Jumatano, 23 Oktoba 2013

JOYOUS YATANGAZA TAREHE YA KUREKODI DVD MPYA, MASHABIKI WALUMBANA


Mwanadada Sphumelele Mbambo au mwite Ntokozo kwa jina lingine, akiwajibika jukwaani.
Hatimaye kundi mahiri la gospel barani Afrika la Joyous Celebration limetangaza rasmi tarehe na ukumbi ambao wanatarajia kurekodi album yao mpya ya 18 mwishoni mwa mwaka huu. Kupitia ukurasa wao wa Facebook kundi hilo limesema litarekodi album yao tarehe 21 December katika ukumbi wa ICC Durban na kuahidi kutoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo.

Hata hivyo tofauti na ilivyotarajiwa na mashabiki wa kundi hilo kutoka Cape town nchini humo ambao walidhani kutokana na shoo mbaya iliyofanywa na kundi hilo mapema mwezi wa nane mwaka huu basi wangekwenda kufuta makosa hayo kwakwenda kufanya rekodi yao jijini humo. Tangu kuwekwa kwa ujumbe huo hapo jana majira ya mchana kumekuwepo jumbe mbalimbali kutoka kwa wapenzi wa kundi hilo wanaoishi Cape town wakilalamikia uamuzi huo, huku wenzao wa Durban wakifurahi na wengine wakitoa pole kwa wenzao hao na kuwataka kukumbuka kwamba Joyous makao makuu yake ni Durban.

Kundi la Joyous Celebration kwasasa linatambulika zaidi nchini Afrika ya kusini kuliko ilivyokuwa kwa siku za nyuma hali inayofanya mashabiki wao kufunga safari ya masaa zaidi ya nane kulifuata kundi hilo sehemu ambayo itakuwa ikifanya onyesho, katika hilo wapenzi wa Durban wameonekana kutopitwa na ziara za kundi hilo kila mwaka, ambapo kwa uchunguzi uliofanyika inadaiwa kwamba kundi hilo lina mashabiki wengi sana katika mji huo pia waimbaji wengi wapya na wazamani wanatokea mji huo lakini kubwa kuliko hata viongozi na sehemu kundi hilo lilipoanzia ni mji wa Durban.

Kati ya jumbe za mashabiki wa Joyous kutoka CapeTown wakilalamikia uamuzi wa kundi hilo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni