WAKWANZA KULIA NI MCH. WA KANISA HILI LA VICTORY CENTRE ALOYCE MBUGHI NA WA KWANZA KUSHOTO NI MAMA MCH. CATHERINE MBUGHI. |
Ninayo
furaha ya hali ya juu kukukaribisha hususani ewe uliye mpenzi wa blogu hii ya www.mwakasegeinjili.blogspot.com,
siku ya leo kama ilivyo kuwa jana
ninakuletea muendelezo wa somo la HATUA SABA ZA KUIMARISHA USHIRIKA WAKO NA
MUNGU.(maamuzi saba).
Kwa uwezo wa
YESU KRISTO na tumaini tutakuwa pamoja na kufanyika kazi,kabla hatuja endelea
na hatua ya pili, tafadhali kama uliikosa hatu ya kwanza bonyeza link hii ili
usome sehemu ya kwanza kisha ndipo uendelee na sehemu hii ya pili, http://mwakasegeinjili.blogspot.com/2013/12/hatua-saba-za-kuimarisha-ushirika-wako.html#more
Kabla ya
kukujuza hatua ya pili kwanza tujikumbe mstari wetu wa kusimamia,
ZAB 27:4 Neno moja nimelitaka kwa Bwana nalo ndilo nitakalolitafuta,nikae nyumbani
mwa Bwana siku zote za maisha yangu
niutazame uzuri wa BWANA nakutafakari hekaluni mwake.
Andiko hili
linatufundisha ya kwamba Daudi alilipa kipaumbele jambo hili ili atafakari uzuri
wa MUNGU.
Hatua ya pili, HUUISHA JUUDI YAKO KUTAKA KUMJUA YEYE KWA UKARIBU ZAIDI.(yeye maana yake ni MUNGU, Neno
kuuwisha maana yake kufufu)
Tafadhali soma name mstari huu,WAFILIP 3:10 ILI NI MJUE YEYE, NA UWEZA WA KUFUFUKA KWAKE , NA
USHIRIKA WA MATESO YAKE NIKIFANISHWA NA KUFA KWAKE .
Kwa ajili ya
YESU Paulo aliacha mambo ambayo yalikuwa ya mpe au yaliyomfanya aonekane kama
ni mtu mwenye sifa na heshima kubwa sana kwa watu kwani alikuwa ni msomi wa
hali ya juu na mwalimu wa torati na pia litoka katika kabila la Benjamini ambalo
ndilo kabila la kwanza kumtoa mfalume ambae ni Sauli pia alikuwa ni mwebrani
aliye kijua kiebrania.Ila kwa ajili ya Mungu aliviacha hivyo vote.
Mpendwa
MUNGU hujifunua kwa mtu kulingana na kiu na shahuku aliyonayo kwake.Wanathiolojia wanasema ya kwamba wakati
Paulo antoa kauli hiyo alikuwa na mika thelathi ya kutembea na YESU KRISTO
lakini bado kwake haikutosha kutokuwa na shahuku ya kuendelea kumjua MUNGU.
Paulo
alihitaji kuzama ndani zaidi yaani hakutaka kuwa na uhusiano wa juu juu, ndugu
msomaji siju shahuku yako ni ipi ila mtume PAULO shahuku yake ilikuwa ni kumjua
MUNGU.
Katika
shahuku hii yake ndipo MUNGU alijifunua kwake zaidi kwani ndie mwenye mchango
mkubwa zaidi kweyne AGANO JIPYA ,,unapo soma karama tano,HUDUMA TANO ni mtume
PAULO.
Hayo yote ni
matunda na matokeo yake kutokakana na shahuku yake ya kumjua MUNGU,,Wanatheolojia
wanasema ya kwamba katika ulimwengu alioishi PAULO hakukwepo mtu aliye mcha
MUNGU kama yeye.
Laiti kama dunia
ingemtafuta MUNGU kama inavvyo tafuta fedha kwani watu huamka alufajiri,huamua
kuchimba madini na shuhuli ngumu ili wapate fedha ila kwa MUNGU wengi ni wavivu
hadi wasukumwe, Ila PAULO hakuwa hivyo alijiwekeza kwa MUNGU zaidi.
Tuachane na
ukristo wa kidini dini, tuzame ndani zaidi,Ukiwa na ushirika wa karibu na MUNGU
utaitambua sauti yake .
YOHANA 10:4 NAYE AWATOAPO NJE
KONDOO WAKE WOTE,HUWATANGULIA; NA WALE KONDOO HUMFWATA KWA MAANA WAIJUA SAUTI
YAKE.
Kuna
mmarekani mmoja alienda mashariki ya kati na kuwakuta wachungaji wakilaza
kondoo katika pango moja na inapofika asubuhi mchungaji moja huwaita kondoo
wake nao humfwata na mmarekani Yule alijaribu kuvaa nguo zayule mchungaji
akawaita lakini hawakuja,kwa nini ? kwa sabau hawakuijua sauti zake.
Tazama tena
andiko hili,
ZAB
103:7 ALIMJULISHA
MUSA NJIA ZAKE WANAWAIZIRAELI MATENDO YAKE.
Pia tembelea
andiko hili,KUTOKA 33:1-10 Utaona
jinsi ambavyo MUSA alivyo kuwa akishirikiana na MUNGU.,NI vizuri kuyajua
matendo ya MUNGU kama wana waiziraeli, ila ni vizuri zaidi kuzijua njia zake
kama MUSA.Wanahistoria wanasema ya kwamba hakujawai kutokea nabii ambae
alitembea na MUNGU kama MUSA.
Musa aliijua
sauti ya MUNGU haraka,,Njia za kumjua MUNGU ni kusoma NENO kwa bidii kwani
unaposoma NENO MUNGU husema nawe, pia MAOMBI na KUABUDU,KUSHUKURU,KUSIFU, na
pia SADAKA.
1TIMOTHEO 2.1 BASI KABLA YA MAMBO YOTE NA TAKA
DUA,
DUA ni
maombi ya kusihi.
SALA ni
mazungumzo kati yako na MUNGU. Kukemea sio maombi kwani maombi ni yale ambayo yanaelekea
kwa MUNGU.
MAOMBEZI, ni
pale unapo ombea kanisa,nchi mtu au sehemu Fulani pia SHUKURANI ni maombezi.
Hatuwezi
kumjua MUNGU pasipo NENO, MUNGU wetu anaishi katika NENO.Lazima uwe na kawaida
ya kulisoma NENO kila uchwao.
Unapo
endelea kumsogelea MUNGU hautahitaji maombi kwani yataondoka yenyewe kwani
MUNGU wetu ni moto ulao, kwenye moto mende na nzi hawasoge.
Tatizo la
wakisto wanataka kuishi leo kama enzi za agano la kale kwani zamani watu wache
ndio waliokuwa wakiingia kwenye PATAKATIFU-PATAKATIFU ila toka pazia lipasukuke
pale YESU akiwa msalabanii sasa kila mtu anayo haki ya kumwendea MUNGU wetu.
Tutazame
kitabu cha,
DANIELI 11:12 NA WALE WAMJUAE MUNGU WATAKUWA HODARI NA WATENDA MAMBO
MAKUU.
Maana yake
watu wasiomjua MUNGU wao hawawezi kuwa hodari na hawataweza kufanya mambo
makuu,Danieli alipitia nyakati Ngumu lakini alishinda kwani alimjua MUNGU
wake,Danieli alikuwa ni mtu wa maombi hata pale walipo tafuta makosa kwake
waliyakosa hadi ikabidi wayatafute kwa ushirika wake na MUNGU wake; ilibidi wa
mtupe kwenye simba.Simba hawezi kumtafuna mtu mwenye ukaribu na MUNGU.
Unaweza
kuishi kama mfalume utumwanai kama unamjua MUNGU,
Ujumbe huu
umetolewa leo madhabahuni katika kanisa la VICTORY CENTRE LA TAG lililopo hapa
mkoani ARUSHA eneo la kwa MOROMBO na mwalimu EZEKIELI JOSEPH kutoka jijini DR
ES-SALAAM,
LANGU JINA NI OSCAR SAMBA, nimeokoka
na ninampenddaa YESU WEWE JE?
Kama bado
basi ungana nami kwenye sala hii kisha utaokoka kumbuka kuokoka sio dini mpya
bali ni mwanzo mpya na MUNGU WETU ALIYE MBINGUNI , tuanze sasa;
“Ee MUNGU WANGU ULIYE MBINGUNI MIMI NI MWENYYE DHAMBI NA
MIMESIKIA HABARI ZAKO NA KUZIAMINI EWE YESU NI SAFISHE KWADAMU YAKO NA UNIKOWE”
Ongera kwa kuokoka na sasa tafuta
kanisa la walokole linalo hubiri injli iliyo hai,siku njema na endelea
kuifwatilia blogu hii ya www.mwakasegeinjili.blogspot.com
SIKUKUU
NJEMA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni