Alhamisi, 24 Oktoba 2013

UKOO WA MALKIA UINGEREZA WATAKIWA KUMLEA MTOTO AMJUE YESU, ANGALIA PICHA ZA UBATIZO


Askofu mkuu wa Canterbury kanisa Anglican duniani Justin Welby amewataka wazazi na wadhamini wa mtoto Prince George Alexander Louis kuhakikisha mtoto huyo anamjua Yesu ninani katika maisha yake. Askofu Welby ameyasema hayo wakati akimbatiza mtoto wa kwanza wa mjukuu wa malikia Elizabeth wa Uingereza, Prince William na mkewe Kate Middleton katika ibada fupi iliyohusisha familia pamoja na wageni wao 22 na kufanyika katika kanisa la kifalme ndani ya jengo la Mtakatifu James jijini London.

Wakati wa ibada hiyo baba mdogo wa mtoto huyo Prince Harry alisoma neno kutoka kitabu cha Yohana 15:1-5 ukizungumzia suala la mzabibu na matawi huku mama mdogo wa George, Pippa Middleton kwa upande wake alisoma neno kutoka kitabu cha Luka 18:15-17 ukizungumzia Yesu aliposema waacheni watoto wadogo waje kwangu. Katika ubatizo huo uliohudhuriwa na malkia pamoja na mumewe Prince Philip jumla ya wadhamini ama walezi wa mtoto wapatao saba walichaguliwa wakiwemo kutoka ukoo wa ufalme, marafiki wa karibu na Prince William pamoja na rafiki wa karibu sana na marehemu Princess Diana aitwaye Julia Samuel.

Askofu Welby alitumia maji ya mto Yordani katika kumbatiza prince George maji ambayo yamekuwepo katika kanisa hilo lenye historia ya ukoo wa kifalme toka mwaka 1894. Kwa mujibu wa Prince William amesema mwanae hajasumbua hata kidogo ikiwa ndio siku yake ya kwanza hadharani toka azaliwe, ambapo imeelezwa mtoto huyo kuonekana mwenye furaha na tabasamu toka awasili na kutoka kanisani hapo, huku muonekano wake ukiwa kama baba yake alivyokuwa katika umri kama huo.



Kate Middleton akiingia na mwanae.


Prince William akiwa mwenye furaha na mtoto wake Prince George mwenye miezi mitatu.


Wazazi wenye furaha na mtoto wao ambaye yupo katika mstari wa tatu katika urithi wa kiti cha ufalme Uingereza.


Prince William, mkewe, mtoto pamoja na askofu mkuu wa Anglican duniani Justin Welby.



Mwe gauni hilo reeefu, ni la kitamadauni katika ukoo wa kifalme, sio magauni haya mengine he he he. Gauni kama hili aliwahi kuvalishwa mtoto wa kike wa malkia Victoria wakati wa ubatizo wake.


Baba mdogo Prince Harry.


Malkia Elizabeth na mumewe Prince Philip, nyuma yao ni Prince Charles baba yake na William wakifika katika ubatizo huo.





Dada yake Kate aitwaye Pippa Middleton akiingia katika ubatizo.


Mama yake Kate akiingia katika ubatizo wa mjukuu wake.


Baba yake Kate naye alikuwepo.


Kama kawaida.


Shangazi wa Prince William ambaye ni mjukuu wa pili wa malikia Elizabeth, aitwaye Zara Philips akiingia kanisani hapo na mumewe.


Walikuwepo washangiliaji kama kawaida.


Kanisa ambalo limetumika kwa ubatizo, ndilo kanisa ambalo Malkia Victoria na mumewe Prince Albert walipofungia ndoa yao.


Waingereza wanapenda vya kwao ni utamaduni kama kawaida, wakimtakia kila la kheri mtoto George katika ubatizo wake.









Marehemu Princess Diana, mama mzazi wa Prince William akiwa na rafikiye kushoto Julia Samuel ambaye alichaguliwa na Prince William kuwa mdhamini wa mwanae.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni