Jumatatu, 21 Oktoba 2013

MOYO WA NCHI ,UFAHAMU MOYO WA ULIMWENGU WA ROHO



Mchungaji(Resident Pastor) Adriano akifundisha mapema leo ibadani
Na Mch. Adriano Makazi

Yona 2:1-10
Ninawi ulikua ni mji ambao watu wake walikua wamemuacha Bwana, na Mungu alikua amemtuma Yona ninawi na alimpa ujumbe kwaajili ya watu wa Ninawi, lakini Yona akaghairi na kwenda Tarshishi ambako Bwana hakumtuma.

Na alipokua akielekea ambako hajatumwa na Bwana ikatokea dhoruba, kura ilipopigwa ikaangukia kwa Yona, walipomhoji wamtendee nini Yona akasema wamtupe baharini. Alipotupwa baharini Bwana akaandaa samaki ili ammeze.

Nivizuri kujua samaki huyu hakua samaki wa kawaida, kwasababu angekua samaki wa kawaida Yona asingekaa ndani ya tumbo la samaki kwa siku tatu.


Baada ya siku tatu Bwana akasema na samaki na samaki yule akamtapika pwani ya Ninawi ili kwenda kuifanya kazi aliyokuwa akiikimbia.

Mathayo 12:40 Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la nyangumi kwa muda wa siku tatu mchana na usiku, vivyo hivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika moyo wa nchi siku tatu, mchana na usiku

Yesu alikua anajaribu kuwaelezea mafarisayo kua kizazi hiki kinahitaji ishara ya ufufuo, alikua anawaelezea namna yeye atakavyoshuka katika kuzimu na kufufuka siku ya tatu
Ninakutia moyo leo kama vile Yesu alivyoshuka katika kuzimu na siku ya tatu kufufuka ndivyo hivyo leo Yesu ashuke katika ile shida yako na kuleta ufumbuzi kwa jina la yesu.

1 Petro 3:18-19 “Kwa kuwa Kristo naye aliteswa mara moja tu, mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili awalete ninyi kwa Mungu. Mwili wake ukauawa, lakini akafanywa hai katika Roho, ambayo kwa hiyo alikwenda na kuzihubiria roho zilizokuwa kifungoni

Ufunuo 1:17 Nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama aliyekufa. Ndipo akaweka mkono wake wa kuume juu yangu na kusema, “Usiogope, Mimi ni wa Kwanza na wa Mwisho Mimi ni Yeye aliye hai, niliyekuwa nimekufa na tazama, ni hai milele na milele! Nami ninazo funguo za mauti na kuzimu

Ni vizuri kufahamu kua Yesu hakuuawa na mtu yeyote bali aliutoa uhai wake ili aupokee tena na aliposhuka chini aliwafungua wale waliokua kifungoni na anazo funguo za mauti na kuzimu.

Moyo wa nchi ni kuzimu na Yesu aliposema anazo funguo za mauti na kuzimu alikua anamaanisha anaweza kuwafungua wote walioshikiliwa na mauti na kuzimu

KWANINI YESU ALIIFANANISHA KUZIMU NA MOYO??

Ezekiel 27:4 Mipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari, wajenzi wako walikamilisha uzuri wako

Ezekiel 27:27 Utajiri wako, bidhaa zako na mali zako, mabaharia wako, manahodha wako, mafundi wako wa meli, wafanyabiashara wako na askari wako wote na kila mmoja aliyeko melini atazama kwenye moyo wa bahari siku ile ya kuvunjika kwa meli yako,

Biblia hapa inaonyesha kuna watu wanazo bidhaa ambazo zimeunganishwa na moyo wa bahari, hii inaonyesha kuna bidhaa, mali au utajiri ambao asili yake ni kuzimu

NINI KAZI YA MOYO?

Kazi ya moyo katika mwili wa mwanadamu ni kusukuma damu katika sehemu mbali mbali za mwili, na moyo unapoanza kupata matatizo mtu anakua anapata matatizo na kupelekea magonjwa mbali mbali na mwili kuishiwa nguvu.

Kama ambavyo kazi ya moyo ni kuachilia damu mwilini na oksijeni ndivyo na kuzimu kazi yake ni kuachilia uovu kuja duniani, kuzimu inakazi ya kusukuma uovu kutoka chini na kuja duniani na ndio maana ikaitwa moyo wa Nchi.



Mchungaji (Resident Pastor) Adriano akiwaongoza sala ya toba mamia ya watu leo ibadani
Ufunuo 13:11 Kisha nikamwona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika dunia. Alikuwa na pembe mbili kama mwana-kondoo, lakini akanena kama joka.

Hapa utaona mnyama akipanda kutoka kuzimu kuja kusababisha uharibifu duniani, mnyama alionekana kama mwanakondoo lakini aliponena tu ikagundulika ni joka.
Kuna wakati tunapata matatizo ya namna mbali mbali lakini ni kwasababu moyo wa nchi (kuzimu) imeyaachilia duniani kwaajili ya kuleta uharibifu katika maisha ya watu

Vitu vinavyopanda kuzimu kuja duniani vinaweza kuingia ndani ya mtu, wanakua ni viumbe wa kishetani wenye uwezo wa kusababisha uharibifu katika maisha ya mtu, viumbe hawa wanaweza wakatumwa na mtu na kusababisha magonjwa mbali mbali na udhaifu/magonjwa kwa wanadamu.

Baada ya Yona kumuomba Mungu katika tumbo la yule samaki,Bwana akazungumza na samaki na samaki akamtapika Yona.

Wapo watu wengi ambao walimkosea bwana na walipomlilia Bwana akawaokoa na kuwaponya na kila uovu.

Zaburi 107:13-20 “ Ndipo walipomlilia BWANA katika shida yao, naye akawaokoa kutoka kwenye taabu yao….”
Ukiona uko kwenye shida unatakiwa kumlilia Bwana naye atakuokoa.
Nini maana ya kufunikwa na uvuli wa mauti??
Ukifunikwa na uvuli wa mauti inamaanisha kila ulichonacho kinakufa,kama ni biashara inaharibika, kama ni kazi unafukuzwa mambo yote unaoyategemea na yaliyokuzunguka yanakufa, hii ndio maana ya kufunikwa na uvuli wa mauti

Shetani anaweza akautoa moyo wa mtu na kumbadilishia moyo mwingine au akaushikilia moyo wa mtu.

Namna moyo wa mtu ulivyo ndivyo huyo mtu ataonekana kwa namna ya nje, shetani anaweza kuwawekea watu moyo wa ukatili na wa mnyama na kumfanya mtu kuwa wa namna ya ajabu. Moyo ni kama kitabu ambacho Mungu anakua ameweka maelekezo kwenye maisha ya mtu.

1 Samwel 1:14-18 Hana akajibu, “Si hivyo bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye huzuni kubwa. Mimi sijanywa mvinyo wala kileo, nilikuwa ninaumimina moyo wangu kwa BWANA
Namna moyo wa mtu ulivyo ndivyo mtu huyo anaonekana. Hana alikua na huzuni moyoni na huzuni yake ikaonekana mpaka nje.
Mithali 15:13 Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke, bali maumivu ya moyoni huponda roho


Moyo wa mtu unaweza ukaibiwa na kuwekewa moyo mwingne
Nebukadneza alibadilishwa moyo wake na kupewa moyo wa mnyama

Daniel 4:16 "Moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu na apewe moyo wa mnyama, nyakati saba zikapite juu yake."

Kuna watu wamebadilishiwa mioyo yao na kuwa na moyo kama wa mnyama, watu wa namna hii wanakua na matatizo mbali mbali na mambo yasiyo ya kibinadamu, wanakua na hasira na hawataki suruhu, tunaona hapa Nebukadneza alibadilishwa moyo na maandiko yanasema akaanza kula majani akaota na manyoya porini, hivyo tunajifunza ukibadilishwa moyo huwezi tenda kusudi lile Bwana alilokupangia kufika hatma yako.

Marko 7:21 "Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka: Mawazo mabaya, uasherati, wizi,uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu,matukano, kiburi na upumbavu. Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi."

Mtu anapokua na moyo ambao ni wa bandia, moyo huo unakua na kawaida ya kutoa vitu ambavyo mtu hapendi, unakuta mtu anafanya mambo mabaya ambayo mtu mwenyewe hayapendi

Mathayo 15:19 "Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi,ushahidi wa uongo na masingizio"

Luka 6:45 "Vivyo hivyo mtu mwema hutoa mambo mema kutoka kwenye hazina ya moyo wake, naye mtu mwovu hutoa mambo mabaya kutoka kwenye hazina ya moyo wake. Kwa kuwa mtu hunena kwa kinywa chake yale yaliyoujaza moyo wake"

Shetani anajua akiushikilia moyo wa mtu anaweza akamtawala mtu huyo na kumpeleka kokote anakotaka kwenda, hii ndio sababu unamkuta mtu ameokoka lakini kinywa chake hakiachi kutoa matusi. Mtu wa namna hiyo anakua anatamani kuacha lakini anashindwa kwasababu moyo unakua umeshikiliwa na shetani na maamuzi yote yanafanywa na shetani.

Kuna watu wengine wana mioyo ya jiwe, katika jiwe huwezi kuweka chochote kikaota, watu hawa wanakua hawazai matunda

Matendo 13:8 Lakini Elima yule mchawi (maana ndio tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akimtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.
Shetani na wachawi wanaweza wakamtia mtu moyo wa kuacha kitu kizuri unachokifanya, unamkuta mtu anafanya kazi nzuri lakini anaamua kuiacha bila sababu maalumu na baada ya muda anakua na maisha mabaya sana, hii ni kwasababu mtu anakua ametiwa moyo wa kuacha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni