Jumatano, 1 Januari 2014

TUNAJIFUNZA NINI KWA HABARI YA LAZARO ALIYEFUFULIWA NA BWANA YESU.


Mtumishi Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe....
Haleluya....

Kupitia Biblia maandiko matakatifu,wapo Lazaro wawili tuwasomao.
Lazaro wa kwanza ni yule aliyekuwa muombaji,mtu aliyekuwa akiwekwa mlangoni mwa tajiri mmoja,akishibishwa kwa makombo,mtu aliyekuwa maskini. (Luka 16:19-31).

Lazaro wa pili ndio yule ambaye alikuwa hawezi na baadaye akafa. Huyu alikuwa ni mkazi wa Bethania,mwenyeji wa mji wa Mariamu.Lazaro huyu alikuwa pia mfuasi wa Kristo Yesu,pia alikuwa rafiki wa Bwana Yesu Kristo.Kupitia habari za Lazaro huyu wa pili,ndio nataka tujifunze kidogo.

Wengi wetu tulishasoma habari zake Lazaro kipitia kitabu cha Yoh.11:1-44
Lakini si wote wenye kuelewa fundisho la Lazaro.
Lakini leo ipo Neema ya pekee mahali hapa ya kujifunza zaidi kwa habari hii.
Yapo mengi ya kujifunza kupitia habari ya Lazaro,nasi tutajifunza kwa kadri ya Roho apendavyo.

Biblia inatuambia yakwamba Lazaro alikuwa mkazi wa Bethania,ambapo neno
BETH ni neno lenye asiri ya kiebrania lenye maana NYUMBA(House)

Pia na neno,
..ANIA.. Ni neno lenye asiri ya kiebrania lenye maana YA KIMASKINI (of poor)
Hivyo ukiyaunganisha maneno haya,utapata hivi;
BETHANIA=Nyumba ya kimaskini(the house of poor)
Au ukanda wa kimaskini.
Kwa maelezo haya inaonesha Lazaro alikuwa akiishi sehemu duni,sehemu yenye hali ya kiumaskini,sehemu yenye hali ngumu kiuchumi.Hivyo yawezekana hata yeye mwenyewe alikuwa ni maskini.

"Basi mtu mmoja alikuwa hawezi,Lazaro wa Bethania,mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha,dada yake."Yoh:1

Haleluya...

Jambo moja la kwanza tunalojifunza hapa kwa habari hii ya Lazaro ni ;
*URAFIKI KATI YA LAZARO NA BWANA YESU.

Tunasoma;
"Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema,Bwana,yeye umpendaye hawezi."Yoh.11:3

Neno "yeye umpendaye "huwakilisha urafiki kati ya Bwana Yesu na Lazaro.Lazaro alikuwa ni kipenzi cha Bwana Yesu ingawa alikuwa sio miongoni mwa mitume.Kwa lugha nyingine ninaweza kusema kwamba Lazaro alikuwa na mahusiano makubwa na Bwana Yesu.
Na ndio maana wale maumbu walipomuona Lazaro amekuwa hawezi,mtu wa kwanza kumfuata alikuwa ni Bwana Yesu,achilia mbali na kumuamini Bwana Yesu kwamba ndiye mwenye nguvu za Mungu pekee,Bali pia alifuatwa kwa sababu Lazaro alipendwa na Bwana Yesu.

*Katika urafiki kuna penzi.
Penzi lililopo kati ya rafiki na rafiki lina nguvu sana.

Pale Bwana Yesu alipopewa taharifa ya rafiki yake Lazaro,hakuona shida kufunga safari na kumuendea.
Ni kama vile wewe ukipewa tahari ya ugonjwa juu ya rafiki yako basi ni dhahili kabisa utafunga safari na kwenda kumjulia hali.

Tazama vizuri ile taharifa iliyotolewa na maumbu zake Lazaro kwake Bwana Yesu,Wale maumbu hawakuhitaji wamueleze saana Bwana Yesu juu ya ugonjwa wa Lazaro kana kwamba wamvutie kwa maelezo yao ili Bwana Yesu aende pamoja nao,la hasha !
Haikuwaa hivyo.

Bali wao walimueleza Bwana Yesu kwa ufupi tu,Lakini kwa sababu ilikuwepo nguvu ya pendo kati yake Lazaro na Bwana Yesu,nguvu ile ikamsukuma Bwana Yesu kurudi Uyahudi tena,maana Bwana Yesu alikuwa huko Uyahudini na wanafunzi wake,ilimbidi arudi tena.

Tunasoma;
"Kisha,baada ya hayo,akawaambia wanafunzi wake,twendeni Uyahudi tena.Wale wanafunzi wakamwambia ,Rabi ,juzi juzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe,nawe unakwenda huko tena? Yoh.11:7-8

Sio rahisi kwa mtu kuweza kurudi sehemu ambayo watu walitaka kumpiga mawe,juzi juzi tu.
Ipo nguvu iliyokuwa imekamata moyo wa Bwana Bwana Yesu.

Jina la Bwana liinuliwe...
Haleluya...

Ooh,kumbe unapofanyika rafiki na Bwana Yesu,ujue yakwamba ipo nguvu ya pendo itakayokamata moyo wa Mungu,kiasi kwamba itamfanya Bwana Yesu akurudie tena na kukuponya.

Wayahudi walikuwa wakitafuta kumpiga Bwana Yesu kwa mawe huko Uyahudini,lakini Yesu hakuangalia hayo yote,Bali Yesu alimuangalia Lazaro.

Bwana Yesu hakuangalia juu ya kupigwa kwa mawe,
Bwana Yesu hakuangalia uchovu wa safari ya kurudi Uyahudini,
Bwana Yesu hakuangalia yapi yatakayompata huko Uyahudini.
Bali aliangalia jambo moja tu,nalo ni Kuyafanya mapenzi ya Baba aliyempeleka.

Hali hiyo kama ingejitokeza Leo hii kwa wapendwa,je tung'efanya kama Bwana Yesu alivyofanya kwa Lazaro?

Chukulia unapewa taharifa ya ugonjwa wa mpendwa mwenzako,alafu eneo alipo huyo mgonjwa ni eneo ambalo watu wake walitaka kukupiga kwa mawe juzi juzi tu.
Swali kwako,;
Je utarudi katika eneo hilo?

*Mungu atusaidie sana,tupone katika eneo hili.

Kati ya jambo la msingi litupasalo kulifanya ni kujenga urafiki na Bwana Yesu.Kama Lazaro alivyofanya.

"Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro" Yoh.11:5

Bwana Yesu asifiwe...

Hivyo jambo moja tunalojifunza kwa habiri ya Lazaro ni kuwa na Mahusiano mazuri kati ya Lazaro na Bwana Yesu.

Ukiwa na mahusiano mazuri na rafiki yako,basi ni dhahili mtakuwa na mawasiliano ya mara nyingi.
Mara nyingi utaongea naye kumjulia hali yake,
Mara nyingi utakubali kulipa gharama yoyote itakayo jitokeza juu yake . NK

Lazaro alikuwa na Bwana Yesu mara kwa mara,walikuwa na urafiki ndani yao,hivyo ikamfanya Bwana Yesu ampende.

Nami ninakuambia ya kwamba ukitaka kupata mpenyo katika maisha yako ,basi huna budi kufanya urafiki na Bwana Yesu.
Kwamba yakupasa uzungumze naye mara kwa mara,siku zote,kwa njia ya maombi,ujae neno lake kwa wingi.

Tazama tena jambo jingine tunalojifunza hapa kwa habari ya ugonjwa wa Lazaro.Biblia haikutuambia ni ugonjwa gani aliokuwa nao Lazaro ,lakini inatueleza vizuri sana nini walifanya ndugu zake lazaro,pale alipokuwa hawezi.

Tunasoma ;
"Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema,Bwana,yeye umpendaye hawezi." Yoh.11:3

Lazaro alipokuwa hawezi,maumbu zake wakagundua kwamba yupo YESU WA NAZARETI mwenye kuweza. Waliona uwepo wa Bwana katika ile shida ya ndugu yao.
Wakaamua kumuendea BWANA YESU.

Hapa napapenda sana,maana hakuna jambo zuri kama kujua jibu la tatizo lako.
Maumbu hawa wanatufundisha kwamba
Upatapo tatizo,ugonjwa,msiba umkimbilie Bwana Yesu Kristo maana Yeye ndio njia,kweli na uzima...

ITAENDELEA...

*Kwa huduma ya maombezi;
0655-111149.

UBARIKIWE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni