WATU ZAIDI YA SABA AMBAO WALIKUWA NI WALEMAVU KABISA WA MIGUU, HATIMAYE WAWEZA KUTEMBEA BAADA YA KUOMBEWA NA MCH.KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA KATIKA MKUTANO MKUBWA WA INJILI UNAOENDELEA MJINI MOSHI, MATUKIO HAYA NI YA SIKU YA JUMATANO TAREHE 23.10.2013
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kutoka Kawe Jijini Dar es Salaam akiwaombea maelfu ya waamini katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi, maelfu ya wakazi wa mjini Moshi walikusanyika kwa ajili ya kusikiliza Neno la Mungu,Kuombewa na kuwekwa huru kutoka katika vifungo vya shetani.
Mchungaji kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima wa kwanza kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na walioponywa ulemavu wa miguu na kushoto kwake ni Petronila anafuatiwa na Mama Ruckless na wa mwisho kulia ni Mama Martha.
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima (wa pili kutoka kushoto), akiwa na Mchungaji mwandamizi (wa kwanza kushoto) Mchungaji Mwangasa, wakiwa na baadhi ya wananchi wa Mjini Moshi ambao wameweza kufunguliwa kutoka katika kifungo cha ulemavu wa muda mrefu katika Mkutano wa mkubwa wa Injili unaoendelea katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi, Pichani wakiwa na nyuso za furaha , wakiwa wamenyanyua magongo , wakimshukuru Mungu kwa kuwafungua kutoka katika kifungo cha shetani.
Mama Sarapia ambaye ni mkazi wa Moshi aliyekuwa mlemavu kwa kipindi kirefu hatimaye aweza kutembea na awa huru baada ya kuombwa na Mchungaji Kiongozi wa Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima.
Kwenye picha ni kijana aliyefahamika kwa jina la GEOFREY,(mwenye T-shirt nyeupe) ana umri wa miaka 33, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu huku akiwa ana uvimbe mgongoni. Alionekana mwenye furaha na tumaini jipya mara baada ya kupokea uponyaji wake baada ya kufika na kuombewa katika mkutano unaoendelea katika viwanja vya mashujaa mjini moshi.
Mchungaji Mwandamizi Maximillian Machumu, akiwa anamuongoza Kijana Godfrey ambaye ni mkazi wa Moshi aliyefika katika viwanja vya mashujaa na kupokea uponyaji kutoka kwa Bwana Yesu kupitia kwa Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima akiwa na Martha,
katika picha, amabye ana umri wa miaka36, alikuwa akisumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba na kuumwa kiuno kwa muda mrefu sana, jambo lililosababishwa na ajali ya pikipiki. alikuwa akielezea huku akibubujikwa na machozi ya furaha mara baada ya kupokea uponyaji wake. Alishuhudia mbele ya madhabahu kuwa ameteseka na tatizo hili kwa muda mrefu sana na amekuwa ana kwenda hospitalini mara kwa mara bila mafanikio yoyote. Sifa apewe Yesu aliye mponyaji wa Kweli.
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima akiwa ameshikilia magongo ya kijana mkazi wa Moshi aitwaye Gervas ambayo hayahitaji tena baada ya Bwana Yesu kumfungua kutoka katika kifungo cha ulemavu wa shetani.
GERVAS, ana umri wa miaka 23, alipooza miguu kwa muda wa miaka 3. Kijana Gervas alionekana akiwa na mshangao alivyoweza kutembea na kuamua kumpa Yesu maisha yake baada ya kammponya na magonjwa yake pamoja na madhaifu.
Wachungaji Waandamizi, Mchungaji Mwangasa kulia na Mchungaji Machumu kushoto wakiwa wanampokea Mama Petronila baada ya kuokolewa na Bwana Yesu kutoka katika kifungo cha Ulemavu katika maombezi aliyoyafanya Mchungaji Kiongzi wa kanisa la Ufufuo na Uzima Mchungaj Josephat Gwajima.
Mama huyu anaitwa SARAPIA, ana umri wa miaka 70, amekuwa akisumbuliwa na miguu iliyompelekea kushindwa kutembea kwa muda wa miaka 20 lakini baada ya maombezi ya mchungaji kiongozi Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameweza kuachia magongo, amepokea uponyaji. Mama huyu anamshukuru Mungu kwa kumponya.
Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, akiwa anawaombea na kuwabariki Maelfu na Maelfu ya waamini waliofika katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi katika mkutano mkubwa wa Injili wa kihistoria kufanyika katika mji wa Moshi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni