Jumatano, 2 Oktoba 2013

USIJIKATISHE TAMAA SIMAMA NA UANZE UPYA


Nikikaa na kutafakari majina kadhaa katika tasnia mbalimbali, basi Napata jibu kwamba kukata tamaa mara unaposhindwa jambo yaweza kuwa ujinga. Ni ujinga kwasababu hatujui ni kitu gani kipo mbele yetu iwapo tutasimama kidete na kuendelea kujaribu kupenya kwenye magumu yaliyotokea.

Kwa wapenzi wa filamu, wengi watakuwa wanaifahamu na hata kuishabikia Harry Porter, na kuna rafiki yangu mmoja ni amekubuhu, maana anaweza kukuhadithia Harry Porter zote mwanzo hadi mwisho, na akatumia dakika zilezile

Kimsingi nataka nikuambie tu kuwa mwandishi wa mfululizo wa vitabu hivyo, mwanamama J.K Rowling, alikwama mara 12 kwenye kuchapisha kitabu chake kimojawapo kabla hajatoka, na kasha baadae kampuni moja ndogo ya uchapaji jijini London ikakubali kuchapa kitabu cha kwanza, Harry Potter and the Philosopher’s Stone.

Katika mihangaiko yake, hakurudi nyuma, aliendelea kusonga mbele na hivi leo, ni mwanamama tajiri sana kupitia uandishi wake wa vitabu ambao hakuukatia tama, aliangushwa mara 12, lakini leo anagombaniwa, kiasi cha kufikia kuchapa kitabu kwa jina linguine ilia one watu watampokeaje, lakini waaapi. Amestukiwa na watu wanaendelea kumiminika kununua kitabu chake kipya.


"No matter how hard you work for success, if your thought is saturated with the fear of failure, it will kill your efforts, neutralize your endeavors and make success impossible."
~ Baudjuin



Huu ni msemo wa mwanazuoni mmoja ambaye kimsingi anasema kuwa hata ukifanya kazi kwa bidii namna gani, kama mawazo yako yamekaa ama yanawaza kuhusu kufeli hiyo kazi, basi hautofanikiwa katu maana juhudi zako zitakwamishwa na munachowaza, labda ujirekebishe kwanza.


Hapa cha umuhimu ni kwamba, ukipata jambo la kufanya, na ulikazanie. Rejea Mhubiri 9:10 “Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako;…”


Ukiamua kukaa na kulialia kuhusu jambo la kufanya eti kwa kuwa umejaribu mara mbili au tatu bila mafanikio, basi ujue umeamua kufeli mwenyewe. Hata Jemadari Naamani pamoja na kusita, aliamua kujichovya mtoni mara 7 na hatimaye akapata uponyaji. Rejea 2 Wafalme 5:14. Wewe umejaribu mara ngapi hadi ukaona kuwa huwezi kufanikiwa maishani? Simama ujaribu tena na tena na tena, na tena, na tena na tena - hadi kieleweke.


Basin a sasa tumgeukie Abraham Lincoln, unaweza ukawa umelisikia jina, maana ni Rais wa 16 wa taifa la Marekani, alipokuwa bwana mdogo, alikwenda jeshini akiwa n ache kikubwa cha ‘captain’ lakini akarudi akiwa na cheo kidogo, ‘private’.


Alishindwa kwenye biashara, uanasheria nao ukawa ni tabu tupu, kwani hakufanikiwa. Akageukia siasa, na hapo akashindwa alipogeombea mara ya kwanza kwa ajili ya ubunge, na tena akashindwa alipogombea mara ya kwanza congress, akashindwa alipogombea kuwa kamishna wa ofisi kuu ya ardhi, akashindwa kwenye kinyanganyiro cha kugombea useneta 1854, na pia akashindwa kwenye harakati za kugombea umakamu wa rais mwaka 1856, na tena kwenye uchaguzi wa useneta 1858 akashindwa tena.


Lakini kama angekata tama na kuamua kuketi akilaumu maisha yasivyo na usawa, basi asingeweza kuwa rais mwaka 1861 – 1865. Kwa kufeli huku wewe huwa unafanyeje? Unaketi na kujisongesha mawazo ama unaendelea kujaribu?


Haya na sasa tugeukie nuru unayoiona chumbani mwako, kupitia taa yako. Thomas Edison ndiye mgunduzi wa bulb, lakini kipindi chake akiwa darasani, mwalimu wake aliwahi kusema kuwa Thomas ni mjiga sana kuweza kujifunza kitu chochote. Na kwamba alifukuzwa kwenye ajira mbili tofauti kwa kutokuwa makini kazini.


Akiwa kama mgunduzi, Thomas alijaribu mara 1000 ili afanikiwe kuwasha taa yake bila mafanikio. Na mwandishi mmoja w ahabari aliwahi kumuuliza, “Ulijisikiaje kufeli mara 1000”, ambapo jibu alilopewa ilikuwa ni “Sikufeli mara 1000, ila balbu imepitia hatua 1000 hadi kuundwa.”


Kwa wiki hii nikuachie hapa, ila nikugusie tu kwamba hata yule mtaalamu wa Fizikia, Albert Einstein, hakuweza kuongea hadi alipofikisha umri wa miaka 4, na pia hakuweza kusoma hadi alipofikisha umri wa miaka 7. Wazazi wake walidhani kwamba hayuko sawa, na mmojawapo wa walimu wake alimuita kwamba ana ana ubongo wake unatafakari mambo polepole na mambo kadha wa kadha ilimradi tu.


Taabu kwa Einstein haikuishia hapo tu, kwani alikataliwa kujinga na chuo cha ufundi Zurich. Lakini baadae alijifunza kusoma na kuandika, na pia hesabu kadhaa


Ni jambo gani ambalo limekusitisha kuendelea kufanya mambo uliyokuwa unafanya hapo awali? Ni nani alikusemea maneno maovu hata ukaamua kutoendelea na mkakati wa kuboresha maisha yako na ya jamii inayokuzunguka?
"Our greatest glory is not in never falling but in rising every time we fall." Confucius.
"Great success is built on failure, frustration, even catastrophy." Summer Redstone

Chukua hatua, ukijikwaa ni sharti uendelee kutembea, ukianguka ni sharti usimame na ujipanguse vumbi na kisha usonge mbele. Kwa vyovyote vile, bidii yako itakufikisha mahala ulipoahidiwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni