Jumanne, 15 Oktoba 2013

Kiingilio kwenye Semina!!


Shalom naamini mnaendelea vyema kwa neema ya Mungu, popote mlipo watumishi wa Mungu naomba mnisaidie kunielimisha juu jambo hili, mara nyingi nasikia watumishi wa Mungu wanasema Mungu amewapa ufunuo fulani ili wawasaidie watu wanaoteseka ktk jambo fulani na wanaandaa semina na kualika watu ili waende wakajifunze, na hapo wanatangaza kuwa kutakuwepo na KIINGILIO kwenye semina hiyo je ni halali watu kulipa pesa kwa ajili ya kujifunza Neno la Mungu? na unakuta semina hiyo imeandaliwa kwenye kanisa fulani, je ina maana wasio na na pesa hawaruhusiwi kwenda kujifunza?
Mara nyingi nimeona watu wanazuiliwa kwenye milango kisa hawana hela, kama ni kufidia gharama kwenye semina kunakuwepo na sadaka mbalimbali ambazo zinaweza kufidia gharama, za maandalizi. tumepewa bure ni kwa nini tuwauzie watu ujumbe au maono uliyopewa na Mungu?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni