Alhamisi, 10 Oktoba 2013

JE, Kuna Usalama kwa Wakristo?


Somalia – Al-Shabaab inajulikana kama kundi la wanamgambo wa Kiislamu kupigana kwa ajili ya nafsi ya Somalia. Ni chimbuko la mtandano wa al-Qaeda. Serikali imeshindwa kukabiliana na uharamia wa kundi hili la ugaidi.
Msemaji wa Voice of the Martyrs USA Todd Nettleton. Anasema serikali ya Somalia imejaribu kila hali hivi karibuni kuandaa mkutano wa jumla ya wasomo 160 wa kiislamu, wazee na maimanu kutoka nchi za nje, kujaribu kufanya ufumbuzi wa usalama na utulivu nchini Somalia
Nettleton anasema, “Matokeo ya mwisho wa mkutano huo walitoa Fatwa dhidi ya al -Shabaab , walisema, ‘ Hawafuati uislamu ipasavyo wanavyofanya siyo uislamu haipaswi waungwe mkono”
Hii ni mara ya kwanza viongozi wa dini wamekuja na suluhisho la fatwa dhidi ya kundi lililo na nguvu vijijini.
“sisi ni wasislamu wa kweli na wale si waislamu wa kweli lazima waadhibiwe” ndiyo makubaliano yaliyotajwa na wasomi hao wa kiislamu.
Fatwa mara nyingi zinazohusiana na vitisho vya kuuawa au hukumu.
Somalia ni moja ya nchi inayojulikana duniani kwa kuwatesawakristo, Pamoja na historia ya muda mrefu ya ukandamizaji, Je hii fatwa itawasaidia wakristo kupata unafuu?
Wengi wa Wakristo Somalia wanaabudu kwa siri au makanisa ya nyumbani, al -Shabaab, wameapa kutokomeza Wakristo wote wa Somalia. Idadi ya Mauaji ya Wakristo wanaompa Yesu maisha yao inatisha. Waumini wengi wamekimbia nchi
Wakristo popote tulipo ni jukumu letu kuomba juu ya roho hii inayotaka kumaliza Ukristo, roho ya mpinga Kristo, Unaweza kuomba kwa ajili ya Somalia usisahau Tanzania na Afrika kwa ujumla ambapo lengo kuu ni kuibadili Afrika liwe bara la Kiislamu.
———————————–
Al shabab wamefanya mashambulizi Nairobi, Kenya kwenye Supermarket ya Westgate na kuua jumla ya watu 72 siku ya tarehe 22 September 2013

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni