Jumamosi, 12 Oktoba 2013

YEYOTE ANAYEHITAJI KUTUBU NA KUANZA UPYA NA BWANA YESU AOMBE MAOMBI HAYA KISHA AFUATE MAELEKEZO HAPO CHINI.

‘’BWANA YESU, niko mbele zako mimi ni mwenye dhambi, lakini leo naamua kukufwata wewe BWANA YESU, Natubu dhambi zangu zote, ninazokumbuka na nisizozikumbuka, Futa jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike jina langu kwenye kitabu cha uzima, tangu leo nimeokoka, naufunga ukurasa wa dhambi na kuanzia sasa ninafungua ukurasa wa kumcha MUNGU nikiwa ndani yako BWANA YESU. 

Nipe ROHO MTAKATIFU ili aniongoze kuanzia sasa. Asante BWANA YESU kwa kuniokoka, niongoze BWANA na niwe mbali na kuonewa kuanzia sasa, navunja maagano yote ya shetani niliyoingia, najitenga na laana za za ukoo na roho za mizimu katika jina la YESU KRISTO, nishindie vyote BWANA. Katika jina lako takatifu BWANA YESU nimeomba, nimeamini na nimepokea. AMEN’’

Baada ya maombi haya Tafuta kanisa la kiroho wanapohubiri kweli ya MUNGU na wanakiri WOKOVU tena wanaikemea dhambi hadharani, waeleze na watakuombea na kukuongoza kisha utaukulia Wokovu wa BWANA YESU pamoja na washirika wengine.
MUNGU akubariki sana  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni