Ijumaa, 18 Oktoba 2013

ANGALIA JUMBA LA KIFAHARI LA ASKOFU KIUNA WA KENYA


Askofu Kiuna na mkewe.

Angalia nyumba ya kifahari ya Askofu Allan Kiuna iliyopo maneo ya Runda huko nchini Kenya, nyumba hiyo ni gumzo kutokana na uzuri wake, hasa ikiwa na huduma mbalimbali kama ilivyo kwa hoteli za hadhi ya juu, angalia picha hizi kama zilivyotolewa na mtandao wa SoftKenya.com

Askofu Kiuna anatunza kanisa kubwa la Jubilee Christian Centre (JCC) lililopo jijini Nairobi nchini Kenya,ni mume wa mchungaji Kathy Kiuna na baba wa watoto watatu. Pamoja na mafanikio yote hayo askofu Kiuna amekuwa akipitia majaribu mengi ikiwemo kuvumishiwa kwamba amegeuza nyumba ya Mungu kuwa sehemu ya biashara kutokana na utajiri wake, lakini pia kama haitoshi ametajwa kuwapa kazi vijana wenye uwezo mkubwa wa kuzungumza kiingereza ili kuvutia vijana wengi zaidi kujumuika kanisani kwake.

ANGALIA PICHA ZA JUMBA HILO LA MPAKWA MAFUTA WA MUNGU
















Hakuna maoni:

Chapisha Maoni