Jumamosi, 12 Oktoba 2013

KANISA LA SAA YA UFUFUO NA UZIMA YASIMIKA MCHUNGAJI WA ARUSHA

Mchungaji Gewajima akiwa na Mchungaji Frank Andrew kwenye viwanja vya kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha.


Taarifa ambazo zinarindima jijini Arusha muda huu ni kuhusu kusimikwa kwa Mchungaji wa kanisa la Utukufu wa Kristo nchini (Glory of Christ) ambalo ni maarufu kwa jina la Ufufuo na Uzima chini ya Mchungaji Josephat Gwajima, ni kuhusiana na kusimikwa kwa mchungaji wa kanisa hilo kwa Arusha.

Mchungaji Frank Andrew, wa kwanza kulia mstari wa mbele


Mchungaji Frank Andrew ndio kiongozi wa kanisa hilo kwa Arusha, ambapo amesimikwa kwenye kusanyiko la maelfu ya watu waliopo viwanja vya Engo Sheraton, ambapo atakuwa na jukumu la kulea wana-Arusha na kuwaleta kwa Kristo.

Kupitia ukurasa wa facebook wa kanisa hilo, taarifa zimewekwa muda mchache uliopita, wakielezea tukio hilo, na hatimaye sasa kutoa fursa pale mikutano itakapoendelea kwenye mikoa ya Kilimanjaro, Tanga na kwingineko.


Hata hivyo, GK iliona dalili za mchungaji Frank kuachiwa kanisa ili apate kuliendeleza jijini Arusha, kutokana na namna alivyokuwa akiwajibika ama kutakiwa kuwajibika kwenye mkutano unaoendelea.

Ujenzi wa ofisi ya kanisa la Ufufuo jijini Arusha ukishika kasi.
Maombi ya pamoja, Mchungaji Frank akiongoza.

www.mwakasegebibilia.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni