Jumapili, 20 Oktoba 2013

MAJESHI YA BWANA KAZINI, MOSHI KAENI CHONJO


Mkutano wa injili ambao umeandaliwa na kanisa la Utukufu wa Kristo (Glory of Christ) maarufu kwa jina la Ufufuo na Uzima, hatimaye utaendelea jijini Moshi baada ya miujiza kufanyika Arusha, ambapo maelfu kwa maelfu wameokoka na kufunguliwa kutoka vifungo vya kila aina.


Mkutano huo ambao umepelekea kuanzishwa kwa tawi la kanisa hilo Arusha eneo la Engo Sheraton, unatarajia kupelekea maajabu ya nguvu za Mungu kwenye kila mkoa watakapopita, na pindi wakimaliza Moshi tarehe 20 - 27 Oktoba, wataelekea Tanga, mahali ambapo kwa hakika inatarajiwa kuwa mapinduzi makubwa yatafanyika.


Zifuatazo ni baadhi ya picha ambazo Gospel Kitaa imezipiga katikati ya wiki kwenye viwanja vya kanisa hilo, shuhudia mwenyewe kilichojiri, ambapo watu hufundishwa kuhusu Neno la Mungu, na kidogo kidogo, utaona wameshaanza pia kuwa jeshi kamili - haoa jeshi liko kazini, linapiga kwelikweli.








Kuna style tofauti za kupokea pale Neno linapomgusa mtu, Mchungaji Bihagaze akiwa ameruka kimo, huku Mchungaji Kiongozi Gwajima akiendelea kuhubiri, na kushoto kwake Mchungaji wa Ufufuo Arusha, Frank Andrew nae akijipanga.




Ni kama vile wanacheza mpira wa kikapu, wenzio wako Rohoni hapo.


Picha zifuatazo zinaonesha majeshi yaliyofundishwa namna ya kupiga, wakiendelea na zoezi la kummaliza shetani ambaye amekuwa akiwasumbua kwenye mambo mablimbali bila wenyewe kujua kinachoendelea.




















































Baadhi ya wana Information na Media, hakuna utakachokosa.



Jacson Benty, Potential akitabasamia GK huku wenzake nyuma wakimtolea macho.



Kwenye mixer hakuna kitakachoharibika wataalamu waliokubuhu wapo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni