Jumapili, 6 Oktoba 2013

DAMU YA YESU YAENDELEA KUKOMBOA WALICHUKULIWA MSUKULE ARUSHA.


Mchungaji Gwajima akiwa na baadhi ya watu waliofunguliwa kutoka vifungoni na misukuleni siku ya Jumamosi.
Kwa Jina la Yesu njoo, msemo huu umekuwa wa kawaida jijini Arusha, lakini wenye nguvu, kwani waliochukuliwa misukule, waliokuwa vifungoni na kwenye mateso ya hali ya juu kutokana na mwovu shetani, hatimaye wameendelea kufunguliwa, na hapo jana (Jumamosi) zaidi ya waty kumi walirudishwa kutoka walikokuwa, Tunduma, Handeni, Moshi, Tengeru na Mswakini (Arusha), na maeneo mbalimbali.

Mwanamke ambaye kizazi chake kilikuwa kimenin'ginizwa kwenye mti ili asizae.

Umati uliofurika viwanja vya reli umedhihirisha kuwa hakuna kisichowezekana kwake Yesu, kwani kwani wameshuhudia maajabu kwa macho ya damu na nyama. Na hata pale mkutano unapoisha, tayari roho ya kuomba imeshawajaa watoto, kwani popote wanapokuta watendakazi wakiendelea na maombi, basi hujaribu kwa namna yoyote ile kujumuika nao na kuanza kuita NJOO kwa Jina la Yesu. Hakika Arusha imebadilika, inaponywa hasa.
Jumapili (leo) ndio itakuwa hitimisho la mkutano huo mkubwa uliobadili maisha ya wengi kiroho na kimwili, na kwa taarifa ambazo sio rasmi, kuna uwezekano mkubwa kiwanja kilichokuwa kinahitajika kimepatikana, na hivyo leo mkutano utafahamishwa iwapo majeshi yanaendelea na jiji hili ama ratiba itakavyokuwa, kwani kiu ya wana-Arusha kulishwa zaidi bado ipo, na hiyo ilidhihirika pale ambapo waliulizwa, sauti za kukubali zilizikika kama maji vile, Utukufu ni wa Yesu.

Sehemu ya waliofunguliwa.





Sehemu ya umati waliokaribia jukwaa kwa ajili ya maombezi. ©GK/Ufufuo/Frank



Upande mwingine wa umati ulivyokuwa. www.mwakasegebibilia.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni