Jumanne, 15 Oktoba 2013

BIBLIA SIO NENO LA MUNGU!


BIBLIA SIO NENO LA MUNGU!

Naona umeshtuka he!!
Yah ni ukweli kwamba Biblia kama Biblia sio neno la Mungu.
Biblia ni maandiko matakatifu.
Wapo watu wanaoichukua biblia na kuiweka karibu na mto kwajili ya ulinzi ili mapepo yakija usiku yaogope ile biblia yasiwaguse. Huo ni uchanga wa kawaida tu.
Mapepo wala hawaogopi hicho kitabu. Ndio maana utakuta watu wa dini nyingine wanaichukua biblia na kwenda nayo kwenye nyumba zao za ibada na kuikufuru na kuikashifu na hata kuichana wakisema wanalichana neno la Mungu.

Kwahiyo Neno la Mungu ni nini basi?
Neno la Mungu ni hatua ya kuchukua sasa haya maandiko matakatifu yaitwayo biblia na kuchanganya na nguvu ya Roho mtakatifu yanapotoka sasa ndani ya mtu ndio hayatoki tena kama maandiko matakatifu linatoka sasa NENO la Mungu.
2 Timotheo 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

2 Wakorintho 3:6 Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.

Lazima lichukuliwe andiko, liingizwe ndani likutane na pumzi ya Mungu ambayo ni Roho mtakatifu ndipo sasa kizaliwe kitu kinachoitwa NENO LA MUNGU ambalo hilo sasa mwenye dhambi akilisikia machozi yanamtoka, moyo wake unaguswa, mioyo inachomwa, mioyo inasikia hukumu hilo sasa ujue ndio neno.

Usishike au kukumbatia bablia ukadhani umeshika neno la Mungu utakuwa umeshika maandiko tu matakatifu ambayo bila ile PUMZI hayawezi kukusaidia.
SIJUI KAMA UMANIPATA HAPO!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni