Jumatatu, 30 Desemba 2013

Asili hasa ya Uislamu ni nini?



Je, wewe ni Mkristo? Je, wewe ni Mwislamu? Sote tuko kwenye safari ya kuelekea mbinguni huku tukiamini kuwa njia ile tuliyomo ndiyo sahihi; na njia ile waliyomo walio kinyume nasi haiko sahihi.

Ukristo na Uislamu ni dini kubwa ambazo zinadai kuwa zinaabudu Mungu mmoja aliyeumba mbingu na nchi tofauti na dini zingine ambazo zinaabudu miungu mingi. Hata hivyo, zipo tofauti za msingi sana kati ya Uislamu na Ukristo ambazo KATU haziwezi kufanya pande hizi mbili ziwe zote sahihi. Kwa mfano:
Ukristo unaamini kuwa Yesu ni Mungu na Uislamu unaamini kuwa Yesu si Mungu. Haiwezekani kamwe Ukristo ukawa sahihi katika hili na Uislamu ukawa sahihi katika hili. Ni lazima uwe ni upande mmoja TU ulio sahihi katika jambo hili.
Hali ni hiihii katika mambo mengine mengi. Kwa mfano:
Ukristo hauamini hata kidogo kwamba Muhammad ni mtume wa Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo; lakini Uislamu unaamini hivyo.
Ukristo unaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka; lakini Uislamu hauamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka.
Ukristo hauamini kuwa kuna Mwislamu YEYOTE atakayekwenda mbinguni kwa kupitia imani ya Uislamu; lakini Uislamu unaamini hivyo; n.k., n.k.


Kwa kuwa haiwezekani pande zote mbili zikawa sahihi, lazima kuna upande uliodanganywa; na Biblia ilishaonya tangu karne nyingi kabla kwamba yuko Ibilisi audanganye ulimwengu wote. (Ufunuo 12:9).


Je, asili ya Uislamu ni nini? Hata kama wewe ni Mkristo, ni muhimu kuyajua haya maana tunao ndugu zetu wengi walio upande wa pili. Ndugu zetu hawa si kwamba hawataki kwenda mbinguni; la hasha! Mbingu wanaitaka sana. Tena wapo wengi walio na juhudi kubwa kuliko hata sisi tulio Wakristo. Lakini juhudi na nia njema huwa si jibu na suluhisho la shida yoyote. Ni lazima hizi zichanganywe na maarifa sahihi.

UTABIRI WA TB JOSHUA JUU YA KIONGOZI AFRIKA MASHARIKI KUTEKWA WATIMIA


Nabii TB Joshua
Hatimaye utabiri uliotabiriwa na mtume TB Joshua wa Nigeria mwezi Octoba mwaka huu juu ya kiongozi mkuu wa moja ya nchi za Afrika mashariki kutekwa huku akikataa kutaja jina la nchi hiyo ila akisema iko karibu na Kenya zaidi ya kuwataka watu kufunga na kuomba juu ya nchi hiyo. Hatimaye utabiri huo umetimia kwa kiongozi wa Sudan ya kusini ambako kuna mapigano kwasasa.

"UJUE ULIMWERNGU WA ROHO" na Mwl. Christopher Mwakasege

Kitabu kipya kilichotoka mwezi huu wakati wa semina ya Dar es salaam.
Katika kitabu hiki utajifunza mambo mengi yanayohusu ulimwengu wa roho katika mpangilio wa sura kumi kama ifuatavyo;
1. Kufahamu umuhimu wa kujua uhalisi wa kuwepo kwa ulimwengu wa roho.
2. Kwa njia ya maombi unaweza kuwa mahali kiroho ambapo huwezi kuwa kimwili.
3. Mtu aliumbwa aishi katika maeneo mawili kwa wakati mmoja.
4. Mungu anakukaribisa katika ulimwengu wa roho ushiriki maamuzi pamoja naye kwa njia ya maombi yako.

Jumapili, 29 Desemba 2013

MAMBO YA GLORIOUS CELEBRATION "WAKAWAKA" NDANI YA MBEYA

Usiku wa kuamkia leo kundi la Glorious Celebration ama waite "Wakawaka" kutoka jijini Dar es salaam, limefanya tamasha kubwa la kusifu na kuabudu katika ukumbi wa Mkapa Hall uliopo jijini Mbeya wakisindikizwa na Shekinah Glory Band. Hizi ni baadhi ya picha kama zilivyopigwa na John Kuyokwa.





HUYU NDIO BINTI WA MAREHEMU ANGELA CHIBALONZA, MUNGU ANAMTUNZA


Chibalonza, bintiye wa pekee baby Wonder ambaye muonekano wake anafanana na mama yake ingawa MI blogu haijajua kama atafuata nyayo za mama yake ama Mungu amempa talanta nyingine.

Picha hii ni kutoka kwa mama yake wa kufikia ama mlezi ambaye ni mke wa mtume Elisha Muliri ambaye ndiye alikuwa mume wa hayati Angela Chibalonza. Angela bado anakumbukwa na ataendelea kukumbukwa kutokana na alama kubwa aliyoacha kupitia uimbaji wake katika kumtangaza Kristo kupitia album zake mbalimbali.



Hapa Baby wonder akiwa na mama yake mdogo Tete Meshak mdogo wa Angela Chibalonza ambaye pia ni mwimbaji kama alivyokuwa dada yake. Picha ni mali ya Tete.

Hebu tumalizie mwaka kwa kusikiliza wimbo huu "Wewe ni mwema" kutoka kwake marehemu Angela Chibalonza Muliri kati ya nyimbo ambazo zinabariki kuzisikiliza kutokana na sauti, upako na mpangilio wa vyombo kwa ujumla bila kusahau maneno yake. Barikiwa

IT IS WELL WITH MY SOUL (SALAMA ROHONI MWANGU),JUA HISTORIA YA WIMBO HUU AMBAPO MWIMBAJI ALIFIWA NA WANAE WOTE..



Horatio Gates Spafford na Anna Spafford

Katika miaka ya 1860 Horatio aliishi na mke wake Anna Chicago,Marekani. Spafford alikuwa mwanasheria mkubwa aliyewekeza zaidi kwenye majengo (real estates). Maisha yalianza kubadilika mwaka 1870 ambapo mtoto wao pekee wa kiume alifariki kwa ugonjwa wa nimonia, Mda mfupi baadae janga la moto mkubwa wa Chicago uliteketeza sehemu kubwa sana ya mali zake.


Wakiwa na matumaini ya kupunguza maumivu waliyopata kutokana na matatizo yote,
Mwaka 1873 Spafford na mkewe walikubaliana kwenda Uingereza ambapo rafiki yake alikuwa ana hubiri injili.
Katika maandalizi ya mwisho kazi zilimbana Horatio, Akawaambia mke wake na watoto wake wakike wanne watangulie akiahidi kuwafuata haraka.


Ndipo jambo lisiloweza kufikirika likatokea, Boti aliyopanda mke wake na watoto wake ikapata ajali na watoto wake wote wanne walizama na kupoteza maisha, Mke wake pekee alipona nae baada ya kufika ufukweni akamuandikia note spaffors ikisema
"Saved Alone, What shall I do?" yaani "Nimeokolewa peke yangu, Nitafanya nini?"



MKRISTO KAMA SIMBA*sehemu ya mwisho*


Mtumishi Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe...
Heri ya Christmas mpendwa...

Natumaini U mzima wa afya na umesherekea vizuri sikukuu ya kuzaliwa kwa mwokozi wetu.
Karibu tena tuendelee kupata maharifa ya ki-Ungu kupitia fundisho hili.

Kuwa mkristo ni kufanyika mfuasi wa Kristo.Ikiwa na maana kwamba kama vile Bwana Yesu alivyoishi,nasi tulio wakristo yatupasa kuishi hivyo.
Yeye Bwana Yesu aliuvaa mwili kwa kutuonesha kielelezo cha namna gani mkristo aishi.

ROSE MUHANDO AWAKUNA WAKAZI WA TANGA UWANJA WA MKWAKWANI


Mwimbaji mahiri wa nyimbo za kiroho a.k.a Injili,na anaetamba na wimbo mpya wa Facebook,Rose Muhando akiwa sambamba na skwadi lake zima wakilishambulia jukwaa vilivyo jioni ya leo ndani ya uwanja wa Mkwakwani wakati wa muendelezo wa tamasha la Krisimasi lililofanyika leo Mkoani Tanga.

Ijumaa, 27 Desemba 2013

KRISMASI YA KILIO MOMBASA KENYA KANISA LALIPULIWA KWA MABOMU


Picha ya kanisa lililochomwa moto mwezi Octoba mwaka huu mjini Mombasa.©jihadwatch

Taarifa kutoka Mombasa nchini Kenya zinasema vijana wanaosadikiwa kuwa kati ya waumini wa dini ya kiislamu ama wanaounga mkono chama cha Mombasa republican council(MRC) kinachodai uhuru wa mji wa mombasa ambao wakazi wake wengi ni waislamu kujitenga na Kenya, wamechoma moto makanisa mawili mjini humo siku ya sikukuu ya krismasi kwa mabomu ya petroli.

Alhamisi, 26 Desemba 2013

MAPEPO YAGUNDULIKA KUWA VYANZO VYA MATATIZO MENGI YA WATU

Akifundisha katika Mkutano wa maelfu ya watu Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima alieleza kuwa mapepo(mashetani au majini) ndio vyanzo vya matatizo yanayowakumba watu wengi leo hii. Baada ya kufundisha kwa dakika chache Mchungaji alianza kufundisha kwa vitendo na alipoanza tu mapepo yaliyokuwa ndani ya watu mbalimbali yalidhirika na baada ya uponyaji watu hao walielezea matatizo yalikuwa yanawasumbua muda mrefu ambayo yalitokana na kupagawa na pepo waliowangia ndani yao.

Binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Amina Salum (Chini katika picha) ambaye hapo awali kabla ya kuokoka alikuwa muislamu, alikuja katika mkutano wa Ufufuo na Uzima akisumbuliwa na magonjwa mbalimbali.
Akieelezea tatizo lake, Amina alisema kuwa alikuwa na tatizo la tumbo ambalo alikuwa akisikia kuwa tumbo linachoma choma ndani kiasi cha kushindwa kula. Tatizo ambalo lilimdhoofisha mwili siku hadi siku.


Wakati Mchungaji Gwajima akipita katikati ya makutano alimkuta amekaa na mapepo yaliyokuwa ndani yake walipomuona mchungaji wakadhihirika kutokea ndani yake ambapo na baadaye yalipewa amri yamtoke mtu huyo. Baada ya hapo dada huyo alipona kabisa magonjwa yake papo hapo.


Mchungaji Gwajima akiwa amemshika Amina baada ya kupokea uponyaji wake.

WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TAMASHA LA KRISMAS WASUUZA MIOYO YA MASHABIKI UWANJA WA JAMHURI MOROGORO



Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba katika tamasha la Krismas lililofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki huo hapa nchini na mwimbaji wa kimataifa kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti wamesuuza mioyo ya mashabiki baada ya kushusha burudani ya nguvu katika tamasha hilo, Katika tamasha hilo, mashabiki wamejitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Jamhuri, Tamasha hilo linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam na linatarajiwa kuendelea mkoani Tanga Desemba 28 mwaka huu.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MOROGORO)

Mwimbaji Edson Mwasabwite akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake wakati akitumbuiza kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo jioni.

SOWETO GOSPEL CHOIR KUREJEA AFRIKA YA KUSINI BAADA YA ZIARA BARANI ULAYA


Soweto Gospel Choir ©SGC

Baada ya ziara ya takribani miezi miwili barani ulaya, kundi la Soweto gospel choir linatarajia kurejea nyumbani kwao Afrika ya kusini mwishoni mwa wiki kujiunga na familia zao kusherehekea mwaka mpya. Kundi hilo ambalo kwasasa lipo nchini Ujerumani likimalizia ngwe yake, lilikuwa katika ziara ya kusherehekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.

NASI TUMEKUJA KUMWABUDU.


PICHANI NI WANAKWAYA WA KANISA HILI LA VCC WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA MADHABAHUNI,picha na makitaba  mwanzoni mwaka huu.
                                               NA OSCAR SAMBA.
Hakika ni siku nyingine tena iliyosheheni utukufu mkuu wa MUNGU wetu wa mbinguni,Kwa jina la BWANA wetu YESU KRISTO nina kukaribisha katika makala hii inayo zungumzia Kuzaliw akwa YESU pamoja vitu muhimu vinavyo ambatana na sikuu hiyo.
Ujumbe huu umetolewa jana madhabahuni katika kanisa la VICTORY CENTRE LA TAG lililopo hapa mkoani ARUSHA eneo la kwa MOROMBO na mwalimu EZEKIELI JOSEPH kutoka jijini DR ES-SALAAM,      
Bila kupoteza muda na tutazame maandiko; MATHAYO 2:1-12.
Mpendwa ukisoma maandiko hayo utaona Yesu alivyozaliwa katika bethilehemu ya uyagudi enzi za mfaulme Herode,,Ukiendela utaona jinsi mamajusi walivyo tazama nyota na kwenda kumuona YESU pia walimtolea zawadi nyingi.

Jumanne, 24 Desemba 2013

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA HAKI-LEO OSCAR SAMBA NA SAFU YOTE YA WAFANYAKAZI NA WANAHISA WA KAMPUNI HII WANAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA CHRI-MASS NA MWAKA MPYA.

JE UNAJUA UMUHIMU WA KWENDA KANISANI JUMAPILI?


Pastor Carlos Kirimbai
MUHIMU SANA KWENDA IBADANI JUMAPILI.

Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa BWANA. (ZAB. 122:1 SUV).

Mungu aweke ndani yako hali ya kufurahia kwenda ibadani kila J2.

wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. (EBR. 10:25 SUV).

Kutokwenda ibadani kwa sababu yoyote ile sio tabia nzuri hata kidogo. Kusali peke yako, au kwa njia ya TV haijakaa poa. Uwe na kanisa ambalo unakwenda kuabudu. Uwe na mchungaji ambaye atawajibishwa na Mungu kwa habari ya ustawi wa roho yako. Uwe na mahali ambapo unalishwa ufahamu na maarifa.

HATUA SABA ZA KUIMARISHA USHIRIKA WAKO NA MUNGU.(maamuzi saba) (2)

WAKWANZA KULIA NI MCH. WA KANISA HILI LA VICTORY CENTRE ALOYCE MBUGHI NA WA KWANZA KUSHOTO NI MAMA MCH. CATHERINE MBUGHI.
Ninayo furaha ya hali ya juu kukukaribisha hususani ewe uliye mpenzi wa blogu hii ya www.mwakasegeinjili.blogspot.com,  siku ya leo kama ilivyo kuwa jana ninakuletea muendelezo wa somo la HATUA SABA ZA KUIMARISHA USHIRIKA WAKO NA MUNGU.(maamuzi saba).

Kwa uwezo wa YESU KRISTO na tumaini tutakuwa pamoja na kufanyika kazi,kabla hatuja endelea na hatua ya pili, tafadhali kama uliikosa hatu ya kwanza bonyeza link hii ili usome sehemu ya kwanza kisha ndipo uendelee na sehemu hii ya pili, http://mwakasegeinjili.blogspot.com/2013/12/hatua-saba-za-kuimarisha-ushirika-wako.html#more

Kabla ya kukujuza hatua ya pili kwanza tujikumbe mstari wetu wa kusimamia,
ZAB 27:4 Neno moja nimelitaka kwa Bwana  nalo ndilo nitakalolitafuta,nikae nyumbani mwa Bwana siku zote za  maisha yangu niutazame uzuri wa BWANA nakutafakari hekaluni mwake.

Andiko hili linatufundisha ya kwamba Daudi alilipa kipaumbele jambo hili ili atafakari uzuri wa MUNGU.
Hatua ya pili, HUUISHA JUUDI YAKO KUTAKA KUMJUA YEYE KWA UKARIBU ZAIDI.(yeye maana yake ni MUNGU, Neno kuuwisha maana yake kufufu)

Tafadhali soma name mstari huu,WAFILIP 3:10 ILI NI MJUE YEYE, NA UWEZA WA KUFUFUKA KWAKE , NA USHIRIKA WA MATESO YAKE NIKIFANISHWA NA KUFA KWAKE .

Kwa ajili ya YESU Paulo aliacha mambo ambayo yalikuwa ya mpe au yaliyomfanya aonekane kama ni mtu mwenye sifa na heshima kubwa sana kwa watu kwani alikuwa ni msomi wa hali ya juu na mwalimu wa torati na pia litoka katika kabila la Benjamini ambalo ndilo kabila la kwanza kumtoa mfalume ambae ni Sauli pia alikuwa ni mwebrani aliye kijua kiebrania.Ila kwa ajili ya Mungu aliviacha hivyo vote.

Mpendwa MUNGU hujifunua kwa mtu kulingana na kiu na shahuku aliyonayo  kwake.Wanathiolojia wanasema ya kwamba wakati Paulo antoa kauli hiyo alikuwa na mika thelathi ya kutembea na YESU KRISTO lakini bado kwake haikutosha kutokuwa na shahuku ya kuendelea kumjua MUNGU.

Paulo alihitaji kuzama ndani zaidi yaani hakutaka kuwa na uhusiano wa juu juu, ndugu msomaji siju shahuku yako ni ipi ila mtume PAULO shahuku yake ilikuwa ni kumjua MUNGU.

Katika shahuku hii yake ndipo MUNGU alijifunua kwake zaidi kwani ndie mwenye mchango mkubwa zaidi kweyne AGANO JIPYA ,,unapo soma karama tano,HUDUMA TANO ni mtume PAULO.

Hayo yote ni matunda na matokeo yake kutokakana na shahuku yake ya kumjua MUNGU,,Wanatheolojia wanasema ya kwamba katika ulimwengu alioishi PAULO hakukwepo mtu aliye mcha MUNGU kama yeye.

Laiti kama dunia ingemtafuta MUNGU kama inavvyo tafuta fedha kwani watu huamka alufajiri,huamua kuchimba madini na shuhuli ngumu ili wapate fedha ila kwa MUNGU wengi ni wavivu hadi wasukumwe, Ila PAULO hakuwa hivyo alijiwekeza kwa MUNGU zaidi.

Tuachane na ukristo wa kidini dini, tuzame ndani zaidi,Ukiwa na ushirika wa karibu na MUNGU utaitambua sauti yake .
YOHANA 10:4  NAYE  AWATOAPO NJE KONDOO WAKE WOTE,HUWATANGULIA; NA WALE KONDOO HUMFWATA KWA MAANA WAIJUA SAUTI YAKE.

Kuna mmarekani mmoja alienda mashariki ya kati na kuwakuta wachungaji wakilaza kondoo katika pango moja na inapofika asubuhi mchungaji moja huwaita kondoo wake nao humfwata na mmarekani Yule alijaribu kuvaa nguo zayule mchungaji akawaita lakini hawakuja,kwa nini ? kwa sabau hawakuijua sauti zake.
Tazama tena andiko hili,

ZAB 103:7 ALIMJULISHA MUSA NJIA ZAKE WANAWAIZIRAELI MATENDO YAKE.
Pia tembelea andiko hili,KUTOKA 33:1-10     Utaona jinsi ambavyo MUSA alivyo kuwa akishirikiana na MUNGU.,NI vizuri kuyajua matendo ya MUNGU kama wana waiziraeli, ila ni vizuri zaidi kuzijua njia zake kama MUSA.Wanahistoria wanasema ya kwamba hakujawai kutokea nabii ambae alitembea na MUNGU kama MUSA.
Musa aliijua sauti ya MUNGU haraka,,Njia za kumjua MUNGU ni kusoma NENO kwa bidii kwani unaposoma NENO MUNGU husema nawe, pia MAOMBI na KUABUDU,KUSHUKURU,KUSIFU, na pia SADAKA.

1TIMOTHEO 2.1 BASI KABLA YA MAMBO YOTE NA TAKA DUA,
DUA ni maombi ya kusihi.
SALA ni mazungumzo kati yako na MUNGU. Kukemea sio maombi kwani maombi ni yale ambayo yanaelekea kwa MUNGU.
MAOMBEZI, ni pale unapo ombea kanisa,nchi mtu au sehemu Fulani pia SHUKURANI ni maombezi.

Hatuwezi kumjua MUNGU pasipo NENO, MUNGU wetu anaishi katika NENO.Lazima uwe na kawaida ya kulisoma NENO kila uchwao.
Unapo endelea kumsogelea MUNGU hautahitaji maombi kwani yataondoka yenyewe kwani MUNGU wetu ni moto ulao, kwenye moto mende na nzi hawasoge.

Tatizo la wakisto wanataka kuishi leo kama enzi za agano la kale kwani zamani watu wache ndio waliokuwa wakiingia kwenye PATAKATIFU-PATAKATIFU ila toka pazia lipasukuke pale YESU akiwa msalabanii sasa kila mtu anayo haki ya kumwendea MUNGU wetu.

Tutazame kitabu cha,
DANIELI 11:12  NA WALE WAMJUAE MUNGU WATAKUWA HODARI NA WATENDA MAMBO MAKUU.
Maana yake watu wasiomjua MUNGU wao hawawezi kuwa hodari na hawataweza kufanya mambo makuu,Danieli alipitia nyakati Ngumu lakini alishinda kwani alimjua MUNGU wake,Danieli alikuwa ni mtu wa maombi hata pale walipo tafuta makosa kwake waliyakosa hadi ikabidi wayatafute kwa ushirika wake na MUNGU wake; ilibidi wa mtupe kwenye simba.Simba hawezi kumtafuna mtu mwenye ukaribu na MUNGU.

Unaweza kuishi kama mfalume utumwanai kama unamjua MUNGU,
Ujumbe huu umetolewa leo madhabahuni katika kanisa la VICTORY CENTRE LA TAG lililopo hapa mkoani ARUSHA eneo la kwa MOROMBO na mwalimu EZEKIELI JOSEPH kutoka jijini DR ES-SALAAM,      

LANGU JINA NI OSCAR SAMBA, nimeokoka na ninampenddaa YESU WEWE JE?
Kama bado basi ungana nami kwenye sala hii kisha utaokoka kumbuka kuokoka sio dini mpya bali ni mwanzo mpya na MUNGU WETU ALIYE MBINGUNI , tuanze sasa;
“Ee MUNGU WANGU ULIYE MBINGUNI MIMI NI MWENYYE DHAMBI NA MIMESIKIA HABARI ZAKO NA KUZIAMINI EWE YESU NI SAFISHE KWADAMU YAKO NA UNIKOWE”
Ongera kwa kuokoka na sasa tafuta kanisa la walokole linalo hubiri injli iliyo hai,siku njema na endelea kuifwatilia blogu hii ya www.mwakasegeinjili.blogspot.com
                       SIKUKUU NJEMA


TAARIFA YA KUBADILISHWA JINA KWA BLOGO YA MWAKASEGE BIBILA NA KUITWA www.mwakasegeinjili.blogspot.com

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA HAKI-LEO OSCAR SAMBA AMBAYO NDIYO INAMIKI BLOGU MBALIMBALI IKIWEMO YA MWAKASEGE INJILI AMBAYO HAPO AWALI ILIITWA MWAKASEGE BIBILIA ANAWATANGAZIA RASIMI YA KWAMBA BLOGU HIYO SASA ITAITWA MWAKASEGE INJILI NA KUWA NA ANUANI www.mwakasegeinjili.blogspot.com

HATUA HIYO IMEFIKIWA BAADA YA ANUANI YA AWALI KUWA NA UKAKASI NA KUWAFANYA ADHIRA KUTOKUIPATA KWA URAHISI.

PIA  SAMBA ANAWAOMBA RADHI SANA KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAO JITOKEZA.

Jumatatu, 23 Desemba 2013

HATUA SABA ZA KUIMARISHA USHIRIKA WAKO NA MUNGU.(maamuzi saba)

Wa kwanza kulia ni Catherine Mbughi ambae ni mama mchungaji na wa kwanza kushoto ni ALOYCE MBUGHI ambae ndie Mchungaji wa kanisa hili la TAG VICTORY CHURCH,wengine ni watoto wao.
Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha ewe mteule wa MUNGU wetu aliye mbinguni katika makala hii, ambayo inalenga kukujuza na kukuhabarisha njia kuu saba ambazo zitakusaidia kuimarisha mahusiano yako na MUNGU.
Ujumbe huu umetolewa leo madhabahuni katika kanisa la VICTORY CHURCH LA TAG lililopo hapa mkoani ARUSHA eneo la kwa MOROMBO na mwalimu EZEKIELI JOSEPH kutoka jijini DR ES-SALAAM,       KARIBU SASA.
Mstari wa kusimamia.
ZAB 27:4 Neno moja nimelitaka kwa Bwana  nalo ndilo nitakalolitafuta,nikae nyumbani mwa Bwana siku zote za  maisha yangu niutazame uzuri wa BWANA nakutafakari hekaluni mwake.

IBADA MAALUMU YA KRISMASI LUTHERAN JIJINI LONDON KATIKA PICHA

Hapo jana imefanyika ibada maalum ya sikukuu ya Krismasi katika kanisa la St. Anne's Lutheran lililopo jijini London nchini Uingereza na kuhudhuriwa na watu zaidi ya mia moja kutoka Afrika mashariki ambao makazi yao yapo nchini humo. Ibada hiyo iliyoambatana na ubatizo wa mtoto mmoja iliongozwa na askofu Jane akisaidiwa na mchungaji mwenyeji aliyeongoza ibada hiyo Tumaini Kalaghe pamoja na mchungaji Moses Shonga. Baada ya ibada waumini wote walijumuika kwa pamoja kupata chakula kusherehekea Krismasi.



Kwaya ya vijana Anoint ya kanisa hilo ikimsifu Mungu.


Masomo ya Krisimas yalisomwa.



Jumamosi, 21 Desemba 2013

Tutafakari juu ya Yesu Kristu, Ukristu

IMEANDIKWA NA GAZETI LA TANZANIA DAIMA LA LEO.
NIANZE makala hii kwa kuwatakia wasomaji wangu heri ya Krismasi na Mwaka Mpya wenye baraka tele.

Ni miaka mitatu sasa nimeachana na utamaduni wa kutumiana salamu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani; msimamo wangu ni kukwepa kuzitajirisha kampuni za simu wakati wa sikukuu hizi za mwisho wa mwaka.

Wale wote watakaonitumia ujumbe kwenye simu, nitaupokea, lakini sitaujibu, badala yake najibu kupitia makala hii: Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuturuhusu kuendelea kuwepo; si kwa ubora wetu bali kwa neema zake.

Hivyo basi, kwa vile tumejaliwa bure bila hata kustahili, tuelekeze nguvu zetu zote katika upendo, amani na kuwahudumia jirani zetu.

Nitakayoyaandika leo, inawezekana nilikwishayaandika miaka iliyopitia. Nitakuwa ninayarudia kama ilivyo kawaida yetu ya kurudia mambo yale yale kila mwaka.

Mfano tukio hili la Krismasi tunalirudia kila mwaka na bila kuwa waangalifu tunaweza kujikuta tunatumbukia kwenye mnyororo wa kufuata ratiba bila kuwa na tafakuri.

Hatari ya kujenga utamaduni huu ni siku moja kujikuta hatuna majibu ya maswali mengi yanayoweza kujitokeza kutokana na matukio haya tunayoyarudia kila mwaka. Hivyo katika makala hii kama nitakuwa nimejirudia, si kwa bahati mbaya bali ni kutaka kujenga utamaduni wa kuyatafakari matukio haya ambayo yamegeuka kuwa ni sehemu ya maisha yetu.

MKRISTO KAMA SIMBA.*sehemu ya kwanza*


Mtumishi Gasper Madumla. NA GK

Bwana Yesu asifiwe...

Nasema;

Haleluya…

Karibu katika fundisho hili ambalo limekujia katika muda na wakati sahihi kabisa.

Leo nimemfananisha mkristo kama Simba,nami ninakuita wewe uliye mkristo ni Simba.

Ijumaa, 20 Desemba 2013

NAMNA YA KUONGEZA IMANI UNAPOKUWA KWENYE JARIBU


Mpenzi msomaji Shalom,
Naomba sana radhi kwa Mungu na kwako pia kwa kuchelewa kuweka masomo tangu mwaka huu uanze. Kuna baadhi ya majukumu yalinibana sana, namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuyamaliza vema na sasa nitaendelea kuweka masomo kama kawaida. Katika mwezi huu wa Januari nimeona ni vema tuanze na ujumbe huu wa imani ambao naamini utafanyika msaada kwenye maisha yako.

IJUE NA KUITUMIA NAFASI YAKO KAMA MLINZI KWENYE ULIMWENGU WA ROHO

Na: Patrick Sanga Shalom.

Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana Mungu kwamba leo nimeweza kumalizia sehemu ya mwisho ya ujumbe huu maalum ambao nililazimika kuugawanya katika sehemu sita tofauti. Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha katika hili na kwa ajili yako wewe msomaji kwa kutenga muda wako kuusoma na zaidi kuniombea. Naam karibu sasa tumalizie sehemu ya mwisho ya ujumbe huu wa pekee…

Alhamisi, 19 Desemba 2013

MOTO WA INJILI UNAWAKA MAJUMBASITA, WANAFUNZI WASHUHUDIA

NA GOSPLE KITAA

Mchungaji Moses Maghembe.
Mungu azidi kujidhihirisha katika mkutano wa injili Afrika kumepambazuka ulioandaliwa na kanisa la T.A.G Majumbasita chini ya mchungaji Moses Maghembe. Mkutano huo ulioanza tarehe 8 mwezi huu unatarajiwa kumalizika tarehe 29 ukiongozwa na kichwa kisemacho "Yesu ni yeye yule jana leo na hata milele". Wahubiri katika mkutano huo uliofunguliwa na mchungaji Abdiel Mshashi kutoka mkoani Kilimanjaro na kupokewa na mwenyeji mchungaji Moses Maghembe ambaye atampisha askofu Elia Lugwami kumalizia ngwe.

Jumatano, 18 Desemba 2013

NIFANYE NINI ILI KUSHINDA TAMAA ZA MWILI?



Na: Patrick Sanga

Septemba mwaka huu, Mwanafunzi mmoja wa shule ya Sekondari alinitembelea nyumbani kwangu hapa Dodoma. Alipofika nilimkaribisha ndani nikajua amekuja kunisalimia tu. Baada ya muda akaniambia kaka Sanga nina swali nahitaji msaada wako sana. Tukatoka nje mahala penye utulivu ndipo akaniambia tamaa za mwili kwa maana ya uasherati/zinaaa zinanitesa nifanye nini ili kushinda? Jambo hili linanitesa kiasi kwamba nahisi kama vile sijaokoka kutokana na vita niliyonayo katika fahamu zangu na mwilini mwangu?

MISUKULE WAENDELEA KURUDISHWA KATIKA MKUTANO WA UFUFUO NA UZIMA

Ikiwa ni siku ya tatu ya mkutano wa Ufufuo na Uzima mjini Morogoro maelfu ya watu waliendelea kuhudhuria huku uweza wa Mungu wa namn aya ajabu ukiendelea kudhihirishwa kupitia mchungaji Josephat Gwajima

Mchungaji Josephat Gwajima alifundisha somo la NYOTA YAKO INATUMIWA NA MTU. Akifundisha alisema kila mtu anayo nyota katika maisha yake au kipawa ambacho Mungu ameweka ndani yake ili kupitia hiyo aweze kufanikiwa

Lakini wachawi na waganga wa kienyeji wanakua na uwezo wa kuichukua nyota ya mtu na kuitumia kwaajili ya kazi zao binafsi, akielezea mtu aliyechukuliwa nyota ana dalili zipi, mchungaji Josephat Gwajima alisema unakuta kwa mfano mtoto alikua ana akili darasani lakini baada ya kuchukuliwa nyota yake unakuta ule uwezo wote unaondoka na anakua hawezi tena kufanya vile vitu alivyokua anafanya mwanzoni.

Baada ya kufundisha mchungaji Josephat gwajima alianza kuomba maombi ya kuwarudishia watu nyota zao na baada ya hapo aliwarudisha wale waliokua wamechukuliwa msukule.




Jina:Rose Mwakipesile
Anaishi mzumbe alichukuliwa na wachawi na wakampeleka kariakoo ambako alikua akitumiwa na wachawi kufanya biashara kariakoo ya nguo na alisikia sauti ikimuita njoo akajikuta yuko mkutanoni

MCHAWI ANASWA KATIKA MKUTANO WA UFUFUO MOROGORO


Ikiwa ni siku ya tatu ya mkutano wa ufufuo na uzima unaoendelea katika viwanja vya vya shule ya sekondari ya morogoro mchawi mmoja aliyejulikana kwa jina la Fatuma amekamatwa katika mkutano huo akiwa yuko katika shughuli zake za kila siku za kichawi.
Dada huyo aliyekamatwa na Nguvu za Mungu alielezea akasema alikuwa na wenzake ambao walitumwa na bosi wao ambaye ni mchawi na mganga wa kienyeji maarufu kutoka mjini Bagamoyo wilaya ya pwani kuja katika mji wa Morogoro kuchukua miili ya watu waliokufa katika nyumba za kuhifadhia maiti za hospitali(mochuari) kwa ajili ya kitoweo.

NAMNA YA KUONGEZA IMANI UNAPOKUWA KWENYE JARIBU

Na: Patrick Sanga


Mpenzi msomaji Shalom,

Naomba sana radhi kwa Mungu na kwako pia kwa kuchelewa kuweka masomo tangu mwaka huu uanze. Kuna baadhi ya majukumu yalinibana sana, namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuyamaliza vema na sasa nitaendelea kuweka masomo kama kawaida. Katika mwezi huu wa Januari nimeona ni vema tuanze na ujumbe huu wa imani ambao naamini utafanyika msaada kwenye maisha yako.

Biblia katika kitabu cha Mathayo 17:18 inasema‘..Ni kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana amini nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. Hii ni habari ya yule kijana aliyekuwa na pepo bubu na kiziwi, mzazi wake akamleta kwa wanafunzi wa Yesu wamwombee. Biblia inatueleza kwamba wanafunzi walijaribu kumtoa yule pepo wasiweze, wakati huo Yesu alikuwa amepanda Mlimani kwenda kuomba.

JIFUNZE KUMILIKI MAJIBU YA MAOMBI YAKO.

Yoshua 13:1-7

Utangulizi,

Katika dunia ya leo watu wengi sana wamekuwa wakitumia muda wao mwingi ikiwa ni pamoja na kufanya maombi ya kufunga na kuomba ili kumuomba Mungu awabariki, awaponye, awalinde kwa kifupi awajibu mahitaji yao waliyonayo mbele zake siku zote. Wapo waliokuwa hawazai wamezaa, vipofu wameona, wasioajiliwa wameajiliwa, biashara za wengi zimefanikiwa, ndoa nyingi Mungu ameziponya, wapo waliotaka kuolewa au kuoa na Mungu amewapa waume na wake wazuri.

Jumatatu, 16 Desemba 2013

HAYA NDIO YALIYOJILI KATIKA MKUTANO WA INJILI,DAR KITUNDA-RELINI


Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya...

Kumbe watu wanamuhitaji sana Bwana Yesu katika maisha yao tofauti na vile tunavyofikilia.
Nasema hivi; Wapo watu wengi sana wanaomuhitaji Bwana Yesu.
Kama utakuwa ni mtu wa kanisani tu kila siku huwezi kuyaelewa haya nisemayo, ni mpaka uwe na spirit/roho ya kuhudhuria mikutano ya nje ya injili,jaribu siku moja uhudhurie katika mikutano ya nje,mikutano ya injili na utadhibitisha hili nisemalo kwamba wapo watu wanamuhitaji Bwana Yesu sana kuliko vile unavyofikilia.

Ijumaa, 13 Desemba 2013

MWANAMKE ANAYESAKIKA KUWA NI JINI AIBUKA NA KUTOWEKA MKUTANO WA MCH. GWAJIMA - JIJINI TANGA



Mkutano mkubwa wa Ufufuo na Uzima na mchungaji Josephat Gwajima umehitimishwa kwa tukio la aina yake lililosisimua watu waliohudhuria mkutano huo. Ni tukio la ajabu kutokea ikiwa ni siku moja tu mara baada ya mkutano wa Ufufuo na Uzima kuhamia katika jengo moja maarufu mkoani Tanga.


Pamoja na kufundisha kuhusu misukule, nyota, ndoto na kuhusu wafu; Mchungaji Gwajima alifundisha pia kuhusu majini na jinsi ya kuwashinda ambapo alisema wazi kuwa majini ni viumbe ambavyo ni vya rohoni na vinaweza kuvaa umbele lolote la binadamu au mnyama.
Akinukuu hay ya kitabu cha Shehe Falsihi wa zanzibar alisema "majini ni viumbe vya angani ambavyo havina viwiliwili hivyo huwezi kuviona kwa macho, lakini vinaweza kuvaa ima umbo la kifuu cha nazi au umbo lolote" alisoma haya hiyo akieleza kuwa uislamu na ukristo wote unataja viumbe hivi yaani majini.



Wakati somo likiendelea kukatokea jambo la ajabu ambalo kwa tafsiri ya rohoni ilikuwa ni uthibitisho wa kile ambacho Mchungaji Gwajima amekuwa akifundisha katika jiji hilo la Tanga.


Mchungaji Gwajima alipokuwa akizunguka katikati ya makutano ili kuwafungua wenye vifungo, zilisikika kelele za watu zikipiga kelel kuwa kuna mtu amevaa ushungi yupo kwenye kona ya bati. jambo ambalo lilivuta hisia za wengi. Kwani mwanamke huyo alionekana na watu wote akiwa kwenye bati la nyumba moja ya ghorofa pembeni mwa jengo la kuabudia.


Watu waliokuwepo wakiwa wanamshangaa muda mfupi kabla hajatoweka.. (Ghorofani amezungushiwa rangi)




Ni kweli kuwa kwa ghorofa lile hakuna ambaye angeweza kupanda, wala kukaa kule juu na ukizingatia ni mwanamke. Watu wakiwa wametaharuki na wengine kuliitia jina la Bwana ghafla mwanamke huyo akatoweka mbele ya macho ya watu wote na kuweka hofu miongoni mwa watu wote.

MWILI WAKO NI HEKALU LA MUNGU


Conrad Conwell.
Mwili wako ni Hekalu la Mungu!
Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe.

AMBWENE MWASONGWE AACHIA VIDEO YA MISULI YA IMANI


Hatimaye baada ya kusubiri kwa muda mrefu video ya Ambwene Mwasongwe imeanza kupatikana jana baada ya kukamilika kwake. Video hiyo iliyobeba jina la "Misuli ya Imani" audio yake imetokea kupendwa na kuwavutia wengi hasa jumbe zilizomo katika nyimbo hizo ambazo zimejaa matukio ya kweli yanayowatokea watu.


Ambwene Mwasongwe Mwasongwe
10 hours ago via mobile
Video ya misuli ya Imani tuliyoingoja muda mrefu sasa iko madukani kuanzia Leo! Napenda kukushukuru kwa maombi yako na naamini ile nguvu ya Mungu iliyokuwa katika nyimbo hizo itakugusa na kukuhudumia! Karibu tubarikiwe site.Ambwene ambaye alitoa video ya kwanza ya Majaribu ni mtaji, alikuwa kwenye mpango wa kutoa album mbili za video kwa pamoja ikiwa ni toleo lake la pili na la tatu ambapo ameamua kuachia kwanza toleo la tatu ambalo lilikuwa likiuliziwa na watu wengi hasa kukiwa na nyimbo kama Upendo wa kweli, Misuli ya imani, Natamani na nyingine nyingi.

Jumatano, 11 Desemba 2013

WEZI WAVUNJA NYUMBANI KWA ASKOFU DESMOND TUTU AKIWA MSIBANI


Askofu mkuu mstaafu wa kanisa Anglikana Afrika ya kusini, Desmond Tutu ©standard

Polisi wamesema wizi huo ulifanyika wakati bwana Tutu akiwa katika ibada ya Nelson Mandela Mjini Johannesberg.
Aidha wameelezea kuwa uvamizi ulifanyika nyumbani kwake mjini Cape Town Ahamisi jioni baada ya kutoa hotuba katika ibada ya Mandela siku hiyo.Inaarifiwa Tutu aliibiwa vitu vyake wakati akiwa anahudhuria ibada maalum ya kumuaga Hayati Nelson Mandela siku ya Jumanne.
Ibada hiyo ilifanyika katika uwanja wa FNB mtaani Soweto.
Wizi na uvamizi wa nyumba za watu ni jambo la kawaida nchini Afrika Kusini ambako visa vya uhalifu viko juu sana.
Chanzo BBC SWAHILI

KWA TAARIFA YAKO : JE UNAJUA KWANINI FLORA MBASHA ANAAMBATANA NA MUMEWE KILA MAHALI?

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Jumatatu, 9 Desemba 2013

SHAMRA SHAMRA ZA MIAKA 25 YA KWAYA YA UINJILISTI KIJITONYAMA ILIVYOFANA


Kijitonyama Lutheran .

Jana ilikuwa jubilee ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama Lutheran jijini Dar es salaam, jubilee hiyo iliyokuwa ya aina yake ilihudhuria na mamia ya washarika wa kanisa hilo, waimbaji wasasa na wazamani, wageni waalikwa, ndugu jamaa na marafiki wa kwaya hiyo, ikiwemo kwaya ya Tumaini Shangilieni Arusha ambao kazi yao ilikuwa njema.

Kati ya matukio ya kupendeza ilikuwa ni uzinduzi wa nembo mpya ya kwaya hiyokusikia historia jinsi kwaya hiyo ilivyoanzishwa, kwaya ya Tumaini kuimba wimbo wa Naburudika wa Kijito huku wenyeji nao wakiimba wimbo wa Hakuna Mungu kama wewe ulioimbwa na Tumaini katika album yao iliyopita.

SOMO:KUWAFYEKA WATUNZA KUMBUKUMBU


Utangulizi
Kwenye biblia shetani anaitwa mshitaki wa ndugu. Ufunuo 12:10. "Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.".1Petro 1:8

Jumamosi, 7 Desemba 2013

NENO : KUONA NJAA, KUSHIBA , KUWA NA VINGI NA KUPUNGUKIWA


Mtumishi Gasper Madumla.
Tusome WAFILIPI 4 : 12-13

‘’ Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. ‘’

MOROGORO KUTIKISWA NA UFUFUO NA UZIMA

Baada ya mikutano iliyovunja rekodi kwa idadi ya watu yaani Arusha, Moshi na Tanga; sasa kanisa la Ufufuo na Uzima linahamishia mikutano yake mkoani Morogoro ambapo Mchungaji Gwajima ambaye pia ni mchungaji kiongozi wa kanisa hilo anatarajiwa kuhubiri kwa siku nane mfululizo.

Pamoja Mchungaji Gwajima atafuatana na timi ya watendakazi zaidi ya mia tatu na waimbaji maarufu wa injili kama Flora Mbasha, John Lisu, Jackson Benty na Mwanamapinduzi Band.


Mkutano huo wa kwanza kufanyika Morogoro kwa kanisa la Ufufuo na Uzima unatarajiwa kushuhudia misukule wakirudi, wagonjwa kupona, viwete kutembea na mambo mengine mengi ya ajabu.


Usikose kuhudhuria na wewe ili kupokea muujiza wako.

Dady Gwajima

JOYOUS YAMUOMBA DRUMMER WAO WA ZAMANI AREJEE KUNDINI KUOKOA JAHAZI


Siyabulela Sabu Satsha.©Sabu Facebook page.
Kundi la Joyous Celebration limeamua kumuomba mpiga ngoma(drum) wake wa zamani Siyabulela Satsha kurejea kundini, ili kuwasaidia kuwapigia ngoma katika rekodi yao ya DVD ya 18 inayotarajiwa kufanyika tarehe 20 na 21 mwezi huu katika kanisa la City Hill lililopo Durban Afrika ya kusini.

Alhamisi, 5 Desemba 2013

JE UNALO JAMBO LA IMANI LITAKALO MGUSA MUNGU,WAKATI WA KUFA KWAKO ? * sehemu ya mwisho*


Mtumishi Gasper Madumla.


Nakusalimu mpendwa katika Jina la Bwana;
Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya...

Ni matumaini yangu U mzima wa afya siku ya leo,Nami ninakukaribisha tushiriki pamoja kujifunza mambo ya msingi kwa habari ya maisha yetu ya kila siku.

Mkristo yakupasa uwe na mambo ya IMANI utakayoyaacha kama ALAMA katika kipindi ambacho hautakuwepo hapa chini ya jua,
Au katika kipindi cha hatari ya kufa kwako,ambapo ALAMA hiyo itakusaidia kwa kukuongezea muda wa kuishi.