Alhamisi, 10 Oktoba 2013

JUA KISA CHA AMBWENE KUIPA JINA LA "MISULI YA IMANI" ALBUM YAKE

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


KWA TAARIFA YAKO hii leo tunaye mwanakaka Ambwene Mwasongwe ambaye ana album tatu za muziki wa injili mpaka sasa ambapo ya tatu ndiyo mpya iitwayo "Misuli ya Imani" Je? unajua kwanini muimbaji huyu aliamua kuipa album yake jina hilo? KWA TAARIFA YAKO kupitia maswali ambayo amewahi kuulizwa na wasomaji wa blog hii ya GK Ambwene amesema aliamua kuipa album yake jina hilo kutokana na kisa ama ushuhuda ambao ameuimba katika wimbo huo wa mama aliyekuwa na watoto saba na wote wakafa siku moja

Kutokana na ushuhuda huo ndipo mwimbaji huyu akagundua kwamba kuna watu ambao mara nyingi Mungu huwaamini katika dunia ya leo kama ilivyokuwa wakati wa Ayubu ambaye mateso yake yanajulikana kwa kila msomaji wa Biblia hayatofautiani sana na mama huyo aliyefiwa na watoto wake saba kwa siku moja hali ambayo Ambwene amesema watu hao wana "Misuli ya Imani" kwamba wanaweza kuhimili shida na matatizo yanayowapata.



Kama haitoshi KWA TAARIFA YAKO Ambwene amesema kwahiyo kwakuimba kwake wimbo huo ilikuwa ni kuwaeleza watu jinsi Imani inavyotenda kazi nanamna watu wanavyotakiwa kumuamini Mungu katika shida na raha wanazozipitia, aidha mwimbaji huyo amesema nyimbo alizoimba katika album hiyo na zilizopita shuhuda zote ni zakweli ambazo zimewatokea watu na pia nyingine ni shuhuda zake binafsi kwahiyo si vitu vya kutunga. KWA TAARIFA YAKO mwimbaji huyu ni mwanafunzi bado yupo jijini Mbeya chuo cha uhasibu na kwamba mpaka sasa anavideo moja ya album yake ya kwanza na kwamba video za album yake ya pili na mpya anatarajia kuzitoa hivi karibuni mambo yakikaa sawa pia anampango wa kusambaza mwenyewe kazi zake.

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kama ulikuwa hujui vinginevyo tukutane wiki ijayoooo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni