Jumapili, 6 Oktoba 2013

SHEREHE YA VIJANA ILIVYONOGA NDANI YA AZIMIO REVIVAL CHRISTIAN CENTRE ARUSHA

Miezi, wiki, na siku na hata masaa yalisubiriwa hadi kufikia siku ya vijana ambayo wameisheherekea leo kwenye kanisa la T.A.G Azimio Revival Christian Center jijini Arusha, ambapo kwa wiki hii yote, vijana wamekuwa wahudumu kwenye ibada zote.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za ibada ya Jumapili hii ambapo pamoja na kuhubiri, kuongoza sifa, uigizaji na kadha wa kadha, wamepata pia kutoa zawadi kwa wachungaji kanisani hapo, Kanisa linaloongozwa na Mchungaji Munisi.


Baada ya Ibada, vijana walirejea kwa ajiliya kusheherekea, kwa sasa Gospel Kitaa inakupatia picha za ibada ilivyokuwa, karibu.












Picha kuanzia ya kwanza mpaka hii ni vijana wakionyesha igizo linalohusu wavivu wa kushuhudia na wanaojituma katika kushuhudia.




Inaitwa kanyaga shetani hiyo.


Vijana wakimsifu Mungu.


Vijana wakibadilishana mawazo nje ya kanisa baada ya ibada.



Hakika ilipendeza kama wahusika walivyopendeza.www.mwakasegebibilia.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni