Jumatatu, 21 Oktoba 2013

KWAYA ZA AIC SHINYANGA ZATIKISA UWANJA WA CCM KAMBARAGE MAADHIMISHO MIAKA 20 YA DAYOSISI YAO


Mercy Nyagwaswa kutoka AIC Dar es salaam Choir akishambulia jukwaa hapo jana.
Kwaya na waimbaji binafsi kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga wamependezesha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa dayosisi ya mkoa huo kwa kanisa la African Inland (AIC)Tanzania mwaka 1993, tamasha hilo lililoanza siku ya ijumaa lilihitimika hapo jana katika uwanja wa CCM Kambarage mkoni humo.

Jumla ya kwaya 13 zimeshiriki toka siku ya ijumaa, ikiwemo kwaya ya AIC Shinyanga wana wa kung'ang'ania, AIC Kambarage kwaya wana wa Piga kelele, mwanadada Mercy Nyagwaswa kutoka AIC Dar es salaam kwaya ambaye amealikwa kama mwimbaji binafsi, AIC Mwadui na kwaya nyinginezo.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuendelea wiki nzima hii kwa mkutano mkubwa wa injili utakaohubiriwa na maaskofu wa kanisa hilo nchini na nchi jirani ya Kenya pamoja na maaskofu kutoka jumuiya ya Kikristo nchini (CCT) wakiongozwa na mwenyekiti wake askofu mkuu wa Kanisa la Kilutheri nchini Dkt. Alex Gehaz Malasusa.

Ambapo kilele cha maadhimisho hayo kinatarajiwa kuwa siku ya jumapili, kwa kuanza kwa maandamano kuelekea uwanja wa Kambarage sambamba na shughuli ya uchangiaji wa pesa kwa ajili ya kuchangia shule ya dayosisi hiyo Bishop Nkola school yatakayoongozwa na waziri mkuu mstaafu ambaye pia ni mbunge wa Monduli mheshimiwa Edward Lowasa pamoja na mhamasishaji akiwa ni mchungaji matarajiwa bwana Masanja Mkandamizaji, huku kwaya maarufu ya AIC Chang'ombe Vijana (CVC) wanatarajiwa kunogesha zaidi maadhimisho hayo.



Askofu wa Dayosisi ya Pwani Askofu Salala pamoja na mwenyeji wake Askofu Dr Nkola wakiendelea kufuatilia hitimisho la tamasha la uimbaji.


Waimbaji mahiri wa AIC Shinyanga Choir wana wa kung'ang'ania wakisukuma sauti.


AIC Shinyinga Choir.




Mercy akifuatilia uimbaji uwanjani hapo.


AIC Kambarage Choir wakimsifu Mungu.


Kwaya ya akinamama AIC Kambarage wakimsifu Mungu.



Kwaya ya wanafunzi wa shule ya Bishop Nkola nao wakimsifu Mungu.


AIC Kambarage wakionekana kwa mbali wakimsifu Mungu siku ya ijumaa.


Mercy Nyagwaswa akimsifu Mungu akipewa kampani na wana wa Kung'ang'ania.


Baadhi ya mamia ya waumini na wakazi wa mkoani Shinyanga wakifutalia tamasha hilo viwanjani. Picha kwahisani ya AIC Dayosisi ya shinyanga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni