Jumamosi, 18 Januari 2014

BALOZI AWAONGOZA WATANZANIA NCHINI UINGEREZA KATIKA IBADA KUIOMBEA MAFANIKIO NCHI YAO


Kiongozi wa kanisa la Worldchangers mtume Mathew Jutta akimsifu Mungu kanisani hapo.
Waumini kutoka sehemu mbalimbali za jiji la London nchini Uingereza walikutanika jumapili iliyopita maeneo ya kusini mashariki mwa jiji la London kuombea mpenyo na mafanikio kwa mwaka mpya wa 2014 kwa Taifa la Tanzania chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kiwete,maombi ambayo yaliandaliwa na kanisa la Worldchangers ministries chini ya mtumishi na mwanzilishi wake mtume Mathew Jutta na kuhudhuriwa na balozi wa Tanzania nchini Uingereza mheshimiwa Peter Kallaghe.

Ibada ilifanyika Abbeywood south East London,akizungumza katika ibada hiyo mheshimiwa Peter Kallaghe aliwaasa watanzania kuombea, umoja na ushirikiano, Amani na maono ya mtanzania kufikia malengo yaliyopangwa. Ibada hiyo ambayo ilisimamiwa na neno kutoka kitabu cha 2 Nyakati 7:14-18 "ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao".

Ibada hiyo ambayo ilianza kwa kipindi kizuri cha kumsifu na kumwabudu Mungu kupitia waimbaji ambao walikuwa wamejiandaa kupaza sauti zao za sifa kwa Mungu, pia zilihudhuriwa na Askofu Dkt. Ernest Irungu, Mchungaji Ben and Flora Maira, Mchungaji Allan Wilson, Nabii Elineema Gibongwe na bwana Vicent Gibogwe, Mchungaji Moses Shonga, pamoja na mchungaji Tumaini Kallaghe ambao wote walichukua muda kuwatia waumini changamoto ya kuukaribisha mwaka wakiwa na mikakati ya kufanikisha yote waliyoyaomba.



Mtume Jutta hakuwa nyuma kuyasimulia matendo makuu ya Mungu.


Meza kuu ikiongozwa na mheshimiwa balozi Kallaghe wakipiga makofi mbele za Mungu.


Balozi wa Tanzania nchini Uingereza mheshimiwa Peter Kallaghe akizungumza na waumini.


Baadhi ya waumini waliohudhuria.


Mmoja kati ya wachungaji akizungumza.


Kucheza na kusifu mbele za BWANA maana fadhili zake ni za milele.



Hakuna na hata kuwepo kama Yeye.


Ni kuimba tu, Mungu mwenyewe hukaa katika sifa.


Mke wa mtu Jutta katikati akiwa na waimbaji wenzake wakimsifu Mungu.


Sehemu ya maakuli nayo ilitayalishwa vyema.




Hakika mambo yalikuwa safi katika kanisa la Worldchangers ministries. ©Blandina Andy Kilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni