Jumatatu, 21 Oktoba 2013

GLORIOUS YABARIKI WATU MWANZA, WAMTEMBELEA MJANE WA ASKOFU KULOLA


Baadhi ya waimbaji wa GWT wakiwa mbele ya kaburi la marehemu Askofu Dkt. Moses Kulola, E.A.G.T Bugando jijini Mwanza.
Kundi la Glorious Worship Team(GWT) lenye makao makuu yake jijini Dar es salaam limeendelea na ziara yao ya kihuduma jijini Mwanza wakiambatana na mlezi wao bwana Eric Shigongo mkurugenzi wa Global Publisher, ambapo hapo jana waliweza kuwabariki watu waliofika katika ibada ya kusifu na kuabuduiliyofanyika ukumbi wa JB Belmont hotel kwa jinsi walivyoweza kushusha uwepo wa Mungu katika sifa na kuabudu.

Pamoja na huduma waliyoiendea kundi hilo, pia siku ya jumamosi waliweza kumtembelea mjane wa marehemu askofu Dkt Moses Kulola nyumbani kwake, ambako waliweza kuimba baadhi ya nyimbo zao. Moja kati ya vitu vilivyovutia zaidi kundi hilo ni kurudi kwa mwimbaji wao aitwaye David Silomba ambaye awali alikuwa katika kundi la Glorious Celebration ikiwa ni mara ya pili kama GK haijakosea kwa mwimbaji kujiunga na GWT awali alikuwa ni mmoja kati ya waanzilishi wa GWT lakini aliamua kurudi G.C na sasa amerejea tena GWT.



Baadhi ya waimbaji wa kiume wa GWT wakiwa na mjane wa askofu Kulola nyumbani kwake.


Joel Lwaga kushoto na David Silomba waimbaji waliongeza nguvu GWT. Picha kwahisani ya meneja wa GWT, Emanuel Mabisa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni