Jumatatu, 27 Januari 2014

NILIITWA MWANAMKE MBAYA KULIKO WOTE DUNIANI, LAKINI UZURI UPO NDANI YANGU -- LIZZIE


Mwanadada Lizzie Velasquize (24) mzaliwa wa Texas Marekani ambaye ameitwa majina na maneno mbalimbali mabaya kutokana na watu kudai ni mwanamke mwenye muonekana mbaya zaidi duniani amesema uzuri upo ndani ya mtu na si nje kama wengi wanavyodhani.
Lizzie ambaye toka amezaliwa alikosa virutubisho vinavyomfanya ashindwe kunenepa amesema amelelewa vizuri sana na wazazi wake bila ya kuonyeshwa ubaguzi wa aina yeyote ama kuonekana ana kasoro kwa wazazi wake ama kuwa tofauti na watu wengine. Amesema wazazi wake walimwambia atembee akiwa ameinua kichwa (tofauti na alivyokuwa akiinamisha kichwa chake) hali itakayowafanya watu kujua kwamba naye ni mtu kama walivyo watu wengine.

Lizzie akiwa katika matembezi na rafiki zake.
Lizzie amesema alikuwa akiomba na kutamani kwamba siku moja ataonekana watofauti kama watu wengine. Amekuwa akipata sapoti kubwa sana kitu ambacho kimemsaidia sana kuwa hapo alipo hii leo, aliambiwa kuwa ingawa wakati mwingine mambo yanakuwa magumu tofauti na alivyotarajia lakini hiyo isiwe kitambulisho cha namna alivyo.

Amesema siku moja video iliwekwa kwenye mtandao ikipewa kichwa cha "mwanamke mbaya zaidi duniani"na kusoma ujumbe chini ya video hiyo ikisema ajiue kwa kujipiga risasi kichwani kwake kitu kilichomliza kwa siku nyingi lakini akakumbuka udhaifu huo si ukweli wa jinsi alivyo kama mtu. Mwanadada Lizzie ameamua kuhakikisha malengo na mafanikio yake yatamtambulisha yeye ninani na kutumia ubaya unaosemwa juu yake kama kichocheo cha kusonga mbele. Kwasasa amemaliza chuo na kuwa mtu wa kutia hamasa na kubariki maelfu kupitia mazungumzo na historia yake. Huku pia akiwa ameandika baadhi ya vitabu.

Mwanadada huyo amewatia moyo watu wengine kutumia udhaifu unaonenwa juu yao kama kichocheo cha kufanikisha malengo yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni