Jumatano, 23 Oktoba 2013
NATAKA NIPATE KUONA *sehemu ya kwanza*
Mtumishi Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya...
Karibu katika mfululizo huu wa fundisho zuri kupita maelezo.
Mfululizo huu ndio kwanza umeanza siku ya leo na una DHIMA KUU ya kukufundisha KUONA KIROHO kama vile Bwana atakavyo tuwe.
Tunasoma sasa;
Marko 10 : 51
" Yesu akamjibu, akamwambia,Wataka nikufanyie nini ? Yule kipofu akamwambia,Mwalimu wangu, NATAKA NIPATE KUONA "
Haleluya...
Hiyo habari ni ya kipofu Bartimayo,
Bartimayo alikuwa ni kipofu yaani mtu asiyeweza kuona kama watu wengine waonavyo.
Na si tu alikuwa ni kipofu pekee ,Bali Bartimayo alikuwa pia ni muhitaji. Ninaposema ni MUHITAJI ninamaanisha kwamba alikuwa ni mtu MWOMBAJI.
Alikuwa ni mtu mwenye kuishi kwa kutegemea kusaidiwa mahitaji ya kila siku ,kama vile chakula,mavazi N.K
Hivyo,kwa lugha nyingine ni kwamba; Bartimayo alikuwa ni MASKINI. Mtu mwenye kulishwa na wenye mali.
Hata leo hii wapo wakina Bartimayo katika majumbani mwetu,na mara nyingi tunawapita kama vile hatuwaoni. Hawa wakina Bartimayo wa sasa tunaishi nao majumbani,makazini hata katika njia njia wapo tu.
Wapo vile kwa sababu wanahitaji sana msaada wako wewe ambaye umepewa NEEMA ya kuwa hivyo ulivyo.
Biblia leo hii inatuambia kitu cha ajabu sana ambacho sijawahi kukutana nacho.
Nami namuomba sana Mungu anisaidie niweze kukiachilia kwako kama vile Mungu alivyo kiachilia kwangu.
Biblia inatupa habari ya kutushtua,habari ya Bartimayo . Ambayo habari hii wengi tumeisoma kama vile hadithi na kudhani kwamba ilikuwa ni habari ya rahisi rahisi vile.
Sasa ona hapa;
Makutano makubwa pamoja na wanafunzi wa Yesu Kristo pamoja naye Bwana Yesu Kristo,tunaona wakishika njia kutoka Yeriko.
Na huko kulikuwa na KIPOFU. Biblia inatupa na jina la huyo kipofu kwamba anaitwa Bartimayo,ambaye mtu huyu alikuwa ameketi kuomba kama kawaida yake.
Na alikuwa akitaraji kupokea kitu kutoka katika lile kusanyiko lililopita mbele yake.
Lakini haikuwa rahisi kwa Bartimayo kuusogelea makutano hata kama walipita mbele yake.
Maana mkutano ulimsonga songa,hata baadhi ya wanafunzi wake Yesu walimzuia Bartimayo asikutane na Yesu.
Kumbe kukutana na Bwana Yesu sio jambo la rahisi kama wengine wadhaniavyo.
Ili ukutane naye ni lazima UZINGATIE MOYONI kwa kufanya maamuzi magumu,ukikubali kabisa kupoteza kila kitu ili ukutane naye.
Wengi hujifariji kwamba wamekutana na Bwana Yesu,huku kuna vitu wameshikilia kwamba HAWAJAZINGATIA MOYONI kufipoteza kwa ajili ya kumpata Bwana Yesu.
Biblia inatuambia ingawa Bartimayo alizongwa,lakini hakuacha kupaza sauti yake kwa kumuita Bwana Yesu.
Huyu Bartimayo mimi nampenda sana. Maana alikubali yote,
Alikubali kutukanwa na makutano,
Alikubali kudharauliwa na makutano,
Alikubali kuonekana MJINGA kwa ajili ya Bwana Yesu.
* Bartimayo alikuwa na AKILI za kuigwa.
Alichokitafuta Bartimayo ni KUONA tu.
Na sio apewe pesa,au msaada mwingine uwayo wote.
Alijua maana ya kuona. Na ndio maana aling'ang'ana kuona. Nasema ni KUONA tu.
Haleluya...
Jina la Bwana lipewe sifa...
Makutano kamwe hawawezi kukuruhusu hukutane na Yesu kirahisi rahisi tu.
Hata wanafunzi wa Yesu wengine hawatakubali hukutane na Bwana Yesu kirahisi rahisi tu.
Leo yapo makutano,
Leo wapo wanafunzi wa Yesu,
Hawa wote usifikiri wako upande wako vile umwitavyo Bwana Yesu ukutane naye. Watahakikisha wakikusonga songa usionane naye.
Tazama habari hiyo ya Bartimayo,jinsi alivyosongwa songwa. Kama Bartimayo
ang'elikata tamaa basi ni dhahiri kabisa asingepata KUONA.
Leo hii wajapokusonga songa kwama usikutane na Yesu,wewe ngangana tu kama vile Bartimayo alivyo ngangana.
Makanisani mwetu hivi leo,wapo makutano ya kutosha kuhakikisha hupati hata nafasi ya kuonana na Bwana.
Tena wapo baadhi ya wanafunzi wake Bwana ambao wapo makanisani,wenye kukukwamisha usikutane na Bwana Yesu.
Kundi la namna hii hufananishwa na ROHO YA NYOKA. Ambayo hipendi kuona inafanikiwa kiroho hata kimwili pia.
Ukiona una kiu ya kujifunza siri za ufalme wa Mungu,lakini gafla ukiona watu wanakukwamisha basi ujue hao ni MAKUTANO waliomkwamisha Bartimayo asikutane na Yesu.
ITAENDELEA...
*Usipange kukosa muendelezo huu.
Kwa maombezi ;
0655 111149
0783 327375
UBARIKIWE.www.mwakasegebibilia.blogspot.com
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni