Katika orodha iliyotoa, shirika hilo limeonyesha nchi ambazo wakristo wanaishi kwa kujificha, manyanyaso, kutekwa lakini pia wakiwa katika hatari ya kuuwawa na serikali za nchi hizo ama vikundi hatari vya dini vya watu wenye msimamo mkali wa dini.
Hii ni listi ya nchi hatari zaidi duniani kwa wakristo kuishi, ambao hadi Tanzania kushika '50 bora', basi hakika hilo ni jambo la kuombea kwa nguvu zote, na kama hufahamu, Baraza la Makanisa ya Kipentekoste nchini limeshatangaza maombi ya kufunga na kuomba kwa siku 40 kuanzia Januari 6, hili ni mojawapo ya jambo linalostahili kushughulikiwa.

Taarifa za nchi tano duniani ambazo ni hatari zaidi kwa wakristo kuishi ni kama ifuatavyo;
1. NORTH KOREA/KOREA KASKAZINI
Ni kosa la jinai kuwa mkristo au kushiriki katika shughuli za za Kikristo
Katika vizazi vitatu mpaka sasa mmoja kati ya wanafamilia kuna uwezekano wamefungwa kwa kosa la kumiliki Biblia.
Takribani wakristo 70,000 wapo gerezani wakitumikishwa kwa shughuli mbalimbali
2. SOMALIA
Wakristo wanahusishwa kushirikiana na upande wa mataifa ya kikoloni yenye nguvu ya Ulaya
Imependekezwa adhabu ya lifo kea mtu kuwa mkristo
Kutokana na ukosefu wa serikali makini fujo zinazoletwa na vikundi vinavyopinga ukristo vinapewa nguvu na majeshi ya nchi.
3. SYRIA
Makumi elfu wamekuwa wakihama makazi kutokana na vitisho na vurugu
Takribani 50-60,000 ya wakristo katika mji wa Homs wameondolewa
Makanisa mengi yamelipuliwa.
4. IRAQ/Iraki
Idadi ya wakristo wanaoishi kwenye mateso inazidi kuongezeka toka vita ya kwanza ya Juba mwaka 1990
Ongezeko la vitendo vya utekaji nyara, vitisho na mauaji tokea vita ya Gulf mwaka 2003.
Asilimia 25 tu ndio wakristo sawa na idadi ya mwaka 1990
5. AFGHANISTAN
Serikali imetoa vitisho vya adhabu ya kifo kwa yeyote atakayeacha Uislamu
Kuna wakristo 1,200 nchi nzima
Hakuna makanisa.
PATA IDADI KAMILI KIDUNIA BONYEZA HAPA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni