.
MATHYO 15:18-19
MIMI nimeokoka na ninampenda YESU
WEWE JE?
Kama bado
basi ungana nami kwenye sala hii kisha utaokoka kumbuka kuokoka sio dini mpya
bali ni mwanzo mpya na MUNGU WETU ALIYE MBINGUNI , tuanze sasa;
“Ee MUNGU WANGU ULIYE MBINGUNI MIMI NI MWENYYE DHAMBI NA
MIMESIKIA HABARI ZAKO NA KUZIAMINI EWE YESU NI SAFISHE KWADAMU YAKO NA UNIKOWE”
Ongera kwa kuokoka na
sasa tafuta kanisa la walokole linalo hubiri injli iliyo hai,siku njema na
endelea kuifwatilia blogu hii ya www.mwakasegeinjili.blogspot.com
ONGERA KWA INJILI
JibuFuta