Jumamosi, 12 Oktoba 2013

SIKU YA AJABU KUTOKA KWA WANA WA GUSA CHANG'OMBE


Habari ya jumapili mdau wetu wa GK, hapana shaka kwa wale wa kazi wa jijini Dar es salaam siku ya leo watapiga kambi Kijitonyama Lutheran ambako kwaya ya Uinjilisti ya kanisa hilo waliotamba na nyimbo mbalimbali kama "Hakuna Mungu kama wewe, Simba wa Yuda, Hakuna mwanaume kama Yesu na nyingine nyingi siku ya leo wanazindua album yao mpya iitwayo "Namtangaza Kristo" ikienda sambamba na jubilee yao ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa kwaya hiyo ambapo wanatarajia kuimba nyimbo mpya na zazamani.



Basi kati ya kwaya zinazotarajiwa kuwepo Kijitonyama leo ni pamoja na AIC Chang'ombe Vijana Choir(CVC) ama waite wana wa Vunja ama Gusa, kupitia kwaya hii tumekuchagulia wimbo uitwao "Siku ya ajabu" unaopatikana katika album yao mpya ya "Usiku wa manane", ni matarajio yetu kwamba utabarikiwa nao utazamapo na kusikiliza. Kumbuka Kijitonyama leo hakuna kiingilio ni bure kabisa, wapo Kijito wenyewe, AIC Chang'ombe, Upendo Nkone, Miriam Lukindo na waimbaji wengine. Barikiwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni