Jumanne, 15 Oktoba 2013

Mch. Gwajima asema Mkutano wa Moshi utakuwa wa maajabu makubwa sana

Mchungaji Josephat Gwajima ambaye ni Mchungaji kiongozi wa kanisa la Glory Of Christ Tanzania Church maarufu kama Nyumba ya Ufufuo na Uzima lenye makao yake makuu Kawe, jijini Dar es Salaam; amefanya mahojiano na Mtangazaji wa Radio Sauti ya Injili iliyopo mjini Moshi asubuhi ya leo. Mahojiano hayo ambayo yalidumu kwa muda wa saa nzima yalilenga kuelezea juu ya umuhimu wa neno la Mungu kwa kanisa la leo na pia kujua undani wa mkutano wa Injili unaotarajiwa kuanza jumapili hii mjini Moshi.



Mahojiano ya Mch. Josephat Gwajima na Deo Mosha wa Radio Sauti ya Injili - Moshi.
Mtangaziji huyo aitwaye Deo Mosha aliandaa mada ambayo kwayo ilimpatia wasaa mzuri kwa Mchungaji Josephat Gwajima kuelezea kwa undani juu ya umuhimu wa neno la Mungu kwa wakristo. Akieleza kwa undani juu ya umuhimu wa neno la Mungu, Mch. Gwajima alieleza historia fupi ya Ukristo kuanzia kipindi cha Martin Luther hadi kipindi hiki cha kunena kwa lugha. Alisema, injili ilitoka ulaya na kuja Afrika lakini katika kipindi hiki cha mwisho waafrika ndio watakao kuwa risasi ya mwisho ya injili kutoka katika bunduki ya Mungu.





Akieleza changamoto alizokutana nazo katika mkutano wa Injili wa Arusha, Mch. Gwajima alijibu kuwa changamoto zipo ukiwemo ukweli kuwa kuna gharama kubwa kwasababu mkutano ni mjumuiko wa mambo mengi sana. Akitolea mfano wa Mkutano wa Arusha, alisema, "tumesafirisha vyombo na mabasi ya wachungaji zaidi ya mia mbili wanaohudimia watu, kwa maana hiyo hizo gharama zote ni changamoto kwetu" Pia alisema, "kanisa hili linajitegemea kwenye mikutano hivyo ni changamoto kubwa kwetu."


Akiongelea Mkutano wa Moshi unaotarajiwa kuanza tarehe 20 hadi 27 Oktoba, alisema kuwa mkutano huo utakuwa wa maajabu na miujiza ya kupita kawaida, na akawaasa watu wa Moshi kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia waliokuwa msukuleni kurudishwa na waliokufa kurudi kwenye uhai wao tena.



Mchungaji Josephat Gwajima akifanya mahojiano na mtangazaji Deo Mosha.
alipoulizwa kwa habari za Misukule na kufufua watu waliokufa; Mch Gwajima alisema kuwa kazi hii si ya mtu mmoja bali ni kazi ya Bwana Yesu ambayo Mtu yeyote wa Mungu atakayeamua kufufua na kurudisha Mungu atamtumia kwa nguvu. Akitoa andiko la Mathayo 10:8 alisema kuwa biblia iko wazi sana kwa habari ya kufufua watu waliokufa; na kusema kuwa tatizo la waafrika wengi ni vile wanashindwa kuthamini kitu kikubwa ambacho Mungu anakianzisha kwa.


Mwisho, alitoa wito kwa wachungaji vijana kwa kusema kuwa "yatupasa kuifanya kazi ya BWANA kungali bado asubuhi maana saa inakuja ambayo hatoweza mtu kuifanya" kwa maneno hayo aliwaasa vijana kuifanya kazi ya Mungu wangali vijana kwasababu mtu akianza kazi ujanani anapata muda mzuri wa ku sahihisha makosa yake lakini akianza uzeeni atakosa muda wa kusahihisha makosa na hivyo kushindwa kufanya vizuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni