Jumanne, 8 Oktoba 2013

UIMBAJI WA CHRISTINA SHUSHO WASABABISHA ATAMBULISHWE KUWA NI MKONGO


Nilipomkabidhi Christina Shusho tuzo yake ya AGMA niliyomchukulia jijini London, ndani ya studio za Clouds TV kupitia kipindi cha Chomoza.

Mwimbaji nyota wa muziki wa injili nchini mwanamama Christina Shusho ametambulishwa kama mwimbaji kutoka nchini Kongo kwa mujibu wa mtu anayemiliki akaunti katika mtandao wa YouTube aliyejitambulisha kwajina la Rehema East African gospel ambaye licha ya kukosolewa na watazamaji wa video za Shusho katika ukurasa huo bado mtu huyo amekuwa akiwakosoa watazamaji hao kwamba mwimbaji huyo ni kutoka Kongo.


Moja ya vitu ambavyo vinajidhihirisha kwamba mtu huyo habahatishi katika kuwakosoa watu ni pale ambapo ameamua kuweka jina la mkongo kwenye mabano akimaanisha Shusho katika kila video ya mwimbaji huyo iliyo katika akaunti yake, ambapo amekuwa akijibu watu kwamba Shusho ni mwimbaji kutoka Kongo ila ameolewa na mtanzania.


Unaweza kujisomea hapo chini kama GK ilivyoweza kukopi kutoka kwenye akaunti ya mtu huyo kuhusiana na Christina Shusho.www.hakileo.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni